Tree Tv Online

Tree Tv Online Fuatana nasi kwa Habari za Uhakika

21/03/2025

RAIS DKT. SAMIA AKIMPONGEZA RAIS MTEULE WA NAMIBIA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimpongeza Rais Mteule wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah mara baada ya kuhutubia hafla ya uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya nchi hiyo Windhoek tarehe 21 Machi, 2025. Mhe. Rais Nandi-Ndaitwah ni Rais wa kwanza Mwanamke kuchaguliwa katika Taifa hilo la Namibia

RAIS MWINYI:NI WAJIBU KUANDAA JAMII YENYE MAADILI NA HOFU YA MUNGURais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ...
10/03/2025

RAIS MWINYI:NI WAJIBU KUANDAA JAMII YENYE MAADILI NA HOFU YA MUNGU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ni wajibu kuandaa jamii yenye maadili na hofu ya Mwenyezi Mungu.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo wakati wa fainali za Mashindano ya 24 ya Kuhifadhi Quran Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Aisha Sururu Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam tarehe 9 Machi, 2025.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kazi kubwa imefanyika kuwaandaa vijana kuwafundisha kukihifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu (Quran).

Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameahidi kushirikiana na wadau mbalimbali kufanikisha kuanza kwa ujenzi wa Kituo cha Taasisi ya Aisha Sururu Foundation cha Mafunzo ya Quraan na ufundi stadi katika eneo la Kiparan'ganda , Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza Taasisi ya Aisha Sururu Foundation kwa kuendelea kuyaandaa mashindano ya Kuhifadhisha Quran hadi ngazi ya Taifa kwa kushirikisha washiriki kutoka Mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Vilevile kwa kuweka mazingatio maalum ya kuwasaidia wajane na watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupitia Taasisi hiyo.

Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi ametumia fursa hiyo kuziomba Taasisi mbalimbali na watu wenye uwezo kusaidia kufanikisha shughuli za kidini ikiwemo za Kuhifadhisha Quraan ili kuzidi kuuimarisha Uislamu na kupata fadhila nyingi kwa Mwenyezi Mungu.

Washindi mbalimbali wa mashindano hayo ya kuhifadhi juzuu 3, 5, 10, 20 na 30 wamepatiwa zawadi za fedha taslimu.

TANGA YAJIPANGA KUTEKELEZA NDOTO YA RAIS SAMIANDOTO ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kuirejesha Tanga ya viwanda, in...
08/03/2025

TANGA YAJIPANGA KUTEKELEZA NDOTO YA RAIS SAMIA

NDOTO ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kuirejesha Tanga ya viwanda, inaendelea ‘kukuna vichwa’ vya viongozi na wakazi wa mkoa huo, ili kuifanikisha kwa maslahi mapana ya nchi na watu wake

Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC)kimekutana chini ya Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga ,Balozi Dkt Batilda Buriani kimeibua hoja kadhaa ikiwemo ya namna ya kufikia ndoto ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyoielezea Februari 28,2025 kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga

Hoja ya ukuzaji viwanda inaibuka kwenye kikao hicho kutokana kuwa sehemu ya Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2025-2026 kwa Fungu 086 la Mkoa wa Tanga yaliyowasilishwa kwenye RCC hiyo

Mbunge wa Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu amesema miongoni mwa malighafi zinazopaswa kutiliwa mkazo katika mipango ya kiuchumi mkoani humo ni mazao ya mifugo,kilimo na uvuvi.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amesema wakati Tanga ikirejeshwa kuwa ya vieanfq,ipo haja ya kuwekeza katika uzalishaji wa mighafi za viwandani ili kuwepo umiliki wa jumla wa umma kayika uendeshaji wa sekta hiyo

Amesema katika kipindi cha miaka miwili ,handeni imepata viwanda vinne vya madini aina ya graphites vikiwemo vya kampuni ya in and Out inayozalisha Tani 150 na viwili vya mfanyabiashara Godmwanga , kimojw kikizalisha tani 200 na kuingiza mapato ya shilingi bilioni 60

Pokeaaaa
08/03/2025

Pokeaaaa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akijumuika na viongozi kwenye Iftar aliyowaandali...
08/03/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akijumuika na viongozi kwenye Iftar aliyowaandalia viongozi wa dini, wazee wa Mkoa wa Arusha pamoja na  makundi mbalimbali katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Arusha tarehe 08 Machi, 2025.

