
19/02/2025
SIMULIZI:SAUTI YA KIFO
MWANDISHI: K. WAMBIA
MAWASILIANO (WSP)
+255 628 364 931
Sehemu ya 2
Ilipoishia.......
Ile nashuka kidogo tu namuona baba Juliet, ni pande la mtu, yuko na askari wawili wanaelekea nyumbani kwake, yeye hakuniona! Nikamwelekeza boda apitie uelekeo wa kule hotelini ili nipate sehemu nzuri ya kuwasiliana, mara ghafla.โฆ...
Endelea....
Uso kwa uso, Lori ya mizigo (semi tralel ilikuwa imepakia nondo) iligongana na basi ambalo lilikuwa linatoka kuoshwa, tairi ya mbele ya basi ilichomoka na kuigonga pikipiki yetu! tulianguka vibaya! Dereva alivunjika mguu ila mimi nikatoka salama, akachukuliwa kupelekwa hospitalini, mimi ikabidi niendelee na safari! Kumbuka nimebakiwa na dakika hamsini tu!! Nikachukua bajaji lakini nilipotaka kupanda tu nikadakwa, โbwana Joseph Aloyse, ...naam! ...uko chini ya ulinzi! Wale watu hawakuwa na chombo chochote cha usafiri, nilichofanya ni kumchomoa dereva bajaji ambaye alikuwa peke yake kwenye bajaji ambayo ilikuwa imewaka tayari! Akarudi ndani ya bajaji wakati huo nimeshaiondoa!!
Wakati tunaendelea na safari kwa mwendo mkali nikamweleza kinachoendelea, nikampa simu nikamwambia aitafute namba ya mwisho kumpigia Juliet, akaipata. Alipoipigia ile namba ikaita, akapokea mtu aliyejitambulisha k**a Mista Kisu, palepale ikabidi niegeshe bajaji, nikachukua simu, nikamwambia mimi ni Joseph! Akacheka sana, kisha akaniambia zibebaki dakika kumi โfika palm plain junction, shika njia ya kushoto, tembea kilomita tatu kisha shika njia nyembamba yenye seng'enge za bluu, vua suruali na shati ingia na pensi na fulana....uwe peke yako!โ akasisitiza nikichelewa hata sekunde, wanamkata shingo. Nikachukua bodaboda, kijana fulani hivi amesuka dred na amevalia ndala. Kwa namna anavyoendesha pikipiki ukiweka mabawa unapaa, kutokana na kuwa mda niliopewa ni mchache, nilimkazania aongeze spidi zaidi!. Ni kweli k**a alivyonielekeza safari yetu ilifikia kwenye seng'enge za blue, mita mia kuelekea eneo lile palikuwa hapawezi kupitika na pikipiki ikabidi tuachane mimi nikaingia!
โ...Huyu mwamba pale atatoka salama kweli! Asije kung'olewa meno k**a yule Dokta, na hivi ni mwepesi sijui!โ alijisemea dereva bodaboda huku akigeuza pikipiki yake, mara ghafla akapigwa mkasi na pikipiki mbili kisha vijana wanne waliovalia vikaragosi vyeusi usoni wakawa wanaingia na pikipiki zingine mbili! Walimuuliza amefika vipi kwenye eneo lile akawajibu โ...niliwaleta vijana wawili kuchukua madini waliyoyaficha ila ni k**a wameshindwa kuelewana wanapigana kule juuโ wanapigana!, wajinga hao ngoja tukawaonyeshe kazi! Alisikika kijana mmoja aliyekuwa na kifua kipana mithili ya mafiga ya kupikia msibani kisha wakapeana ishara wakaondoka kuelekea kule walikoelekezwa! โ...hawa wangenimaliza leoโ akawasha pikipiki akasogea umbali wa mita elfu mbili akaukaribia mji.
