Daily Talk

Daily Talk Content Publisher

26/10/2025

Kuza page Follow Timber TZA

20/10/2025

Follow page Timber TZA

12/10/2025

Kwa mtaji wa 50K fanya biashara hizi mkoani Mara anza leo ufanikiwe
1. Togwa
2. Maziwa
3. Nyama choma+Kichuri
4. Mahindi ya kuchoma/kuchemsha
5. Karanga mbichi (Mafuta ya Bunduki)
6. Uji wa Mtama
7. Dagaa wa kukaanga
8. Miwa
9. Viazi na mihogo
10. Ndizi mbivu

03/10/2025

Follow Timber TZA

20/09/2025

Furaha yetu sio pesa
Timber TZA|| 📸

Powered by MHE. JUMANNE SAGINI

20/09/2025

Ukweli ni kwamba ni ngumu sana kwa mwanamke kuishi na mtoto ambaye hakumzaa yaani mtoto wa mume wake, mwanzoni ataonesha kumpenda ila anapitia maumivu makali moyoni. Ukioa mkoani Mara ni tofauti kwani mwanamke mwwnyewe ana upendo na watoto wa mume wake hivyo anatafuta watoto wa mume wake ili aishi nao nyumbani kwa upendo.

20/09/2025

BAISKELI ZA KUBEBEA ABIRIA

Ukifika Mikoa ya Kanda ya Ziwa hasa kwa wasukuma ni kawaida kukutana na wanawake kwa wanaume wakifanya biashara za kuendesha baiskeli kwa ajili ya kubeba abiria kutoka eneo moja hadi lingine.

Baiskeli hizo hupambwa kwa midoli, taa pamoja na stika za kuvutia wateja, huku nyuma kukiwa na kiti kikubwa chenye kava nzuri ili kisimuumize au kumchosha mteja akiwa amekaa katika safiri ya muda mrefu. Huku bango likiwa nyuma ya taili kama kama ya uyaonayo kwenye magari.

Utafurahia safari yako endapo ukikuta mko wengi ambao mmepanda usafiri huo, kwani wamiliki wa vyombo hivyo huwa hupenda kuendesha wakiwa sambasamba wakipiga stori za hapa na pale kwa kabila lao.

Nakumbuka nilibahatika kufika kufika mikoa ya Geita, Simiyu na Mara nikakuta kwenye taa za barabarani ambazo zinaonesha ishara ya kusimaa, nilishuhudia kuona basikeli ni nyingi kuliko magari zinasubiria taa ziruhusu.

Pia utafurahi kukutana na kundi la wanawake wakiendesha baiskeli hizo huku wakiwa na watoto mgongoni wakitoka au kulekea kliniki au sokoni.

Bei ya usafiri huu inategemeana na umbali unako elekea wakati mwingine unaweza kuchajiwa hata ukubwa mwili ulonao hapa namanisha uzito ulionao.

Hata hivyo kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu hapa nchini mara nyingi baadhi ya wagombea hupaki magari yao na hutumia usafiri wa baiskeli. Lengo likiwa kujishusha kwa wanaomba kura pamoja pia kumrahisishia katika kumfikia mpiga kura wake.

20/09/2025

WAZANAKI NA VITUNGO (MICHEPUKO)

Mzee wa Kizanaki anapokaribia nyumbani kwake baada ya giza kuingia huanza kuimba kwa sauti ya juu wimbo unaojulikana kama kibanziko.

Kwa desturi ni wimbo unaoimbwa na mzee ambaye amekunywa pombe kidogo, na madhumuni ya wimbo huu ni kuwafahamisha watu wote watakaomsikia kuwa mzee mwenye nyumba anarudi nyumbani.

Mwanaume yoyote ambaye anaweza kuwa nyumbani kwa huyu mzee na ambaye hawezi kutoa maelezo ya kuridhisha kwanini yuko pale atafahamu kuwa ni wakati wa kuondoka haraka. Kila mzee wa Kizanaki ana kibanziko chake.

Mzee wa Kizanaki na heshima zake hawezi kumvizia mkewe kwa madhumuni ya kumfumania. Ni tabia ambayo haikubaliki.

