
21/08/2025
Nina jamaa yangu ambaye tumeshibana sana, langu lake na lake ni langu, nilimwamini sana kiasi kwamba hata nikisafiri namwagiza aende nyumbani kwangu akaniangalizie mazingira, na likitokea tatizo mimi sipo namwagiza yeye analimaliza, hata mimi hivyo hivyo kwake.
Viashiria vilianza kwa mke wangu kumsifia sana jamaa, mara ooh ni mpole, anajitambua, na sifa kibao, mwanzo niliona kawaida ila kwa baadae nikaanza kuona k**a inazidi.
Baada ya muda mrefu kupita makucha yao yakaanza kujitokeza, jamaa yangu alikuwa anapenda kuja kwangu hata k**a hakuna inshu ya muhimu tuliyoongea, na akija tu mood ya mke wangu inabadirika, anaanza kuchangamka na kuongea vizuri, kucheka cheka sana, inshort anafurahia uwepo wa rafiki yangu.
Katika uchunguzi wangu wa kina nikagundua rafiki yangu anatembea na mke wangu, na pia nilishasikia tetesi kutoka kwa majirani.
Ikabidi nitenge muda nimuulize mmoja mmoja kwakweli wote walikataa, ikabidi niweke mtego, nikajifanya nimepata safari ya kikazi, nikamuomba rafiki yangu asikanyage kwangu kwani nina mashaka nae, niliongea kwa sauti ya utani "Wewe jamaa sitaki ukanyage kwangu huu muda ambao sipo nyumbani maana nina mashaka na wewe, nikirudi tutaongelea hili zaidi" akajifanya amenielewa, ushauri mwingi eti nijiamini niache dhana, n.k
Nikachukua Bag langu nikaondoka, nikaenda lodge fulani ambayo haiko mbali sana na nyumbani kwangu nikatulia hapo, mpaka saa 6 usiku ndio nikachukua uber nikarudi nyumbani, kumbuka nilimuaga wife nitakaa wiki moja.
Nilishuka kwenye gari nikanyata mpaka dirishani, dirisha la chumbani, maana nyumba yangu imekaa k**a L na dirisha limetazamana na barabara ya mtaa, nikasimama hapo muda mrefu, rafiki yangu hakuwa ndani ila mke wangu nilisikia alikuwa anaongea na simu kwa mahaba na mwanaume niliyehisi ni yule rafiki yangu japo sikuwa na uhakika, nikasikiliza machache k**a dakika 10, nikaondoka kurudi lodge.
Nikiwa njiani narudi kuna jirani yangu alinitumia sms "Babu jinga mali yako yaliwa" ikabidi nimpigie, hakufunguka sana akasema we tumia akili, nikamwambia nipe code japo kidogo akasema we tuma mtu unaye muamini aje kwako hapa mengine hayanihusu.
Ikabidi nirudi, safari hii niliingia moja kwa moja na nilipogonga mlango kwa nguvu, mke wangu alikuja na jazba, we nani unagonga mlango hivyo usiku watu wamepumzika? Nikabadili sauti na kujifanya wa k**e, nikasema "Ni mimi", nilijua hatanitambua ila atleast asijue k**a ni mimi mume wake.
Akafungua mlango nikazama ndani na mlango kwa kusukuma kwa nguvu na yeye akaangukia ndani, sikuamini nilichokiona, kumbe muda ule natoka baada ya kusikilizia dirishani jamaa alikuwa njiani anaelekea kwangu, na muda naingia ndani alikuwa sebuleni amevaa taulo yuko anakula, halafu alivyokuwa fala eti anavaa taulo yangu, aliponiona alihamaki sana, wote walihamaki na kuvurugwa sana, nilisimama mlangoni nikiwa nimeegemea mlango nawatazama, natetemeka kwa hasira ila najaribu kujituliza, nilikuwa nawaza mengi linatoka hili linaingia hili, je nimrukie shingoni ning'oe koromeo, nfate kisu, nichukue panga, nitoboe macho, yaani mawazo yalikuwa yanapishana, alipiga magoti jamaa yangu na kulia kwa hofu nimsamehe.
Sijui ilikuwaje, nikamwambia sintowafanya chochote ila beba huyo mwanamke uende ukaishi nae kwako, inaonekana mnapendana sana, kwahiyo ni vyema mkaishi pamoja, mimi simuhitaji naona hata yeye hanihitaji pia ndio maana yuko na wewe, sasa muondoke ili mume huru na mapenzi yenu halafu na mimi nitatafuta aliye na mapenzi na mimi.
Siwatanii niko serious, na endapo mtafata haya maelekezo basi nitawasamehe bila chembe ya kinyongo ila mkijaribu kuongeza neno k**a ''Nisamehe, sirudii tena, na misamaha yoyote mtanitibua tuingie kwenye vita kali ya mauwaji".
Wewe ni mwanaume k**a mimi sidhani k**a neno msamaha linaweza kufuta ukweli kuwa umemlala mke wangu, kwahiyo mi naona jambo jema huyo akawe mke wako wewe."