Nilifanya k**a nilivyoelekezwa. Nilipoingia ndani palikuwa panatisha sana, mwanga hafifu na pana vumbi jembamba nikajisemea โ Huwa najifanya mjanja, Leo nimedandia mtumbwi wa vibwengo!โ. Nilipokelewa na vijana wawili waliovaa mask na silaha mikononi, walinikagua wakaninyang'anya simu, hawacheki. Nilielekezwa kwa ishara nikafuata. Nilipovuka chumba kimoja nikaona miili mitatu imelala chini ikiwa imetapakaa damu โHawatikisiki, sijui wamekufa!โ kabla sijafikiria zaidi mbele yangu nikamuona mtu mmoja โni pande la mtuโ amenigeuzia mgongo, mkono wa kulia umeshikilia kisu na ule wa kushoto umening'iniza kichwa cha mtu. Nilitetemeka sana nikahisi nabanwa na haja ndogo na kubwa!
Nyumbani kwa akina Juliet hali ya hewa imechafuka. Kila wakijaribu kupiga simu haipatikani, na namba zangu hawakuwa nazo. Ikawa ni simanzi sana siku hiyo.
Joseph kijana wangu! โnikashikwa na butwaa!โ Naam. โKaribu katika ulimwengu wangu!โ โLakini...โ Hapana, wewe ni kijana ambaye k**a ningepewa vijana mia tano ningekuchagua wewe ukiwa mmoja tuโ
Maisha hayana saiti, unaweza kuishi popote, Mjini, kijijini, majini na hata kaburini k**a ukipenda. Pesa haina nembo kuwa hii imepatikana kihalali, kwa wizi au kwa kutakatisha! โ Binadamu tumeumbwa kutenda mema tu, mabaya ni matokeo ya Ibilisi kujikwezaโ nilimjibu kwa ujasiri ambao sikujua umetoka wapi! Kisha akanipiga kichwani na kitako cha upanga aliokuwa nao mkononi.
Katika Dunia ambayo walio wema ndio wanateseka na kusulubiwa, unahisi unafaidika na nini!? Hakuna, hahahaha, hakuna!!! HAKUNA! Dunia imejaa ufisadi, wizi, mauaji ya kutisha, wenye pesa ndio wanaongea, wema hamna sauti....Nataka nikupe sauti na mali (alipaza sauti kwa msisitizo) โK**a mafanikio yangu lazima yapitie kwenye njia yako, nitakufa masikini!โ nilimjibu bila woga. โUtakufa! MFUNGULIENI MLANGO!โ Ulifunguliwa mlango kuelekea kwenye chumba kingine ambacho kilikuwa kikitoa harufu kali sana, kina giza lakini kwa mbele kidogo kuna mwangaza hafifu lakini ni k**a vile kuna watu wawili wamefungwa mikono, tukapiga hatua kuelekea kule. Tulipofika katikati ya kile chumba taa zikawashwa! Mungu wangu! Nilisema kwa sauti nikashindwa kupiga hatua zaidi nikabaki nimesimama, nililia machozi! โEndapo utakataa agizo langu, nakumaliza! Namuua rafiki yako pia!โ ilinibidi nimuulize anachokitaka kwangu.
โUtapewa maelekezo wapi mtaenda na mnaenda kufanya niniโ Nitaenda lakini sitafanya hivyo kabla sijamuona Juliet na kabla hatujaenda naomba umwachie. Waliamrishwa wale vijana wawili wamfungue Juliet โAlaa, kwahiyo hawa washenzi kumbe yule pale ni Juliet, Julieeet! Oh My God! Haiwezekani, mbona amelegea, mmemuua, nakufa na wewe July, kwanini lakini, mbona maisha yangu yana mitihani namna hii!?โ Alinishika begani โHajafa, ila usipotekeleza majukumu, ninamtoa shingo k**a huyu kijana jeuriโ akanipiga kichwani na kichwa kile alichokuwa amekining'iniza.
