Habari Motomoto

Habari Motomoto 3habari na matukio mbalimbali yaliyotokea duniani kote

KUTOKA MTANDAONI
26/12/2021

KUTOKA MTANDAONI

Desmond Tutu afariki dunia akiwa na umri wa miaka 90Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini, ambaye ni mshindi wa Tuzo ya A...
26/12/2021

Desmond Tutu afariki dunia akiwa na umri wa miaka 90

Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini, ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 90.Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza tanzia hiyo leo akimtaja Askofu Tutu k**a kiongozi aliyekuwa dira ya kimaadili ya nchi hiyo. Ramaphosa amesema kifo hicho ni ukurasa mwingine wa majonzi kwa taifa hilo wakati likimuaga kiongozi huyo wa kizazi maalum cha ukombozi wa Afrika Kusini.Tutu alituzwa Tuzo ya Amani ya Nobel kufuatia mapambano yake yasiyo ya vurugu dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi mnamo mwaka 1984.Hata baada ya kuangushwa kwa utawala wa ubaguzi wa rangi, mpiganiaji uhuru huyo aliendelea na harakati zake akikosoa mapungufu ya tawala za Afrika Kusini na visa vya ukiukwaji wa haki za binaadamu popote duniani.Yeye ndiye alinzisha neno maarufu la “Rainbow Nation”, yaani taifa la rangi ya upinde wa mvua, akimaanisha Afrika Kusini wakati Nelson Mandela alipokuwa rais wa kwanza mweusi nchini humo. Credit DW

Address

Buza

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Habari Motomoto posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share