Hata hivyo haina maana kuwa zama zile watu hawakufumaniwa. Enzi za ukoloni wale walioshikwa kwenye fumanizi walidhalilishwa hadharani kwa kuvuliwa nguo, kuchapwa bakora, na kutozwa faini ya ng'ombe kuanzia wawili. Tofauti ilikuwa mtemi anapokuwa ndiyo mlalamikaji; yeye aliruhusiwa kupanga faini aliyoona inastahili.

Kibanziko kina madhumuni mengine ya ziada. kwa kawaida, tendo lile haramu lilifanyika kwenye vichaka, mbali na nyumba ya wenye ndoa.

Ilikuwa ni fedheha kubwa kwa mwanaume Mzanaki anapofumania nyumbani kwake. Kwa hiyo, kwa namna nyingine, uimbaji wa kibanziko ilikuwa ni njia ya kuzuia hiyo aibu na kumsababisha huyo 'mwizi' aondoke na kuepusha aibu ndani ya jamii.

Yawezekana kuwa desturi hii ya kuwapa upenyo hawa 'wezi' inatokana na tamaduni ile ya kupanga ndoa. Mzee huyo huyo ambaye jana aliimba kibanziko alipokaribia nyumbani kwake yawezekana alikuwa amepitia kwenye kilabu cha pombe na kufanya makubaliano na mzee mwenzake kuwaoza watoto wao.

Aliporudi nyumbani alimwambia mwanae wa kiume kuwa umewadia wakati wa kufunga ndoa na kuwa ameshamtafutia mchumba anayefaa ambaye anatoka kwenye familia ya wachapakazi hodari ambao hawana historia ya magonjwa ya kurithi, na kuwa siyo wachawi.

Lakini kabla ya kupangiwa hizi ndoa na wazee yawezekana kuwa hao wanandoa watarajiwa walikuwa tayari wana mahusiano na watu tofauti.

Na yawezekana kwa kutambua uwezekano huo kuwa mtu anapolazimishwa ndoa ambayo hakuitaka anaweza akawa na mahusiano mengine ya pembeni, basi jamii ya Kizanaki ikaja na kibanziko kama njia ya kuruhusu yale ambayo yalifungwa na ndoa za kupangawa na wazee.

Kuna msemo wa Kizanaki unaoashiria kukubali hali hii unaosema, wiguru na wiyasi, ukimaanisha kuna yule wa juu na yule wa chini; kuna mume, na kuna mviziaji - kuna mume (au mke), na kuna kitungo.

Kwa kawaida kitungo ndiyo alikuwa mchumba ambaye angeolewa iwapo kijana angeruhusiwa kuchagua, lakini hakuweza kumuoa huyo kwa sababu ya ndoa ya kupangwa na baba mzazi. Na kwa sababu ndoa aliyopanga mzazi haikuwa na majadiliano kilichotokea ni kuwaunganisha watu wawili ambao walikuwa hawana upendo baina yao.

Matokeo yake ni kuwa walikuwa na mahusiano kama maadui badala ya wanandoa. Mwanaume alimuamrisha mwanamke ndani ya nyumba na mwanamke, kwa hulka, alikuwa mkaidi. ahueni ilitafutwa kwa kitungo.

Na lugha ya kitungo ilikuwa tamu, ya kubembeleza. Walitumia majina ya wapendanao kama 'Nyababiri', Nyabasasaba' au 'Nyabanane' majina yenye kumaanisha 'wa pili', 'wa saba', 'wa nane' na majina ambayo siyo rahisi kutumika baina ya wanandoa.

Kama ilivyo kwa mila na desturi nyingi, kibanziko nacho kinapotea na nyakati. Leo hii vijana wanarudi majumbani mwao bila taarifa. Yawezekana pia kuwa hawana uwezo wa kuimba kama wazee wa Kizanaki.

Follow Timber TZA

https://www.facebook.com/share/p/17DkSVZHDL/
03/09/2025

https://www.facebook.com/share/p/17DkSVZHDL/

FAHAMU KUHUSU MAUAJI YA MGARANJABO MUSOMA

Zinapigwa Stori mbili kuhusu jambo hili.
Stori rasmi na Isiyo rasmi.

Nianze na isiyo rasmi.

