15/10/2025
                                            Vijana wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Karagwe, wakiongozwa na Mwenyekiti wao Alexius Sylivester, wamefanya hamasa kubwa ya kumkaribisha Mgombea Urais wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye anatarajiwa kuzungumza na wananchi na wanachama wa CCM katika mkutano wa kampeni utakaofanyika leo, tarehe 15 Oktoba 2025, katika Uwanja wa Bashungwa โ Kayanga.
Akizungumza wakati wa maandalizi hayo, Alexius alimpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake thabiti na kwa kuendelea kulinda amani, umoja na ustawi wa Watanzania, mambo yanayowezesha wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa uhuru na kuleta maendeleo endelevu.
Hamasa hiyo iliyoenea katika mitaa yote ya mji wa Kayanga ilijaza nguvu ya mapenzi, furaha na uzalendo kwa wananchi, huku vijana wakionyesha ari na shauku ya kumpokea Mama wa maendeleo, Dkt. Samia Suluhu Hassan.