27/08/2026
Nimeishi na mke wangu kwenye nyumba tuliyojenga pamoja miaka mitano sasa na kuna mdogo wake wa k**e alikuja tukaishi nae hapo vizuri tu
Siku moja mimi nikawa nimeenda kijijini kwa baba na mama kuwasalimia siku nataka kurudi mama na wadogo zangu wawili waliniambia kuwa watakuja kututembelea
Mimi k**a utani nikampigia simu mke wangu nikamwambia andaa chumba cha wageni mama na wadogo zangu nakuja nao wanakuja kukusalimia
Baada ya kuongea na mke wangu nikakata simu lakini mama akasema hawataenda na mimi, wao watabaki waandae pia na zawadi za kumpelekea mwenga wao
Mimi nikiwa safarini kurudi nyumbani simu yangu ikazima chaji nikawa nimefika usiku sana nyumbani kiasi kwamba nikakuta mke wangu na mdogo wake wamelala
Kwasababu nilikua na funguo nikaamua kuingia bila kuwaamsha nikawa nimepitiliza mpaka chumba cha wageni nikakuta chakula kimeandaliwa
Mimi nikala kwasababu nilikua na njaa na nilivorudi sebleni nikakuta chakuka kingine inaonekana ndo kilikuwa chakwangu nikawa nimekiacha hapo
Cha ajabu nikiwa nimelala nikasikia mke wangu ananyenyuka kwa kunyata akijua nimesinzia na mimi nikataka nijue anafanya nini nikaona anaelekea kwenye chumba cha wageni
Alivyofika mlangoni akachungulia hakuona mtu akaingia na kukagua chakula alichokua amekiacha hakukikuta nikaona amekuwa na hofu akamuamsha mdogo wake
Anamuuliza k**a ndo kala kile chakula na yeye akakataa mke wangu akaogopa mimi nae nikataka nijitokeze kuuliza shida nini ghafla nikadondoka chini k**a mzigo
Asubuh napata fahamu nipo hospital majibu yanakuja inaonekana nimekula chakula cha sumu sasa nashindwa kumuelewa mke wangu alikuwa na lengo gani
Nawaza nimfukuze au nimuache tu tuendelee na maisha nichukulie tu k**a changamoto za ndoa?