2005
Katika mtaa wa MGARANJABO ,wilaya ya MUSOMA walipita vijana watatu kutokea maeneo ya ZANAKI wakiwa wamebeba nyama za NUNGUNUNGU walizotoka kuwinda kwenye vijiji vinavyozunguka maeneo yale.

KAWAWA KINGUYE akawashuku wale vijana kuwa ni wezi wa mifugo yao inayoibiwa kila mara. Vijana wale wakajitetea kuwa wao sio wezi bali ni wawindaji. Katika kuthibitisha kuwa wao ni wawindaji wakachunguza viroba vyao kuonyesha nyama ya Nungunungu waliyopata mawindoni.

KAWAWA KINGUYE hakuamini utetezi wao bali alipandwa na Munkari akapiga MWANO kujulisha wakazi wengine kuwa kuna wezi kwa sauti ya juu. Wakajitokeza kina "mura" wakiwa na mapanga. Ndani ya dakika tano wale vijana wakawa wamechanganyikana na nyama waliyowinda.

Haikujulikana ipi nyama ya nungunungu na ipi ni nyama za wale vijana watatu. Hata baiskeli wazokuwanazo, haikujulikana ipi ni pedali na ipi ni spoketi. Vijana wale waliuwawa ugenini kinyama kabisa.

Wakati wanaendelea kuwakatakata, akatokea jirani wa "mpiga mwano" alishuhudia haya ambaye tutakuja kuona uhusika wake kwenye mkasa huu mbeleni

STORI RASMI
Mnamo tarehe 27 October 2005, KAWAWA KANGUYE aliibiwa mbuzi 25 kwake Mugarabajo, Msoma mjini. Bwana KAWAWA KANGUYE aliwapigia mwano wa wizi vijana watatu ambao walikuwa eneo la tukio. Wananchi wenye hasira wakatoka na kuwaua. Mmoja aliyeuwawa aliitwa FRED MGAYA

Baada ya tukio hili ndugu wa FRED MGAYA wakajenga chuki na familia ya KAWAWA KANGUYE na walinuia kulipa kisasi dhidi ya familia ya KAWAWA KANGUYE.

Ilipita miaka minne na watu waliamini hali ile imepoa.

Hawakujua....Hawakujua📍

MAKABURI KAMA MATUTA

Usiku wa huzuni tarehe 16 Februari mwaka 2010 ambapo watu 17 waliuwawa kikatili na watu wasiojulikana wenye siraha za kijadi (mapanga na mikuki) walivamia eneo lililokuwa na nyumba tatu za familia moja mtaa wa MGARANJABO eneo la BUHARE wilaya ya MUSOMA

Nyumba ya kwanza, mali ya KAWAWA KANGUYE KANGUYE iliyokuwa ikikaliwa na watu 10, Waliuwawa watu 8 akiwemo mtoto aliyekadiriwa kuwa na miezi 7 au 8

Nyumba ya pili mali ya MORIS MGAYA, waliuwawa watu 6 na mmoja kujeruhiwa.
Nyumba ya tatu mali ya DORICA MGAYA waliuwawa watu Watatu na sita kuponea chupuchupu.
Ingawa tukio hilo liliacha walionusurika na unyama huo ili kuja "To tell a Tale",Hakuwepo hata mmoja aliyewatambua wauaji

Tetesi pekee kuhusu wahusika wa mauaji haya ilipatikana kutoka kwenye maelezo ya mtoto mdogo KULWA KAWAWA (mmoja wa wanusurika katika nyumba ya KAWAWA KANGUYE). Binti huyu KULWA alitoa maelezo yake kwa Detective Constable DC JAVILA

Kwenye maelezo yake kwa DC JAVILA ,ambaye alikuja kuwa shahidi wa kwanza wa jamuhuri kwenye kesi hii(PW1) Kulwa alieza kuwa,Siku ya tukio alimsikia baba yake akimuuliza mmoja wa wauaji "DIWANI MBONA UNANIUA"?

Hata hivyo,Pamoja na maelezo haya,hakuna yeyote aliyemjua "DIWANI"

Askari polisi walipofika eneo la tukio, walikunaliana ni kwa matumizi ya mbwa mwenye mafunzo tu,ndipo wataweza kuwabaini wahusika wa unyama ule.
Hivyo aliletwa mbwa mwenye mafunzo(Tracer Dog No. 1495) aliyekuwa akidhibitiwa na STAFF SERGEANT HASHIMU
Mbwa akanusishwa eneo la tukio

Kisha Mbwa alimwongoza Assistant Superintendent of police ASP KAKOKI(alikuja kuwa shahidi wa tatu PW3)pamoja na askari wengine umbali wa kilomita tano.

