06/08/2025
ZITTO KABWE NA UMALAYA WA KISIASA
Katika Dola la Urumi ya Kale Julius Kaizari alisalitiwa na rafiki yake wa karibu sana aliyeitwa Brutus. Wakati Kaizari anachomwa visu kuuawa ndani ya Bunge la Roma, Brutus alikuwa mmoja ya waliofanya ukatili ule. Kule Burkina Faso, Blaise Compaore alishiriki kwenye kuondoa uhai wa Thomas Sankara, wawili hao wakiwa marafiki wa karibu. Walichofanya Brutus na Compaore kinaitwa umalaya wa kisiasa (political prostitution).
Hapa Tanzania moja ya watu walioko kundi la Brutus na Compaore ni Zitto Kabwe. Mwalimu Nyerere aliwaita malaya wa kisiasa. Alianza kulelewa na Freeman Mbowe akiwa pale UDSM, Mbowe akamlipia hadi kula yake lakini mwisho akashiriki mapinduzi haramu yaliyofeli dhidi ya Freeman Mbowe CHADEMA. Akatimka na kuanzisha ACT. Baada ya mtikisiko wa CUF, Maalim Seif akampa Zitto nafasi na imani kutumia ACT kuingia Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) Zanzibar. Kupitia muungano ule na imani ile Zitto na ACT wakasimama na kuingia tena mjini kisiasa.
Baada ya kifo cha Maalim Seif, CT Zanzibar ikabaki kwenye GNU lakini Zitto akiitumia kufanya biashara zake na umalaya wa kisiasa na hata kushindwa kuhakikisha makubaliano ya Maalim Seif na CCM Zanzibar kuingia GNU yanafikiwa. Naona sasa kaamia CCM Bara kuendeleza umalaya wa kisiasa, Zitto anajua kwamba wana CCM wote wanaohamia ACT sasa hivi hawana nafasi kushinda chochote ila anachofanya yeye ni k**a Malaya. Anawapokea kutengeneza kelele (k**a urembo wa malaya), ili aweze kujenga uhalali wa kuendelea kubaki kwenye soko la umalaya wa kisiasa iwe kwa wanasiasa, Mamlaka au wafanyabiashara wakubwa.
Yoyote iwavyo, duniani hakuna umalaya wa kisiasa uliowahi kujenga taasisi yenye maisha. Tutakuwepo!