wazohurutv

wazohurutv Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from wazohurutv, TV Channel, Dar es Salaam.

MJADALA WA BANDARI USILIGAWE TAIFAWAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mjadala unaoendelea kuhusu uwekezaji kwenye bandar...
29/06/2023

MJADALA WA BANDARI USILIGAWE TAIFA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mjadala unaoendelea kuhusu uwekezaji kwenye bandari ya Dar es Salaam usiligawe Taifa kwa sababu Serikali ya awamu ya sita ni sikivu.

“Mjadala unaoendelea kuhusu bandari ya Dar es Salaam usitugawe Watanzania. Usipelekee tukasambaratika. Tusitumie nafasi hiyo kutugawa kiitikadi, kidini au kisiasa. Sisi ni wamoja na jambo letu ni moja. Serikali yenu sikivu itaratibu haya,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Juni 29, 2023) wakati akizungumza na mamia ya waumini waliohudhuria swala ya kitaifa ya Eid el Adh’haa iliyofanyika kwenye msikiti wa Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco, Kinondoni, jijini Dar es Salaam ambako alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema Serikali inapokea maoni na ushauri kutoka kwa wadau na kwamba ina nia njema kuhusu suala hilo na ndiyo maana ililiweka hadharani. “Natambua kuna watu wana hofu na umiliki wa bandari, ajira, ardhi na usalama wa Taifa lakini tusisahau kuwa TICTS wamekuwepo pale kwa miaka zaidi ya 22. Niwatoe hofu Watanzania kuwa malengo yetu ni kuboresha uchumi wa Tanzania. Tunataka watumiaji waliohama warejee,” amesema.

Amesema Tanzania imezungukwa na nchi nane ambazo hazina bandari na zinategemea bandari ya Dar es Salaam kupitishia mizigo yao. “Kwa hiyo bandari ya Dar es Salaam  ni kitovu cha uchumi. Mwekezaji huyu ana uzoefu mkubwa na teknolojia ya hali ya juu katika uendeshaji shughuli za bandari kwenye nchi 68. Sisi pia tunatamani kufanya vizuri k**a yeye alivyofanya katika nchi nyingine,” amesisitiza.

Amesema yeye binafsi kwa kushirikiana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wataongoza suala hilo la utoaji elimu na anaamini kwamba Watanzania wataelewa malengo hayo na hasa hatua ambazo Serikali inatamani kuzifikia.

Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi huo kufuatia ombi la Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Alhaj Nuhu Jabir Mruma la kuitaka Serikali iendelee kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu suala la uwekezaji kwenye bandari hiyo.

SERIKALI KUTOA MAFUNZO KWA WATAALAM ZAIDI YA 500 WA TEHAMA-MHANDISI KUNDONa Mathias Canal, ArushaKatika mwaka wa fedha 2...
20/06/2023

SERIKALI KUTOA MAFUNZO KWA WATAALAM ZAIDI YA 500 WA TEHAMA-MHANDISI KUNDO

Na Mathias Canal, Arusha

Katika mwaka wa fedha 2023/2024, serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Hbari inatarajia kutoa mafunzo kwa wataalam zaidi ya 500 wa TEHAMA katika nyanja mbalimbali za TEHAMA.

Utekelezaji wa majukumu hayo unaiwezesha Tanzania kushiriki katika uchumi wa kidijitali wakati wa Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (4IR) yanayowezeshwa na kuendeshwa na TEHAMA na kuwa na jamii inayopata taarifa sahihi kwa wakati.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Mhandisi Kundo Mathew Ameyasema hayo leo tarehe 20 Juni 2023 wakati Akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Taasisi ya Usalama wa Mitandao nchini (ISACA) uliofanyika katika Hoteli ya Grand Melia Mkoani Arusha.

Naibu Waziri Mhe Mhandisi Kundo amesema kuwa Wizara imetenga fedha kwa ajili ya kusaidia mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika teknolojia mbalimbali za teknolojia inayochipukia ili kujiandaa na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda.

