Idreams radio

Idreams radio Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Idreams radio, Radio Station, Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Mwanamke mmoja ajulikanaye kwa jina la Hellen Mchahuru (40) kwa tuhuma za ku...
03/06/2022

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Mwanamke mmoja ajulikanaye kwa jina la Hellen Mchahuru (40) kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumkata na wembe sehemu za siri (Korodani ya kushoto) mumewe Vintan Luhiva (42).

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Joseph Konyo  amesema mtuhumiwa aliweza kufanya tukio hilo wakati mwanaume huyo akiwa amesinzia.

ameeleza kuwa mtuhumiwa alichukua wembe na kumjeruhi kwa kumkata korodani moja upande wa kushoto na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda Konyo amesema majeruhi amelazwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Tunduru akipatiwa matibabu na kwamba mtuhumiwa anayedaiwa kutenda tukio hilo yupo mikononi mwa Polisi na hatua za kumpeleka Mahakamani zinafuata baada ya hatua za upelelezi.

Wakati Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu wa 2021/22 ikielekea ukingoni, Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala ...
03/06/2022

Wakati Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu wa 2021/22 ikielekea ukingoni, Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele anahusishwa na mpango wa kuachana na klabu hiyo, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kisoka na kuzifumania nyavu za timu pinzani.

Mayele ambaye amefunga zaidi ya mabao 10 katika ligi hiyo, anahusishwa na mpango wa kuwaniwa na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika RS Berkane, chini ya Kocha Mkuu Florent Ibenge.

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari kutoka Congo DR vimethibitisha kuwa, Kocha Ibenge ambaye aliwahi kufanya kazi na Mayele katika klabu ya AS Vita, amevutiwa na uwezo wa Mshambuliaji huyo baada ya kumfuatilia kwa ukaribu akiwa Young Africans msimu huu 2021/22.

Cc: Dar 24

SAKATA la mtoto mwenye umri wa miaka 8 anayedaiwa kunyongwa na msichana wa kazi eneo la Kimara Temboni mtaa wa Sokoine j...
02/06/2022

SAKATA la mtoto mwenye umri wa miaka 8 anayedaiwa kunyongwa na msichana wa kazi eneo la Kimara Temboni mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam limechukua sura mpya baada ya mzazi kuthibitisha kuwa CCTV Camera zilikuwa zimezimwa.

Baada ya Media yetu kwenda nyumbani kwa Marehemu imefanya mahojiano na wazazi wote wa marehemu ambao wote kwa pamoja wamethibitisha kuwa na sintofahamu kutokana na utata wa mazingira ya kifo cha mtoto wao anayefahamika kwa jina la Erickson.

Erick Kimaro Baba wa marehemu akihojiwa na mwandishi wetu

Mama wa marehemu anadai alikuta alama za michubuko katika shingo ya marehemu pamoja na uvimbe juu kidogo ya jicho lakini Baba wa marehemu anayefahamika kwa jina la Erick kimaro Mumba naye alipofanya mahojiano alisema wasiwasi ulikuwa pale walipouona mwili wa marehemu ukiwa na michubuko maeneo ya shingoni mwake ndipo wakahisi pengine anaweza kuwa amenyongwa.

Madai ya kwamba CCTV Camera ilinasa tukio zima ni madai yaliyokanushwa na Baba wa Marehemu akidai kuwa CCTV Camera ilikuwa imezimwa muda wote tangu siku moja kabla ya tukio hilo.

Rais Samia amesema wananchi wanahitaji mitaji midogo midogo hasa katika uzalishaji wa bidhaa zao ambazo hazina viwango k...
02/06/2022

Rais Samia amesema wananchi wanahitaji mitaji midogo midogo hasa katika uzalishaji wa bidhaa zao ambazo hazina viwango kutokana na kukosa vifungashio vinavyovutia sokoni hivyo TASAF isaidie kuwainua na kuwabadilishia mtazamo.

Pia Rais amewaonywa baadhi ya wafanyakazi walafi kuepuka ulaji wa pesa za mradi huo kwa manufaa yao binafsi kwani fedha hizo zinatokana na mikopo ambayo hulipwa na watanzania wote hivyo wazifanyie kazi iliyokusudiwa.

Awali kabla ya kumkaribisha Rais Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama amesema Rais Samia anaendelea kuweka historia kwa kujenga uchumi na amewathibitishia Watanzania jinsi anavyowajali kwa kuwapatia magari yatakayosaidia utekelezaji wa majukumu na kuwahudumia.

