23/07/2025
Trust me wanaume wengi wako ndani ya nyumba zao, lakini hawapo nyumbani, k**a unaelewa maana ya nyumbani' ni mahali ambapo unahisi uhuru kimwili, kiakili, na kihisia.
Lakini wanaume wengi wanarudi baada ya kazi, wanaketi kwenye kochi, wanashika simu zao, wanakula chakula cha jioni, halafu wanaenda kulala. Inshort wapo kimwili, lakini kiakili na kihisia wameshatoka zamani, wakifika kwenye nyumba zao wananyamaza, wanapooza, hawajihusishi tena na chochote wanasubiri pakuche waondoke.
Mwanamke nae akiona hali hiyo anaanza kujisikia k**a mwanamke asiye na mume japo yupo ndani ya ndoa, anajiona ana mtu ndani ya nyumba lakini hana wa kuzungumza naye, ana mtu wa kushiriki nae kitanda kimoja lakini si yaliyomo moyoni mwake, anajisikia kutoonekana, kutosikilizwa na polepole anaanza kufa ndani kwa ndani kihisia, hatimaye anabadirika mazima.
Leo nataka niongee na wewe mwanamke...
Tambua, ndoa iko mikononi mwako, mwanamke ndiye moyo wa nyumba, damu ya familia, na dira ya kizazi kijacho, mwanamke mjinga huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe, kwa maneno yake(kamdomo), kwa kiburi chake, kwa kutokujali, na kwa kutokutambua nafasi yake k**a mjenzi wa familia.
Lakini mwanamke mwenye hekima, hata wakati wa dhoruba, hujifunza kunyamaza ili asikilize kwa makini, huomba hekima, huwa na heshima, na huongea kwa upole tena hoja za msingi. Mwanamke anayejitambua anajua kwamba upendo haujengwi kwa maneno matamu tu, bali kwa tabia njema, uvumilivu, na heshima.
Tambua, hakuna nyumbani bila uwepo wa mwanamke, mwanamke ndiye anayefanya nyumba iwe na ladha, iwe na amani, iwe na uzuri wa kipekee, mwanamke anaweza kugeuza nyumba ya kawaida kuwa paradiso ya familia, au akaifanya iwe jela isiyovumilika.
Nyumba yoyote imara, ndoa yoyote imara, hujengwa na mwanamke, Yes! Kwa busara yake hutuliza migogoro. Kwa tabasamu lake huleta faraja, kwa usafi wake hujenga heshima, kwa kufanya maombi huombea mume na watoto wake bila kuchoka.
Mwanamke, tambua nguvu ulizonazo.
Usione k**a wewe ni wa pili au mfuasi tu, Wewe ni kiini, ni msingi, ni kiunganishi cha familia. Usipambane kuwa mwanaume au kujilinganisha na mwanaume, usijifanye kuwa juu ya mumeo, pambana kuwa mwanamke wa kipekee anayemsaidia mwanaume wake kuwa bora. Sio kwa kushindana naye, bali kwa kumtia moyo na kumwelekeza kwa upendo.
Mwanamke mjanja haongei kila kitu.
Anajua muda wa kusema na muda wa kunyamaza. Anajua nguvu ya kimya chenye hekima, anajua si kila tatizo linatatuliwa kwa lawama, bali mengine kwa maombi, subira, na maongezi laini ya upendo.
Leo baada ya kusoma ujumbe huu wa Halisi Naturalist fanya uamuzi mpya.
Usiwe chanzo cha migogoro, kelele, na vurugu nyumbani, badala yake, kuwa chanzo cha upendo, maombi, na utulivu.
Watoto wako wanakuangalia, mume wako anategemea faraja yako, japo kuwa unamuona amebadirika tambua wewe unaweza kuwa sababu ya yote hayo, jikague kisha rekebisha unapokosea, na hata k**a unajiona hauna hatia bado unayo nafasi ya kumrekebisha ili ndoa yenu isimame tena, kumbuka mwanaume ni k**a mtoto na wewe ni k**a mama, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, anaweza kuchelewa kuiona thamani yako lakini ipo siku isiyo na jina utaibuka mshindi, Mungu yuko katikati ya kila jambo la kheri na kwa shetani sio pa kudumu ni pa muda tu.
Ndoa ni uwanja wa mapambano ya kiroho, kihisia, na kiakili, mwanamke mjanja hajitoi mapema. Hujifunza, hurekebisha, na kusimama imara.
Hata wewe unaweza.
✍️✍️✍️✍️