Nilipandishwa kwenye gari jeusi kuelekea nisikokujua, njiani nilikuwa najiuliza โhivi ni kweli naweza kuhusika kwenye vitendo haramu nikiwa ninaona! Namkosea Mungu wangu!โ ilibidi nimuulize mwenzangu ambaye kumbe yeye pia amechukuliwa kinguvu, โSina hakika lakini nahisi ni viungo vya binadamu, hawa jamaa wanafanya hizo biashara, wanawateka watu kisha wanawatoa viungo vyao! Lakini pia wanafanya biashara ya madawa, kwahiyo kuna uwezekano huko tunakoelekea tukawa wafaulishaji kwenye halaiki au ukawa mbebaji!. Niliwahi kwenda mara moja nikafanikiwa lakini ni hatari sana!โ
Tulifika sehemu gari likazima ghafla! Tukazungukwa na maafisa usalama. Hawa walikuwa kwenye doria, wakakagua vitu vidogovidogo tu wakatuacha โLakini huenda Mungu ameamua kunitendea muujiza na sijui, nisichezee nafasiโ nilijisemea kimoyonimoyoni kisha kwa siri sana nikaonesha ishara ambayo lazima maafisa wangestuka. Baadae gari liliwaka tukaendelea na safari. Mbele kidogo gari likasimamishwa, dereva akataka kukaidi tukanyooshewa silaha na askari sita ikabidi tusimame. Wakati huo kiongozi akawa ametoa maagizo kwa kila kijana awe tayari kwa lolote, wakaziweka silaha zao tayari!
Tuliamriwa tutoke nje na mikono yetu iwe juu, mimi nilikuwa wa kwanza kutoka, hawa wengine walibaki ndani ya gari kwa muda wa dakika mbili, wakaanzisha mashambulizi, askari wakampiga mmoja wao risasi akaanguka. Dereva akawasha gari ili asogee tairi zikatobolewa, hakuna ujanja zaidi ya kujisalimisha! Tukak**atwa ukaanza upekuzi ndani ya gari. Kuna madawa ya kulevya, risasi na mabomu ya kutupwa kwa mkono. Kuna sanduku special ambalo lilikuwa gumu kufungua kwa kuwa funguo za hilo sanduku zilikuwa kule ambako mzigo ulikuwa unaenda!
โMzee tulia, tunalifanyia kazi, jeshi letu liko imara na tunaliami, lazima ufumbuzi utapatikanaโ alijibiwa Mzee Masoud ambae anaonekana mwenye ghadhabu sana. โK**a haiwezekani niachieni nishughulike nalo mwenyewe!โ โMtoeni nje!โ Alisikika mkuu wa kituo cha polisi akiunguruma kwa jazba mithili ya simba aliyejeruhiwa.
Akiwa njiani anarudi nyumbani simu yake iliita โMzee Masoud, heshima yako!โ โNaam, nani mwenzangu?โ Hatufahamiani lakini taarifa za kupotea kwa mwanao ninaifahamu! Yuko kwenye hatari ya kupoteza maisha, unalitambua hilo? โAmepotea na tunamtafuta, una habari gani kumhusu?โ โMimi ni Stansilaus Mkwere rafiki yake ambaye tulisoma wote Chuo kikuu. Kuna rafiki yangu amenipa taarifa mbaya sana kumhusu, ...Paaaah! Halloo, halooo, halo, halo.....hallo! Amekuaje? Mzee aliongeza spidi k**a swala afukuzwae na chui mpaka kwenye kituo chake cha mafuta, pale anakutana na Mr Stanley ambaye ndiye aliyewalenga wale Majambazi waliovamia kituo cha mafuta akawaua wote. Anamwelezea mkasa mzima! โPole sana mzee, naomba unikabidhi suala hili ndani ya masaa 24 nitakuwa nimepata pa kuanzia! Ila nakuomba uniruhusu nikabidhi lindo kwa dharura pia kuna watu naomba niongozane nao hivyo k**a wana majukumu ni vema wao pia wakakabidhi kwa dharura!โ Mzee Masoud alikubali na kuwatakia kila la kheri!
Mama Juliet akiwa katika hali ya majonzi, akitembeatembea huku na kule asijue la kufanya, ghafla anawaona watu mbele yake, โMama kuanzia mda huu uko chini ya ulinziโ โNyie ni akina nani?โ Sisi ni maafisa polisi, tunamtafuta Joseph mgonjwa aliyetoroka hospitalini bila kuruhusiwa, inasadikika wewe ni mmoja kati ya ndugu zake waliowahi kuja kumuona hospitaliniโ โLakini.....โ
โMama, utaongea tukifika kituoniโ
Walimchukua mpaka kituoni wakamweka mahabusu, kusema kweli hajui wapi Jose anaishi zaidi ya kukutanishwa na mwanae ambaye mpaka sasa hajui yuko wapi. Hana namna..!
Usikose sehemu ya tatu..