07/11/2024
Ndungu mjasiriamali.
K**a unaweka bidhaa zako Facebook Marketplace basi epuka makosa haya.
1. Kutopost Mara kwa Mara: unapoteza wateja wengi kwa kutopost bidhaa mara kwa mara kwenye Facebook Marketplace.
Usipost mara moja halafu basi ukaacha.
Hakikisha unarepost bidhaa kila baada ya siku 7 kupita ili algorithms ipushi zaidi k**a bidhaa mpya.
2. Kushindwa Kutumia Picha Bora: Bidhaa zinazovutia huuzwa zaidi, lakini wengi wanatumia picha zisizo na ubora, na kufanya wateja kupuuza.
3. Kutojibu Haraka DM (messanger): mteja anauliza bidhaa na utaratibu wa kupata wewe unamjibu baada ya siku 3 na kupelekea mteja kutafuta bidhaa kwingine.
4. Kutokuweka Maelezo: Watu wanapenda kujua undani wa bidhaa, lakini wengi hawatoi maelezo ya kina kwenye posti zao.
Mfano, k**a ni nguo size, je used au mpya. Hakikisha unaweka maelezo ya kutosha
5. Bei zisizo Wazi, usipoweka bei maana yake mteja anajua hapa kila mtu anabei yake. So anahisi kupigwa.
Uzuri wa marketplace unaweza kuweka bei mbili moja ya offa na nyingine anzia.
Hebu niambie kwenye comments umewahi kutumia Facebook Marketplace ??