11/11/2025
🚨_|| AMEANDIKA FARHAN JR
Mimi siwezi kujadili HISIA bali HOJA, najadili KITU na sio MTU, we attack MATTER not the SUBJECT na uhalisia ni kwamba nitakuwa Mjinga kukasirishwa na Watu ambao wamewahi kunipost sana kunisifia hivyo wana haki zao pia Kikatiba kunipost wakichukia ila Mimi nasimamia misingi ya kazi yangu ama taaluma yangu, nimewachukulia k**a Watoto ambao Kibiblia hawapaswi kunyimwa mapigo japo wanapambana kupingana na maandiko.
Nitakapoona hapa Young Africans ni haki yao na nikapima nikaona ni haki basi bila kujali ni dhidi ya nani Mimi nitasimama nao na nionapo hapa sio haki siwezi kusimama nao, nikiona hapa Yanga wanastahili sifa zao nitawapa bila haya na nitakapoona hapa wanastahili kukosolewa basi nitawakosoa vikali bila kujali nani kapenda ama hajapenda, mifano ya Vita zao nzito ambazo mikono yangu iliandika bila hofu ipo na Mimi ni yule yule ambaye kwasasa nawaandika wao bila hofu yoyote ile.
Ushauri tu kidogo japo sio lazima hiyo Klabu ni kubwa saana tangu 1935 ina miaka 90 wakati Mkulima nimezaliwa 1997 na nina miaka 28 tu, Kalamu yangu haitishi k**a mnavyojaribu kupambana nayo, hakuna Mkubwa zaidi ya timu yenu hivyo tambueni thamani ya Logo yenu maana Kalamu ya Mwandishi haiwapi Yanga alama tatu, haiwakoseshi alama tatu wala haifanyi icheze vibaya, kuiweka Yanga, ninyi na Mkulima sehemu moja ni kuitukana taasisi hiyo Kongwe ipeni heshima yake, its Young Africans sio Kosovo ya Ifakara.
Kuna mengine siwezi kujadili kwasababu sio Utamaduni wangu, Mimi ni MNGINDO nimeingia Jandoni na nimetairiwa kwa Kisu cha Madafu bila uwepo wa Nesi wala sindano za Ganzi, mengine nayaweka kifuani na kuacha Uanaume ufanye kazi, hayo siyapi nafasi naona kwasasa zinajadiliwa zaidi HISIA kuliko UHALISIA, ukiona Watu wanataka tu kusifiwa basi kuna kitu hakipo sawa sehemu, naisubiri ikirejea International break k**a itakuwa vile vile basi hatutoacha.
Naona napostiwa postiwa sana nimeweka na picha nyingine hapo slide namba mbili inafaa kuitumia kwenye Makala zenu, unaweza kuzoom ukipenda.