22/04/2025
Clement Walid Mzize: Kinara wa Mabao Ligi Kuu Tanzania, Je Atamaliza na Kiatu cha Dhahabu?
Kipaji cha Muheza kinachong'ara Jangwani!
Kutoka kijijini Muheza, Tanga hadi kwenye jukwaa kubwa la soka Tanzania⦠Mzize ameibuka kuwa mmoja wa wachezaji wanaotajwa zaidi kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Akiwa na umri wa miaka 21 tu, na kujiunga na Yanga SC mwaka 2022, Mzize ameonyesha ukomavu mkubwa wa kimchezo. Anacheza k**a mshambuliaji wa kati na mara nyingine hucheza k**a winga wa kushoto. Kasi yake, utulivu mbele ya lango, na uwezo wake wa kupiga mashuti ya mbali vinamfanya awe mchezaji wa kutazamwa kila mechi.
Kwa sasa ana mabao 13 na ndiye kinara wa mabao ligi kuu, akiwa mbele ya washindani wake wakuu Prince Dube na Jean Ahoua walio na mabao 12 kila mmoja.
Kipaji chake kinatisha β lakini pia kinatia matumaini kwa Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania. Mashabiki wengi tayari wanamuona k**a βmchezaji wa kizazi kijacho.β
Je, unadhani Mzize atamaliza msimu akiwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania?
Tuandikie maoni yako hapa chini na usisahau ku-follow kwa taarifa zaidi za soka la nyumbani!