21/09/2025
KUTOKA BOTSWANA: Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amekiri kwamba wamepokea taarifa kutoka CAF ikiwajuza kutoruhusiwa kuingiza mashabiki kwenye mechi yao ya mkondo wa pili ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Gaborone United kutoka Botswana.
Ahmed amesema wameanzisha mazungumzo na CAF ikiwemo kukata rufaa na baadae ndio watatoa tamko rasmi kwa mashabiki wao kujua mustakabali wa jambo hilo.
Simba jana ilicheza mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Gaborone United na kushinda kwa goli 1-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL)