13/10/2025
                                            Ameandika hivi  kupitia insta story yake 
K**a Yupo Mtu Huyu Kwenye Familia Yako Basi
Mpigie Simu Ama Hata Txt Ya Kujua Hali Yake
Watu wengi sana wanaoitwa KICHWA CHA
FAMILIA ama WANAOONEKANA ndio msaada
Mkubwa kwenye familia zao, huwa wanapitia
MAMBO MAGUMU sana na hawana mtu wa
KUWASIKILIZA. Wengi huwa wanatumia sehemu
KUBWA ya KIPATO chao kusaidia ndugu zao.
Wengi hawaishi maisha wanayotamani kwa
sababu
WANAJITOA sana kusaidia ndugu zao.
Wengi wao huwa WANALAUMIWA sana
wanaposhindwa kufanya kitu bila kujali hali zao
na watu husahau kujitoa kwao kwa kila siku.
Wengi hujikuta wakiwa na MSONGO mkubwa wa
mawazo na HAKUNA anayewajali au kuwasikiliza.
Wengi wameingia kwenye MADENI kwa sababu
walikuwa wanatafuta pesa ili kusaidia shida za
ndugu zao.
Wengi huwa wanachelewa kuwa na MAENDELEO
BINAFSI kwa sababu wanatumia PESA zao nyingi
kwa ajili ya NDUGU. Wengi huwa WANAUMIZWA
sana na MANENO ya ndugu au KUSALITIWA na
ndugu waliowahi kuwasaidia. Wengi wao huwa ni
watu wenye HUZUNI za muda mrefu
K**a unae huyu mtu kwenye familia
onyesha thaman ya kujali, Na k**a ni
wewe basi Mungu akuzidishie zaid ya hapo
ulipo Amen
Wako Katika Kukumbushana
"Abal Bashar" Mpemba
  VISION TV 
  UPDATES 
  FOR MORE UPDATES