Walikaa kimya wamejiinamia, nikamwambia mke wangu, naomba usimame ukachukue kila kilicho chako sasa hivi, akawa anataka kuomba msamaha anakuja kunishika miguu nilimpiga teke la mdomo meno mawili ya juu yakaanguka hapo hapo, midamu hiyo ikamtoka na sikujali wala nini, nikamwambia rafiki yangu, wewe chumbani kwangu bila shaka unapajua, nyanyuka uende ukamsaidie mpenzi wako kukusanya matambala yake muondoke kwangu, tena fanyeni haraka, akasimama na kuanza kuelekea chumbani, mimi nikaingia chumba kingine kuchukua mazaga mengine ya mke wangu, rafiki yangu akaitumia k**a chance kukimbia, alipita pale mlangoni k**a radi, akakimbia.
Usiku ule sikumgusa mwanamke maana niliona naweza kumuua au kumdhuru kwa hasira nilizokuwa nazo, nikamtoa nje nikafunga mlango, alilala nje nadhani itakuwa jikoni, kesho yake niliita waungwana nikawaeleza, na tukapanga zoezi la kumpeleka mke wangu kwa yule jamaa, tuliita gari ikabeba mizigo, na yule mwananmke mpaka kwa jamaa yangu, sikumkuta alikuwepo mke wake, tukamueleza kila kitu mke wake, tukashusha mizigo na mke wangu tukamuacha pale sisi tukaondoka zetu.
Mke wa jamaa akaanza mara ooh haujafata taratibu ulitakiwa umrudishe kwao umpe talaka mbele ya washenga maana akiumia utaulizwa na maneno mengi, nikamwambia anayetakiwa kumpeleka kwao sio mimi ni mume wako ambaye ndiye mume wake pia, na kuhusu talaka wala asijali imeshapita hiyo, yeye k**a hajaridhika ndio afunge safari aende kwao akajieleze ilikuwaje sio mimi, kwanza huo muda sina.
Nilivyofika pale kwangu, nilifunga nyumba nikaondoka kwenda kwenye ile lodge na simu zote nikazima, baadae nikapata wazo nikasajili laini mpya nikawa nawasiliana na watu muhimu,
Nilikaa lodge wiki ikabidi nipange chumba sehemu, nikalipa kodi ya miezi mitatu, nikanunua godoro, na ndoo ya kuogea, nikaishi hapo, nilikuwa naenda kulala tu.
Sikutaka kutafutwa na msuruhishi yeyote wala kiongozi yeyote, nilitaka niwe huru, nipate muda wa ku heal, nipate muda wa kuwa peke yangu bila kuingiziwa virus zozote kichwani kuhusu yule mwananmke wala ndoa.
Ni siku moja tu nilifunga safari mpaka pale nikaenda kumchapa talaka yake, mi nikatembea.
Jamaa yangu alituma watu wengi sana waje kunitafuta kazini lakini kila aliyenieleza upuuzi wake nilimpa onyo kali sana asirudie.
Walihangaika kunitafuta bila mafanikio, hata wa kwetu hawakujua nipo wapi isipokuwa mama yangu tu, nae alinitunzia siri.
Mwisho yule mke wangu alimng'ang'ania jamaa yangu akasema haondoki na lazima atamuoa maana yeye ndiye kamvunjia ndoa yake, akamwambia njia pekee ya kutomuoa na kumtoa pale kwake ni kumuua tu basi.
Mke wa jamaa nae kikawaka ikabidi aondoke, wakabaki wasaliti wawili na wakaanza kuishi japo mwanzo waligombana ila mwisho wakaishi.
Nilirudi kwenye nyumba yangu nilipo karibia kuoa, na mwisho wa siku nikaoa, nikawa napata habari kuwa yule mke wangu haelewani na jamaa kila siku ni vita na makesi yasiyoisha, mwanamke akawa mkatili kwa watoto wa jamaa na kubwa zaidi alianza kumsaliti na wanaume wengine pasipo jamaa kujua, maana kazi zake za kusafiri, ni dereva wa halimashauri moja hivi hapa nchini.
Nasikia jamaa anajuta mno, na Mungu asivyo athumani mwanamke niliyenae sasa ana unafuu mkubwa sana kuliko yule, yule alikuwa na kamdomo sana, akifungulia mdomo wake unaweza sema ni zile speaker za club, alikuwa na makelele sana nilikuwa navumilia tu, k**a unavyojua wanaume asilimia 95 tusichokipenda kwa mwanamke ni makelele, dharau, so alikuwa ameshanikera sana sikuwa na jinsi tu, alikuwa na kiburi sana, kwakweli nashukuru ni k**a jamaa yangu alinisaidia kutoa bomu ndani ya nyumba yangu, yeye alijikuta mjanja kumbe bwege tu na sasa anajuta.
Binafsi nimejifunza kitu hapa 👏👏
(Tuma jambo lako inbox unalohitaji kushauriwa, au kushare, zingatia uandishi wako, kuhariri ni kazi sana makosa yakiwa mengi.🙏)