
17/05/2025
Katika msimu wa baridi kali ikiambatana na theluji ikiwa imefunika kila kitu … ndani ya misitu ya Finland, alikuwepo mtu mmoja – mwenye utulivu wa ajabu, macho makali k**a tai, na uwezo wa kulenga na kuua kimya kimya.
Jina lake ni Simo Häyhä (Simo Heiha) – aliyetajwa baadaye na maadui wake k**a “The White Death”.
Simo alizaliwa tarehe 17 Desemba 1905, huko Rautjärvi (Rautijaavi), kijiji kidogo kilichopo mpakani na Urusi. Alikuwa mkulima na mwindaji, mtu wa maisha ya kawaida, mpole, asiyeongea sana.
Akiishi maisha ya upweke, akitumia muda wake mwingi kwenye uwindaji na kilimo.
Lakini mbali na kuwa sura yake ya unyenyekevu, alikuwa na jicho kali lisilokosea shabaha, na roho ya ujasiri isiyoyumba hata mbele ya kifo.
Mnamo Novemba 30, mwaka 1939 – Jeshi la Sovyeti liliivamia Finland. Likiwa na silaha nyingi, magari ya kivita na wanajeshi maelfu, walidhani wataisambaratisha Finland mapema tu. Lakini hawakujua kwamba, walikuwa wamemkanyaga simba mkali.
Simo Häyhä (Simo Heiha), akiwa na umri wa miaka 34, aliitikia wito wa nchi yake kuipigania. Aliingia vitani akiwa na bunduki yake ndogo ya zamani aina ya M/28-30, iliyokuwa haina hata darubini (scope). Hakuipenda darubini kwa sababu mbili kuu:
Mng’ao wa darubini kwenye mwanga wa jua ungeweza kumuonyesha kwa adui.
Darubini ilimlazimisha kuinua kichwa chake juu zaidi ya mwinuko wa theluji – na hilo lingeweza kumgharimu maisha.
Akiwa amevalia mavazi meupe ya theluji, akijificha kwenye kingo za barafu, Simo huketi masaa kadhaa bila hata kusogea, wala kupepesa macho. Aliweka theluji mdomoni wakati akipiga risasi ili moshi wa pumzi yake usionekane kwenye baridi.
Kwa ustadi wa hali ya juu wa kupiga shabaha, aliua wanajeshi zaidi ya 500 wa Soviet kwa kipindi cha chini ya miezi mitatu!
Hawakujua ni nani anayewaua. Hawakumuona muuaji wala kumsikia. Waliona tu wenzao wakianguka tu ghafla, kimya kimya.
Kwa majeshi ya Soviet, aligeuka kuwa jinamizi la kila siku – wakaanza kumwita “The White Death” – Mauti Nyeupe.
Soviet hawakukaa kimya. Kujibu mapigo walituma ma-sniper wao bora kabisa kumtafuta mtu huyu mmoja. Hakuna hata mmoja aliyerudi. Wakatuma vikosi vya kijeshi eneo la tukio – hakuna kilichosaidia. Simo hakuwa tu snipa – alikuwa ni k**a kivuli kisichoonekana.
Baadhi ya siku, aliua hadi wanajeshi 25 kwa siku moja. Wakati mwingine hakurudi kambini kwa masaa 24 – akijificha chini ya theluji kwa kujichimbia handaki dogo lililomficha huku akiwatazama maadui kwa utulivu, kana kwamba tai wa mwituni.
Lakini hatimaye, Machi 6 mwaka 1940, Simo alipigwa risasi ya usoni – mdomo na taya yake vilivunjika vibaya. Hata hivyo, alinusurika kifo.
Alitibiwa kwa siku nyingi, na hata aliporudi katika hali ya kawaida, shape ya uso wake ulikuwa umeharibika vibaya.
Lakini hata hivyo, siku hiyo hiyo aliyopigwa risasi, mkataba wa amani ulisainiwa kati ya Finland na umoja wa soviet – ni kana kwamba kazi ya Simo ilikuwa imekamilika.
Basi bwana, Simo hakupenda mambo mengi. Baada ya vita, alirudi kijijini kwake akaendelea na maisha ya kawaida. Alikataa ofa nyingi zakuingia kwenye siasa za nchi yake. Aliendelea kuwinda, kukaa kimya na kufurahia mandhari ya msituni.. Alikufa mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 96.
Wachambuzi wa kijeshi duniani kote waliendelea kumtazama k**a snipa bora zaidi kuwahi kutokea. Hakuwahi kujigamba. Hakuwahi kuomba sifa aina yeyote. Lakini dunia ikamwandika kwenye vitabu vya historia kwa herufi kubwa.
Simo Häyhä (Simo Heiha)hakuwa shujaa wa kelele nyingi au majigambo – alikuwa mshindi wa kimya kimya. Katika hali ya kawaida, hakuwa na umbile la kutisha, wala sauti ya mamlaka – lakini alibeba sifa ya mauti nyeupe, na alilinda nchi yake dhidi ya nguvu kubwa kwa ustadi, subira, na akili ya vita isiyo na mfano.
Kwa wale waliobaki kusema walimuona:
“Hakuna aliyepiga risasi kwa utulivu k**a Simo. Alikuwa kivuli, baridi k**a theluji, lakini makali kuliko risasi yenyewe.
K**a wewe ni mpenzi sana wa kusoma soma, ninakitabu changu kizuri sana cha Jicho la GENGHIS KHAN.
Kitabu cha Jicho la Genghis Khan kinaangazia:
Mbinu za kiintelijensia zilizotumiwa na Wamongolia kabla na wakati wa uvamizi. Jinsi mak**anda wake hususani wa ngazi za Noyan walivyotisha kwa mauaji na kuvaa ngozi na damu za binadamu.
Mafuvu ya maadui wao kuyaning'iniza kwenye kambi zao za kijeshi.
Ulinganisho wa kiufundi kati ya ujasusi wa Wamongolia na ule wa Dola zingine k**a Warumi, Wachina, na Wapersia.
Urithi wa mbinu hizi kwa mataifa ya sasa na funzo kwa taasisi za kiusalama leo.
Kwa yeyote anayetaka kufahamu mizizi ya ujasusi wa kale na namna ambavyo maarifa haya yanaweza kutumika leo, kitabu hiki kinaelezea mambo yote hayo.
Kwa sasa kipo softcopy, unalipia TZS 9,999 kwa M-PESA +255755448591 ANANIAS KITAGE.