12/01/2026
INAUMIZA: ATAKIWA KUKATWA BANDAMA LAKE HARAKA ILI AWEZE KUISHI, AWAOMBA WASAMALIA WEMA MIL 1.5 ILI AOKOE MAISHA YAKE.
https://youtu.be/qYEN1G3iRvs
ATAKIWA KUKATWA BANDAMA LAKE HARAKA ILI AWEZE KUISHI, AWAOMBA WASAMALIA WEMA MIL 1.5 ILI
Hakika hujafa hujaumbika hivi ndivyo tunavyoweza kusema, Wakati wewe unalalamika mafua tu yanakusumbua kijana huyu yeye kwa miaka kdhaa amekuwa akipambania afya yake walau aweze kupona na kurejea kwenye harakati zake za kila ziku za utafutaji wa ridhiki.
Kijana Jeremia Msimbazi anayesumbuliwa na maradhi ya BANDAMA hali inayompelekea kupungua damu kila siku huku akielezwa BANDAMA lake kwa sasa halifai na limeharibika kabisa njia pekee ya kunusuru maisha yake ni kuondoa bandama hilo kwa kulikata kabisa.
Kijana huyu ambaye ni mwenyeji wa Mwanza amewaomba wasamalia wema toka pembe zote za DUNIA kumsaidia gharama za kwenda kuondolewa BANDAMA hilo ambalo kwa mujibu wa Madaktari lisipoondolewa haraka linaweza kumletea shida kwa viungo vingine ndani ya tumbo k**a kuharibi INI na FIGO.
Zinahitajika Milioni 1.5 Ili akafanyiwe upasuaji wa kuondoa BANDAMA.
CHONDE Watazamaji wetu wa Mkoi Tv Online toka pande zote za Dunia tunaomba tumshike mkono
Kijana huyu ambaye amekimbiwa na mkewe baada kukumbwa na maradhi haya huku mkewe akidhani mumewe huyu ATAKUFA.
NAMBA ZA KUMCHAGIA
M-PESA-0741 161 607
HALLO PESA-0628 946 155
AU WASILIANA NA CHUMBA CHETU CHA HABARI KUPITIA
SIMU NAMBA 0713575718.
ATAKIWA KUKATWA BANDAMA LAKE HARAKA ILI AWEZE KUISHI, AWAOMBA WASAMALIA WEMA MIL 1.5 ILI Hakika hujafa hujaumbika hivi ndivyo tunavyoweza kusema, Wakati wew...