
09/09/2019
TB JOSHUA: XENOPHOBIA, KUKOSA UMOJA VYA ITAFUNA AFRIKA.
Tb Joshua Kiongozi wa kanisa la Tb Joshua Ministry, la nchini Nigeria amesema, xenophobia na kukosekana kwa umoja miongoni mwa Wafrika ndio kitu kinacho itafuna Afrika kwa sasa.
"Tuache tabia itakayo fanya wa Afrika wenzetu wajione hawaruhusiwi kutembelea nchi nyingine za Afrika." alikaliliwa Tb Joshua na ukurasa rasmi wa Facebook wa kanisa hilo.
Tamko hilo la Nabii huyo mwenye ushawishi mkubwa zaidi barani Afrika, ni muendelezo wa matamko yanayo tolewa na watu maarufu nchini Nigeria, kupinga kile kinacho endelea nchini Afrika kusini.
Inakalibia mwezi sasa tangu raia wa Afrika kusini wanzishe vurugu za kuwa shambulia raia wakigene, kwa kile walichokiita kunyang'anywa ajira zao na wa Afrika wamataifa mengine.