Amesema mradi wa huo wa TASAF awamu ya tatu sehemu ya pili utasaidia kuwafikia wahitaji katika vijiji, shehia na kaya zenye wakazi zaidi ya milioni sita na kufanya mpango huu wa maendeleo wa taifa kutekelezwa kwa ufanisi

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dorothy Gwajima amewataka wanawake kuwa vinara kupamban...
02/06/2022

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dorothy Gwajima amewataka wanawake kuwa vinara kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini

Dkt. Gwajima amesema elimu zaidi kwa kutumia wataalam wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii itumike kubadilishabfikra za jamii ili iweze kushiriki kataka kupambana na vitendo vya ukatili hasa kwa jamii kujikita kunako mapambano hayo hasa kuchangia rasilimali fedha na nguvu kazi ili kuondokana na vitendo hivyo. 

Ameongeza kuwa Wanawake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwalinda Watoto na vitendo vya ukatili hasa unaotokea nyumbani na shuleni kwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika Malezi na makuzi kwa mtoto 

“Wanawake tuwe mstari wa mbele katika kupambana na vitendo vya ukatili ila hasa katika kujikwamua kiuchumi kwa kujishughulisha katika shughuli za maendeleo ili kupunguza vitendo hivyo ambavyo sababu kubwa ni uchumi,” alisema Waziri Dkt. Gwajima.

Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake leo Juni Mosi, 2022 wamefikishwa katika M...
02/06/2022

Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake leo Juni Mosi, 2022 wamefikishwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Moshi Kilimanjaro kwa tuhuma za makosa ya uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa Mwendesha mashataka wa Serikali Tumaini Kweka amesema Lengai Ole Sabaya, Nathan Msuya, Sylvester Nyegu, Antheo Boniface Assey na John Aweyo wanashtakiwa kwa makosa saba ya uhujumu uchumi.

Makosa mengine ni pamoja na kuongoza genge la uhalifu, kutenda kinyume na mamlaka yake, kujihusisha na vitendo vya rushwa na utakatishaji fedha.

Awali Wakili upande wa utetezi Hellen Mahuna ameiomba Mahakama hiyo kutenda haki kwa madai kuwa wateja wake na Mahakama ya Arusha haikupata kibali halali cha kuwatoa washtakiwa gereza la Kisongo  Arusha na kuwapeleka gereza la Karanga Moshi.

Hata hivyo Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakamu ya hakimu mkazi Moshi Kilimanjaro Salome Mshasha ameahirisha kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2022 hadi Juni 7, 2022 itakapotajwa tena.

H-Baba amlilia Swalha, mrembo aliyeuawa kwa risasi na mumewe, aweka video mtandaoni ikionesha wakiwa pamoja.Tumekuja
02/06/2022

H-Baba amlilia Swalha, mrembo aliyeuawa kwa risasi na mumewe, aweka video mtandaoni ikionesha wakiwa pamoja.

Tumekuja

Usikose kipindi chako cha   siku ya JumamosiKupitia idreams radio online na youtube idreams media kuanzia saa 10:00 hadi...
01/06/2022

Usikose kipindi chako cha siku ya Jumamosi
Kupitia idreams radio online na youtube idreams media kuanzia saa 10:00 hadi 10:30 jioni

01/06/2022

live performance

Rais Samia Suluhu Hassan ametaja sababu za kukubali kushiriki kwenye tamasha la msanii wa muziki wa HipHop, Joseph Mbili...
01/06/2022

Rais Samia Suluhu Hassan ametaja sababu za kukubali kushiriki kwenye tamasha la msanii wa muziki wa HipHop, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ‘The Dream Concert’ huku akizindua kitabu cha muziki na maisha cha mwanamuziki huyo.

Tamasha hilo limefanyika usiku wa kuamkia leo Jumatano Juni Mosi kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam likiwa ni maalumu kwa mbunge huyo wa zamani wa Mbeya Mjini kuadhimisha miaka 30 kwenye sekta ya muziki.

Akieleza sababu ya kukubali kushiriki tamasha hilo, mkuu huyo wa nchi ameweka wazi sababu mbili akisema "Kwanza kwa Joseph mimi ni mama hivyo niliona fahari kushuhudia mafanikio ya mwana”

Rais Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na msanii wa muziki wa Hiphop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ mara baada ya kuwasili Serena kwa ajili ya kuhudhuria tamasha la maadhimisho ya miaka 30 ya msanii huyo.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Idreams radio posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Idreams radio:

Shortcuts

Share

Category