15/08/2025
*CHAINIZI INAPUNGUZA NGUVU ZA KIUME...? 😳*
Ama ni uzushi mwingine unaotishia afya yako bila sababu...?
Mtaani kumekuwa na mijadala moto moto ya chini chini.....
“Eti ukila sana Chainizi (au Spinach), Unashuka nguvu za kiume...!” 😲
*Hebu ngoja kwanza..!*
JE... Kuna ukweli katika hili au ni hadithi za mitaani tu zinazoogopesha wanaume kupika mboga.?🤔
Uzuri Mimi ni mtaalamu wa Lishe *"Nutritionist"* sasa wacha niichambue Chainizi kitaalamu...👇
*Oxalic Acid kwenye Chainizi, Inashusha nguvu..?*
↳ Ni kweli, Chainizi ina oxalic acid, Asidi inayoweza kuzuia ufyonzwaji wa madini k**a, Kalsiamu, Zinki na Magnesiamu mwilini...
Haya madini ni muhimu sana kwa afya ya uzazi na homoni za Mwanaume...
Lakini... kiwango hicho cha oxalic kwenye Chainizi ni cha chini, na huwezi kupungukiwa kwa kula Chainizi pekee— Hasa k**a unakula mlo kamili.
*Phytoestrogens,Homoni za k**e kwenye Chainizi..?*
↳ Ndiyo, Chainizi ina phytoestrogens, Lakini kiwango ni kidogo Mno...
Hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba unaweza kupata matokeo ya *"kupoteza nguvu"* kwa kula Chainizi...
Kwa lugha nyingine, huna sababu ya kuogopa mboga hii kwa sababu ya maneno ya mtaani...
*Nitrati za Spinach, Adui au Rafiki wa Mzunguko wa Damu..?*
↳ Hapa ndipo ukweli unapokuja kinyume kabisa na madai...
Chainizi ina nitrates, ambazo huongeza upana wa mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu,
Jambo la msingi kabisa katika kudumisha nguvu za kiume, Kwa kifupi, inaweza hata kuwa msaada badala ya tatizo ...!
*NB:* Chainizi ni chanzo bora cha virutubisho k**a Iron, Folate, Vitamin C na K, vyote hivi ni msaada mkubwa kwa afya ya mwanaume — *Si adui..!*
Jiponye afya herbs