26/12/2024
*GLOB8FY HISTORY*
*IJUE HISTORIA YA PICHA HII*
Inawezekana umeiona hii picha mara nyingi, ila leo utaifahamu stori ya kusikitisha iliyojificha nyuma ya hii picha, stori inaanzia karne ya 15 katika kijiji kidogo kilichopo pembeni ya jiji la Nuremberg, huko ujerumani.
Kulikua na familia yenye watoto kadhaa, ilikua ni familia maskini ili kupata mkate wao wa kila siku ilibidi Baba yao afanye kazi kwa zaidi ya masaa 18 kwenye machimbo ya makaa ya mawe na walikula chochote walichopata, ila kulikua na watoto wawili katika familia hiyo ambao walikua na ndoto ya kuwa wachoraji wakubwa.
Walifahamu Baba yao hana uwezo wa kuwapeleka chuo wakasomee fani hiyo ya uchoraji, ikawa kila siku usiku wanajadiliana vipi watafikia ndoto zao, siku moja baada ya majadiliano mengi ya usiku wa siku nyingi kupita hawa watoto wawili walikubaliana kuwa watarusha shilingi juu ili wapate mshindi na atakaeshindwa itabidi aende akafanye kazi kwenye machimbo ya makaa ya mawe kwaajili ya kutafuta pesa na kumlipia ada ya chuo atakaeshinda, na baada ya mshindi kumaliza masomo nae atamsomesha mwenzake aliebaki kwa kuuza kazi ya sanaa ya uchoraji atakayokua anaiuza.
Kulivyokucha walirusha shilingi juu mmoja anaeitwa Albrecht Dürer alishinda na akaenda kusoma jijini Nuremberg, Germany. Kaka yake akabaki kufanya kazi ya hatari kwenye machimbo ya makaa ya mawe kwa miaka 4 ili kulipa ada ya Albrecht, na bahati nzuri Albrecht alikua na uwezo mkubwa sana chuo na hadi anamaliza masomo yake alianza kupata pesa kutokana na kazi zake za sanaa.
Baada ya kumaliza masomo Albrecht Dürer alirudi kijijini kwao na akakuta familia imemuandalia sherehe ya heshima kwa mafanikio hayo, wakiwa wanasherehekea Albrecht alisimama mbele ya meza iliyoandaliwa kwa heshima yake na akamshukuru kaka yake kwa kujitoa ili amsomeshe na akasema pia yupo tayari kumlipia ada kaka yake ili nae akasome k**a ilivyokua makubaliano yao, lakini habari ya kusikitisha ni kuwa kaka yake alikataa
Albrecht Dürer akamuuliza kaka yake kwanini unakataa? Kaka yake akajibu " Hapana mdogo wangu mimi sitaenda Nuremberg kusomea sanaa ya uchoraji, nimeshachelewa sana, hii miaka minne niliyofanya kazi kwenye machimbo imeharibu mikono yangu, kila mfupa ulio kwenye vidole vyangu hakuna ambao haujawahi kuvunjika, vidole vya mkono wangu wa kulia kila siku vinazidi kukak**aa, hata kwenye sherehe yako nimepata shida kushika glass kugonga cheers na wewe".
"Siwezi kushika kalamu wala brash, ila nina furaha mikono yangu hii iliyojaa kasoro imeweza kusaidia wewe kufikia ndoto yako".
Albrecht Dürer alilia sana kwaajili ya kaka yake, kaka aliejitoa kuvunjika vidole ili amsomeshe yeye na mwisho hakuhitaji malipo yoyote.
Ni zaid ya miaka 450 sasa imepita tangu siku ya tukio hilo, Albrecht Dürer alichora picha nyingi zilizojaa kwenye makumbusho ila siku moja aliamua achore picha ya mikono ya kaka yake ikiwa imekutana pamoja na inaelekea mbinguni k**a ishara ya kushukuru, na picha yenyewe ndo hii ambayo imekua maarufu hata kwa wasiojua historia yake.
*GLOBIFY*