Amesema kuwa Sekta ya Habari na Mawasiliano ilikua kwa asilimia 0.7 hadi asilimia 9.1 mwaka 2021. Ukuaji huo unathibitishwa na kuongezeka kwa upatikanaji na matumizi ya huduma za mawasiliano na kuenea kwa huduma zinazotolewa na vyombo vya habari.

Amesema kuwa Watumiaji wa intaneti wameongezeka hadi kufikia milioni 33.1 mwezi wa Aprili 2023. “Tunaona ongezeko la idadi ya watoa huduma za miundombinu, maombi na watoa huduma walioongezwa thamani. Tanzania haijaachwa nyuma katika mapinduzi ya kidijitali. Pamoja na kuimarisha na kupanua miundombinu” Amekaririwa Mhandisi Kundo

Kadhalika amesema kuwa Serikali kupitia Tume ya TEHAMA itaendelea kuratibu mafunzo ya wataalam wa TEHAMA katika maeneo husika ili kuhakikisha nchi inasonga mbele na kutokubaki nyuma katika Mapinduzi ya Nne ya Viwanda na kupitishwa kwa teknolojia kwa uchumi wa Tanzania.

“Tumetoa mafunzo kwa wataalam 352 katika maeneo ya Uchanganuzi wa Data Kubwa na Usalama wa Mtandao na tunapanga zaidi kutoa mafunzo kuhusu Ujasusi Bandia, Uchanganuzi mkubwa wa Data, Cybersecurity, Cryptography, Cloud Computing, Blockchain, Computer Forensics, Development Development, Mobile Application Development,

WAHAMIAJI HARAMU WANNE WANASWA IRINGASAFARI ya raia wanne wa Ethiopia waliopenya nchini kwa lengo la kuelekea Afrika Kus...
24/05/2023

WAHAMIAJI HARAMU WANNE WANASWA IRINGA

SAFARI ya raia wanne wa Ethiopia waliopenya nchini kwa lengo la kuelekea Afrika Kusini bila kuwa na vibali imeishia mkoani Iringa baada ya jeshi la Polisi kuwanasa katika kizuizi cha Polisi Changarawe wilayani Mufindi.

Akizungumza na wanahabari leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi alisema waethiopia hao walik**atwa Mei 22, mwaka huu wakiwa kwenye gari mbili tofauti (IT) zilizokuwa zinapelekwa Zambia.

"Waethiopia hao walikuwa wakielekea Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma kwa kutumia gari hizo ambazo ni IT 3802 aina ya Vits na IT 7485 aina ya mazda," alisema.

Alisema wakati Vits ilikuwa ikiendeshwa na Musa Omari (32) mkazi wa Tabata Dar es Salaam, Mazda ilikuwa ikiendeshwa na Musa Mashala mkazi wa Airport Dar es Salaam.

Wakati majina ya waethiopia wawili hayajajulikana kwasababu ya changamoto ya lugha, Kamanda Bukumbi aliwataja wawili wengine kuwa ni Tesfahun Petros (22) na Degefe Sugumo (20).

"Watuhumiwa hao kwa pamoja wanashikiliwa wakisubiri kufikishwa mahak**ani pamoja na magari hayo yatapelekwa k**a vielelezo," alisema.

Wakati huo huo Kamanda Bukumbi alisema katika oparesheni ya jeshi hilo iliyofanywa kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha kati ya Mei 17 na 23 mwaka huu wamefanikiwa kuwak**ata watuhumiwa wa ujangili wawili Nazareth Miliuka (64) na Jafari Miluka (24).

Alisema watuhumiwa hao wote wakazi wa kijiji cha Wangamaganga wilayani Mufindi walik**atwa wakiwa na silaha tatu aina ya gobole, unga wa baruti, goroli nne, mafundo mawili ya pamba, vyuma vidogo nane na mtego wa wanyama.

Vile vile katika msako uliofanyika katika kijiji cha Mapogoro kata ya Idodi wilayani Iringa walifanikiwa kumk**ata Tony Vitus (48) mkazi wa Mbinga Ruvuma akiwa na meno makubwa manne na vipande saba vya Tembo.

