22/09/2025
BM YAPATA AJALI
•
✍🏿na Dr. Mtawala.
•
Basi la kampuni ya BM, aina ya YUTONG lenye namba za usajili T 816 EED linalofanya safari zake kati ya Arusha na Dar es Salaam, limepata ajali katika eneo la Msasani Maili Sita, Wilaya ya Moshi, alfajiri ya Septemba 22.
•
Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo ilihusisha basi hilo na lori aina ya FAW, mali ya kampuni ya Falcon Animal Feed Ltd ya Dar es Salaam. Inadaiwa lori hilo liliteleza na kuacha njia, hali iliyomlazimu dereva wa basi kukwepa kwa kuligonga tairi la lori na hatimaye kupoteza muelekeo.
•
Mashuhuda walieleza kuwa basi hilo lilitoka barabarani na kutembea umbali wa takribani mita 200, likigonga miundombinu ya umeme kabla ya kutumbukia kwenye korongo kubwa la maji.
•
“Dereva alijitahidi sana kukwepa madhara makubwa zaidi, ikiwemo nyumba inayotumika k**a makazi ya kurekebisha waraibu wa dawa za kulevya ya KRC, pamoja na nguzo za umeme wa msongo mkubwa,” mmoja wa mashuhuda.
•
Licha ya uharibifu mkubwa wa miundombinu ya umeme na magari husika, taarifa zinaeleza kuwa abiria wote walinusurika bila majeraha.
•
K**anda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi (SACP) Simon Maigwa, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
•
“Ni kweli ajali imetokea, lakini hakuna vifo wala majeruhi. Maelezo zaidi yatatolewa na kikosi cha usalama barabarani,” SACP.
•tanzania
•
Endelea kusikiliza Mtawala Radio, tunasikika duniani kote.
•
Follow us on Instagram
+255 758 555 000.
•
✍🏿na wa Mtawala Radio.
•
Mtawala Radio "Duniani K**a Mbinguni"
•