📍Mwanza▪️CDF JACOB MKUNDA AIFARIJI FAMILIA YA PRIVATE JOHN NYEWATA JIJINI MWANZAMkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jener...
08/03/2025

📍Mwanza

▪️CDF JACOB MKUNDA AIFARIJI FAMILIA YA PRIVATE JOHN NYEWATA JIJINI MWANZA

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda amefika Jijini Mwanza kwaajili ya  kuifariji familia ya Private John Nyewata aliepoteza maisha Januari 27 mwaka huu wakati alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya kurejesha amani iliyopotea Mashariki mwa Congo.

Jenerali Mkunda amefika kwenye familia hiyo Ijumaa Machi 07, 2025 kwaajili ya kuwapa mkono wa pole kwaniaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu.

Amesema Jeshi la wananchi la Tanzania linamajukumu ya msingi ikiwemo ulinzi wa amani,kusaidia nchi jirani ambazo amani imeteteleka.

Amesema kunavikundi vingi ambavyo viko nje ya nchi hii kwaajili ya kutekeleza suala la ulinzi, kunakikundi ambacho kiko Lebanoni ambayo iko inje ya Afrika, kunakikundi kipo Afrika ya kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na vingine viko Msumbiji.

“Kijana wetu alitumwa na Taifa kwenda kuwasaidia majirani zetu kurejesha amani walioipoteza lakini katika jitihada za kuitafuta amani hiyo alishambuliwa na kundi la waasi wa M23 Mashariki mwa Congo na mwili wake ulipumzishwa kwenye nyumba yake ya milele Februari 13 mwaka huu Mkoani Mara”, Amesema Jenerali Mkunda

Aidha, ameeleza kuwa Tanzania imekuwa na utaratibu wa kusaidia nchi za jirani tangu enzi za muasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwa upande wake Baba Mzazi wa Private John Nyewata, Nyewata Kibwe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwanamna anavyoendelea kuwafariji katika kipindi hiki cha majonzi.

📍Chamanzi,Dar es Salaam▪️VIJANA WENYE ELIMU YA DINI NI NGUZO MUHIMU YA MAENDELEO-MAJALIWA WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa a...
08/03/2025

📍Chamanzi,Dar es Salaam

▪️VIJANA WENYE ELIMU YA DINI NI NGUZO MUHIMU YA MAENDELEO-MAJALIWA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema vijana wenye elimu na maarifa ya dini ni nguzo muhimu ya ustawi na maendeleo katika jamii kwani imani imara ya kidini hujenga jamii zenye maadili mema, ufanisi katika kazi, na upendo wa dhati kwa kila mmoja.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali ina matarajio makubwa kwa vijana wanaoshiriki mashindano Quran kwani kwa kutumia maarifa na ujuzi wanaoupata katika mashindano hayo kutekeleza majukumu muhimu ya kijamii na kiroho.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 8, 2025) alipozungumza na wananchi katika Mashindano ya 16 ya Kuhifadhi Quran Tukufu ngazi ya Afrika Mashariki na Kati yaliyofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi, Dar es Salaam.

“Mashindano haya ni fursa ya kukuza imani na maarifa yenu. Kuhifadhi Quran ni jambo lenye manufaa mengi kwani inaimarisha uhusiano wenu na Mwenyezi Mungu na inajenga msimamo wa kiroho. Nina hakika mnapokuwa na imani imara, nidhamu, na maadili mazuri baadaye mtakuwa viongozi bora wa familia, jamii, na Taifa kwa ujumla.”

Waziri Mkuu ameongeza kuwa mashindano hayo yana mchango mkubwa katika kuimarisha amani, mshik**ano na utulivu wa nchi, pia yanachangia katika kukuza sekta mbalimbali ikiwemo ya uchumi na utalii kwani kila mwaka washiriki kutoka mataifa mbalimbali wanakuja nchini kushiriki au kushuhudia mshindano hayo.

Akizungumzia kuhusu umuhimu wa mashindano ya kuhifadhi Quran, Waziri Mkuu amesema mashindano hayo yana manufaa kwa washiriki na kwa Taifa kwani yanawawezesha washiriki kuwa na uwezo wa kuhifadhi na kuelewa mafundisho ya Quran Tukufu. “Kupitia mashindano haya, tunawahamasisha vijana wetu kuwa na moyo wa kumtumikia Mwenyezi Mungu kwa juhudi kubwa.”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuipongeza taasisi ya Mana'Hil AL - Irfan kwa juhudi zao kubwa katika kuandaa mashindano hayo. “Uwezo wa kuwa na mashindano haya kwa miaka 16 mfululizo ni dalili ya dhamira thabiti ya kuwahamasisha vijana wetu katika kuzingatia na kuhifadhi Quran Tukufu na kuhakikisha kwamba tunalinda utamaduni wa dini, maadili na imani ya Kiislamu.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kwamba Serikali

📍Dodoma▪️TAARIFA KWA UMMAChama cha Mapinduzi (CCM) kufanya vikao vya Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu Machi 10, 20...
08/03/2025

📍Dodoma

▪️TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Mapinduzi (CCM) kufanya vikao vya Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu Machi 10, 2025 Jijini Dodoma.

Vikao hivi vitafanyika chini ya Uwenyekiti wa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

RAIS SAMIA AWASILI ARUSHA KUONGOZA MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Sam...
08/03/2025

RAIS SAMIA AWASILI ARUSHA KUONGOZA MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan leo Jumamosi Machi 08, 2025, amewasili Mkoani Arusha kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA, na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi na serikali. Rais yupo Mkoani Arusha kuongoza maadhimisho ya siku ya wanawake kitaifa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Sakata la Simba kugomea mchezo dhidi ya watani wao, Yanga, limechukua sura mpya baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB...
08/03/2025

Sakata la Simba kugomea mchezo dhidi ya watani wao, Yanga, limechukua sura mpya baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutoa tamko kwamba mechi hiyo ipo palepale k**a ilivyopangwa.

Simba ilitoa tamko usiku wa kuamkia leo ikisema haitaleta timu uwanjani kwenye mchezo huo kufuatia msafara wa kikosi chake kuzuiwa jana usiku kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambao ndio utatumika kwenye mechi hiyo.

Simba ilizuiwa na kundi la watu wanaodhaniwa ni mashabiki wa Yanga maarufu kwa jina la makomandoo, huku pia ikimtaja meneja wa uwanja kudai hakuwa na taarifa kwamba Wekundu hao watakwenda kufanya mazoezi uwanjani hapo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Steven Mnguto amesema licha ya Simba kudai haitaleta timu mchezo huo upo palepale huku akiwataka mashabiki waliokata tiketi kujipanga kwenda uwanjani.

"Matukio yote tumeyasikia na tunayafuatilia kuanzia hatua ambayo yalijiri, kuna ripoti za awali tumeshazipokea kwa wasimamizi mbalimbali na tunazifanyia kazi," amesema Mnguto.

"Kwanza niwatoe wasiwasi mashabiki wa soka na wadau kwa ujumla. Mchezo upo palepale k**a ambavyo kalenda yetu ya soka inavyosema, hakuna mabadiliko yoyote, mashabiki wajipange kuja kutazama mchezo.".

Tukutane Kwa Mkapa  Vs  GAME IS ON, MCHEZO UKO PALE PALE
08/03/2025

Tukutane Kwa Mkapa Vs
GAME IS ON, MCHEZO UKO PALE PALE

Mbunge wa Jimbo la Kisesa, mkoani Simiyu, Luhaga Mpina, ametoa wito kwa Serikali kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa...
08/03/2025

Mbunge wa Jimbo la Kisesa, mkoani Simiyu, Luhaga Mpina, ametoa wito kwa Serikali kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha sheria kali, ikiwemo adhabu ya kunyongwa kwa yeyote atakayebainika kufanya ubadhilifu wa mali za umma.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Nyakafuru, Halmashauri ya Mbogwe, mkoani Geita, Mpina alieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kudhibiti wizi wa fedha za umma, ambao unaathiri ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa.

Kauli yake imekuja baada ya hoja iliyotolewa bungeni na Mbunge wa Mbogwe, Nicodemas Maganga, aliyewataka wabunge wamuunge mkono katika kutunga sheria itakayoweka adhabu kali kwa mafisadi, wezi wa mali za umma, na wala rushwa.

Mpina alisisitiza kuwa ubadhirifu wa rasilimali za taifa unasababisha madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na vifo vya wajawazito na watoto, uhaba wa dawa hospitalini, na mazingira duni ya elimu kutokana na ukosefu wa miundombinu bora.

“Wananchi wanateseka kwa sababu ya watu wachache wanaotafuna kodi za wananchi kwa tamaa. Hali hii haiwezi kuvumiliwa, lazima Bunge lipitishe sheria kali ili kudhibiti wizi huu,” alisema Mpina.

Alihimiza Serikali na wadau wa maendeleo kushirikiana kuhakikisha kuwa mali za umma zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote na si kwa maslahi binafsi ya wachache.

Address

Tabata
Dar Es Salaam

Telephone

+255766660001

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tree Tv Online posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share