Alisema uchunguzi wa matukio hayo unaendelea na watuhumiwa hao watafikishwa mahak**ani wakati wowote kuanzia sasa pindi uchunguzi utakapokamilika.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi  akutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti w...
22/05/2023

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mwalimu Nyerere Foundation Bw. Joseph Butiku alipomtembelea ofisini kwake Mei 22, 2023 Jijini Dodoma.

TAWI LA CHUO KIKUU CHA MISRI KUANZISHWA TANZANIA- WAZIRI MKENDAChuo Kikuu cha Misri kimebainisha kusudio la kuanzisha ta...
18/08/2022

TAWI LA CHUO KIKUU CHA MISRI KUANZISHWA TANZANIA- WAZIRI MKENDA

Chuo Kikuu cha Misri kimebainisha kusudio la kuanzisha tawi lake nchini Tanzania kwa ajili ya kuanza kutoa elimu katika fani mbalimbali.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameeleza hayo Leo tarehe 16 Agosti 2022 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe Mohamed Gaber Abulwafa katika ukumbi wa mikutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jijini Dodoma.

Waziri Mkenda amemueleza Balozi huyo kuwa serikali ya Tanzania imetoa fursa ya wawekezaji kuja nchini kufuata taratibu za kisheria na kuwekeza haraka iwezekanavyo.

Amemualeza Balozi huyo kuwa wakati taratibu zingine zinaendelea za uwekezaji huo, Chuo kikuu hicho kinaweza kuunda ushirika na Chuo Kikuu chochote kilichopo nchini ili kuanza kutoa elimu kusudiwa kwa haraka.

Waziri Mkenda amemuelekeza Mkurugenzi anayeshughulikia Vyuo Vikuu katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Kenedy Hosea kuhakikisha anaanza mazungumzo na vyuo vikuu nchini ili kuona ni chuo gani kipo tayari kuanza ushirikiano huo ili utekelezaji uanze.

Kwa upande wake Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe Mohamed Gaber Abulwafa amemuhakikishia Waziri Mkenda kuwa nchi yake itaendeleza ushirikiano na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu.

Katika mazungumzo hayo wamejadiliana pia namna ya kuanza utekelezaji wa haraka wa (MOU) zilizosainiwa wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini Misri.

Pia Balozi Abulwafa amewasilisha mualiko wa Waziri wa Nishati wa Misri kumualika katika mkutano utakaokuwa unajadili masuala ya Atomiki pamoja na mwaliko wa Waziri wa elimu wa Misri ili kujadili kwa kina umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika sekta ya elimu.

MWISHO

Mfalme Zumaridi na wafuasi wamefikishwa katika mahak**a ya hakimu mkazi Mwanza
03/03/2022

Mfalme Zumaridi na wafuasi wamefikishwa katika mahak**a ya hakimu mkazi Mwanza

Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa  afurahishwa na ratiba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara  ya kutembelea Miradi katika m...
12/01/2022

Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa afurahishwa na ratiba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ya kutembelea Miradi katika mkoa wake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, na mgeni wake Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakiwa...
10/12/2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, na mgeni wake Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakiwa katika picha yenye waasisi wa Mataifa mawili Tanzania na Kenya Hayati Mwalim Julius Nyerere wa Tanzania na Hayati Jomo Kenyatta wa Kenya wakati Rais Kenyatta alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 2021. Mhe. Rais Kenyatta yupo nchini kwa Ziara ya Kiserikali ya siku moja.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuqpisha Mhe. Innocent Bashungwa kuwa Waziri wa Uta...
24/10/2021

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuqpisha Mhe. Innocent Bashungwa kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo katika ghafla iliyofanyika ikulu ya jijinj Dar es Salaam leo tarehe 24.10.2021.

15/10/2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Sanya Juu Wilay...
15/10/2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Sanya Juu Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 32.2 katika eneo la Sanya Juu Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro leo Octoba 15,2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye ur...
15/10/2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 32.2 katika eneo la Sanya Juu Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro leo Octoba 15,2021. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when wazohurutv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category