Walimfata kwa nyuma mbwa ambaye alipita watu wengi tu mitaani.

Walipofika kijiji cha NYENGINA walikutana na Mwanaume akiendesha baiskeli huku akiwa amempakia mtoto wa kiume.

Mbwa alimrukia mwanaume yule kumaanisha uwepo wake kwenye eneo la tukio.

Mtu huyu alikuja kuwa mtuhumiwa wa pili na jina lake aliitwa ALOYCE NYABASI NYAKUMU aka DIWANI.

Kwenye mahojiano aliyofanyiwa na Detective Corporal DCPL OBEID, mtuhumiwa huyu akamtaja JUMA MGAYA(alikuja kuwa mtuuhumiwa wa kwanza)

Kazi ya kumkamata JUMA MGAYA alikabidhiwa Detective sergeant DSGT LAURENT ambapo alibaini JUMA MGAYA amekimbilia SHINYANGA.

Kwa mbinu za kipelelezi JUMA MGAYA alikamatwa SHINYANGA na akasafirishwa kwenda mkoni Mara ambapo ASP KAKOKI(PW3) alimpokea katika kituo cha Police Bunda.

Mtuhumiwa huyu JUMA MGAYA wakati wa mahojiano aliwataja NYAKANGA WAMBURA BIRASO(3rd Accused),KUMBATA BURUHAI(7th Accused),SADOKI IKAKA aka NYABUGIMBI NYAKUMU na wengine ambao nao walikamatwa.

Pia JUMA alipopekuliwa nyumbani kwake walikuta panga na mkuki vilivyohusishwa na tukio.

Nyumbani kwa mtuhumiwa NYAKANGA WAMBURA(3rd Accused),baada ya upekuzi uliosimamiwa na ACP NELSON SUMARI(PW7)walikuta Magodoro mawili ya Tanfoam,simu ya Nokia C 1200 na shati la blue vilivyoaminika kuibiwa eneo la tukio.

Pia kulifanyika upekuzi nyumbani kwa KUMBATA BURUAI(7th Accused)uliosimamiwa na SSP KIBONA(PW9) ambapo walikuta suruali nyeusi,track suit ya bluu,Jacket na shati la jeupe lenye maandishi "Paradigm" navyo vikihusishwa na eneo la tukio.

Upekuzi kwa watuhumiwa wengine haupata kitu.

Vitu hivi vilivyopatikana kwenye upekuzi vilichukuliwa kama vizibiti.
Vizibiti hivi vilichukuliwa na Assistant Inspector SIMKOKO(PW10) na kupelekwa kwa mkemia wa serikali.

Kwenye ofisi ya mkemia,kazi hii alikabidhiwa GLORIA MACHUMVE(PW23)

GLORIA alifanya FORENSIC DNA PROFILING TEST kwa kulinganisha DNA samples zilizopatikana eneo la tukio,Damu za majeruhi,mate(buccal swabs)ya majeruhi na ndugu zao,Vitu vilivyopatikana kwenye upekuzi wa watuhumiwa,mate na damu za watuhumiwa n.k.

Miaka nane baadae, watuhumiwa 16 kwa pamoja, walisomewa makosa 17 ya mauaji ya watu 17 kinyume cha sheria ya makosa ya jinai namba 196 na 197 sura ya 16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002.

Kesi hii namba 56 ya mwaka 2018 ilikuwa maarufu kama MAUAJI YA MGARANJABO

Wakati wa kusikilizwa na kuhairishwa kwa kesi hii,watuhumiwa saba walifia mahabusu hivyo kubaki watuhumiwa tisa tu.
Upande ma jamuhuri ulisimamisha mashaidi 23 na vielelezo 44 ambabyo ni vizibiti na nyaraka mbalimbali(maungamo ya kukiri kosa,DNA reports n.k)

Jopo la mawakili wa jamuhuri liliongozwa na WALLACE MAHENGA na YESE TEMBA huku Jopo la mawakili tisa wa utetezi liliongozwa na wakili msomi OSTACK MULIGO.

