25/02/2023
Masikini bondia Tony Rashid amevuliwa ubingwa kufuatia rais wa Umoja wa Shirikisho la Ngumi Afrika, Houcine Houichi kugomea ushindi wa Mtanzania kwa mujibu wa kadi ya matokeo iliotumwa kwao na kupelekea Sabelo Ngebinya kupewa mkanda huo wa ubingwa akiwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kurejea kwao Afrika Kusini.
Houcine amekiri kumvua ubingwa Mtanzania huyo baada ya kutokana na matokeo yaliotumwa kwake tofauti na ambayo yalitangazwa baada ya pambano hilo.
Rais huyo wa ABU alisema kuwa: "Ndiyo, ni kweli, msimamizi alifanya hesabu isiyo sahihi kwa jaji wa tatu, matokeo yalipswa kuwa 113-115 lakini badala yake msimmizi aliandika 115-113 ambayo ni makosa kabisa kulingana na 'mastercard' aliyotuma. Lilikuwa pambano zuri sana lakini Tony Rashid alishindwa kwa Split Decision".
Sabelo amekabidhiwa mkanda huo leo akiwa katika uwanja wa ndege kabla kuondoka baada ya kuchukuliwa kwa Tony Rashid aliyetangazwa jana k**a mshindi.
🥊