fadmediatz

fadmediatz Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from fadmediatz, News & Media Website, Dar es Salaam.

18/12/2025

Wameenda jamani 😂

Powered by

18/12/2025

Hali ilivyo muda huu Tanganyika packer Kawe Dar es salaam kuelekea Mkesha wa Mtumishi wa Mungu Buldoza Boniface mwamposa, Maelfu ya watu wapo tayari hapa na wameshachukua nafasi za mbele zote🇹🇿

Powered by


18/12/2025

Msanii na Mfanyabiashara amezungumza na Waandishi wa Habari kwa mara ya kwanza tangu itokee changamoto ya kuungua kwa mgahawa wake wa October 29.

Shilole ameeleza kuhusu mapokeo yake katika hilo, hatua aliyochukua ikiwa ni kurejesha huduma ya chakula kwa kufanya Delivery kutokea nyumbani k**a ambavyo alikuwa anafanya awali.

Powered by

17/12/2025

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo tarehe 17 Desemba, 2025 amezungumza na wakazi wa eneo la Tunduma mkoani Songwe, akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua uharibifu wa miundombinu ya umma na mali binafsi uliosababishwa na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025.

Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Nchemba amewaagiza Watendaji Wakuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kufanya tathmini ya kina ya miradi yote ya ujenzi ambayo tayari malipo ya awali yameshafanyika pamoja na hatua za utekelezaji zilizofikiwa.

Amesisitiza kuwa tathmini hiyo ihakikishe utekelezaji wa miradi unaendana na kiwango cha fedha kilichotolewa, ili kubaini ufanisi, changamoto zilizopo na hatua stahiki za kuchukua ili kulinda rasilimali za umma.

Ziara hiyo inalenga kuhakikisha miundombinu iliyoharibiwa inarejeshwa kwa haraka pamoja na kuchukua hatua za kudhibiti hasara zilizojitokeza, huku Serikali ikiendelea kusimamia matumizi sahihi ya fedha za umma na kulinda maslahi ya wananchi.

Powered by


17/12/2025

‎Ujenzi wa Bwawa Kubwa la Kuhifadhi Maji la Kidunda, linalojengwa mkoani Morogoro, umefikia asilimia 40. Bwawa hilo linatarajiwa kuhifadhi zaidi ya lita bilioni 190 za maji na kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 335.
‎
‎Mradi huo mkubwa unalenga kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, pamoja na kusaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi mara baada ya kukamilika kwake mwaka 2026.
‎
‎Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa bwawa hilo la Kidunda mkoani Morogoro, Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso, ambaye aliambatana na wakuu wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro, amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili kutatua changamoto ya maji kwa wakazi wa mikoa hiyo.
‎
‎Kuhusu ulinzi wa vyanzo vya maji na kuhakikisha bwawa hilo linajaa maji mara baada ya kukamilika, Mheshimiwa Aweso amesema ni wajibu wa wananchi na mamlaka husika kulinda mazingira na vyanzo vya maji ili mradi huo uwe endelevu.
‎
‎Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Adam Malima, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassi, wameeleza umuhimu wa bwawa hilo kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, huku wakisisitiza suala la ulinzi na usimamizi wake.
‎
Powered by

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when fadmediatz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share