30/08/2026
🎙️🔥 CHORUS KILLER WA ZAMANI JUMA NATURE ANAMTAJA WA LEO G NAKO!
Ukitaka kujua historia ya Bongo Flava, lazima ukae chini na mtu k**a Juma Nature mtu ambaye sauti yake kwenye chorus ilikuwa guarantee ya hit moja kwa moja!
🎶 Katika kipindi cha The Playlist cha Times FM hosted by Lil Ommy, legend mwenyewe anaimba baadhi ya chorus zake maarufu alizofanya na wasanii wengine 👇
🎵 "Zali la Mentali" — Profesa Jay ft. Juma Nature
🎵 "Nampenda" — Mike Tee ft. Juma Nature
🎵 "August 13" — Fid Q ft. Juma Nature
🎵 "Hili Game" — Juma Nature
🎵 "Mzee wa Busara" — Juma Nature 🎵 "Haipotei" — ft. Juma Nature
Nyimbo hizi hazikusimama tu zilitetemsha East Africa nzima! 🌍 Sasa hapa ndipo mambo yanakuwa interesting zaidi… Aliulizwa swali moja 👇 "Kizazi cha sasa, nani anachukua kijiti chako cha Chorus Killer?" Na bila kusita, Juma Nature alimtaja mtu mmoja tu 🎤 G NAKO.
🎤 Legend anamthibitisha mwingine. Hiyo ndiyo heshima ya kweli katika ulimwengu wa muziki.
🙌 Wewe unasemaje? Je, unakubaliana na Juma Nature kwamba G Nako ni Chorus Killer wa kizazi hiki? Au mna jina lingine akilini? Drop maoni yenu comments 👇👇