Katika kesi hii jamuhuri ilijenga kesi yake kwa kutoa mlolongo tangu matumizi ya mbwa kumpata mtuhumiwa mmoja hadi mwingine.

Ni katika kesi hii tulishuhudia mbwa akiletwa mahakamani kutoa ushaidi jambo ambalo lilizua hoja mbalimbali za kisheria kuwa mbwa hataweza kuhojiwa ushaidi wake

Shaidi wa 23 wa jamuhuri ambaye ndiye alifanya uchunguzi wa mahakama alielezea mahakama matokeo ya uchunguzi wake.

Alieleza jinsi Cover la godoro ka Tanfoam(Exhibit no. 44) lililopatikana kwa mshtakiwa wa tatu NYAKANGARA WAMBURA lilipofanyiwa DNA PROFILING majibu yalifanana na samples zilizochukuliwa kwenye nyumna ya marehemu KAWAWA KINGUYE

Pia alieleza DNA sample za Mkuki na panga vilivyopatikana kwa mshatakiwa wa kwanza JUMA MGAYA zilifanana na samples zilizochukuliwa kwenye nyumba ya MORIS MGAYA.

Upande wa mashtaka ulimaliza kuweka kesi yake mbele ya mheshimiwa Jaji na sasa ukafata upande wa utetezi kuweka hoja mezani.

1.Kuhusu kula njama kutenda kosa, washtakiwa (kasoro ndugu wawili) walikana kabisa kujuana kabla ya tukio bali walijuana rumande wakshtakiwa kwa kesi hiyo.

Kutokana na hili walipinga vikali hoja za upande wa mashtaka kuwa walikuwa na kikao walichopanga awali ili kutekeleza kisasi. Inawezekana vipi kwa watu msiojuana kupanga kikao?

2.Pia walijitetea kwa ALIBI. Alibi ni utetezi unaegamia kukana kuwa eneo la tukio wakati wa tukio.

Hapa kila mtuhumiwa alikana kuwa alikuwepo kwenye mji wa MGARANJABHO usiku wa tukio. Wengine walidai walikuwa Bunda,Wengine Mwanza na wengine Sirali siku ya tukio. Yaani kila mtu alijitahidi kutema ndoano

3.Pia walikana hati zao za maungamo(Extra judicial statements) kuwa zilichukuliwa kwa njia ya mateso na kulazimishwa kusaini nyaraka hizo.

4.Pia washtakiwa wawili(wale ndugu) walijitetea wakati wanakamatwa walikuwa MINORS (of the age below majority)

Ndugu hawa walisema haki zao kama watoto zilikiukwa na waliwekwa kwenye kesi sawa na watu wazima.

5.Utetezi ulitoa hoja kukwa kilikuwa kuna udhaifu katika kuweka kumbukumbu za vizibiti. Kizibiti cha godoro kilitajwa na shaidi wa police ni No 44 huku mkemia akikitaja No 29.

Katika vizibiti utetezi ulitia shaka uvhukuaji wa vizibiti kwani kuna jacket lilichukuliwa kwa kuwa lilikuwa na damu lakini mikuki na mapanga yasiyo na damu nayo yalichukuliwa kama vizibiti

Hoja nyingine ilikuwa utembeaji wa vizibiti toka mtu hadi mtu(CHRONOLOGICAL HANDS) washatakiwa walikana kutambua vizibiti vilivyoletwa mbele ya mahakama wakidai ndio mara ya kwanza wanaviona pale.

Ilijengwa hoja ya IDENTITY kuwa polisi waliwapa washtakiwa majina yasiyo yao. Mfano mshtakiwa wa pili anasema alikamatwa na kuambiwa yeye ndie anaitwa DIWANI wakati halitambui jina hilo.

Kiufupi kesi iliunguruma mpaka na kuna kipindi iliendeshwa kwa mtandao wakati wa janga la Corona. Hukumu ilikuja kutolewa Januari 15, 2021 ambapo washtakiwa sita walikutwa na hatia na kuhukumiwa Kifo. Watatu waliachiwa baada ya kutotiwa hatiani.

Address

Butiama

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Daily Talk posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share