01/12/2025
Vijana nchini Tanzania wametakiwa kuendelea kuilinda na kuidumisha amani ambayo imeifanya nchi hiyo kutambulika duniani k**a moja ya mataifa yenye utulivu na mshik**ano mkubwa.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Madaba, Mhe. Omary Msigwa, alipokuwa akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Feo Girls, iliyopo wilayani Songea mkoa wa Ruvuma, wakati wa mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
Mhe. Msigwa amesema Tanzania imekuwa ikiheshimiwa kwa amani yake kwa miaka mingi, kiasi cha kuwa kimbilio kwa nchi ambazo zilipoteza utulivu. Hata hivyo, alionya kuwa matukio ya hivi karibuni yanaashiria dalili za kupungua kwa misingi hiyo, na hivyo ni jukumu la vijana kuhakikisha kuwa hali hiyo haijitokezi.
Kwa upande wao, wanafunzi wa Feo Girls wamesema amani ndiyo nguzo ya maendeleo ya taifa lolote, hivyo vijana hawana budi kuendelea kushirikiana na serikali na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha misingi hiyo inasimama imara.
Wamesema bila amani hakuna elimu bora, maendeleo ya kiuchumi wala fursa za ajira, hivyo ni wajibu wa kila kijana kuhakikisha matendo na kauli zao hazitetereshi utulivu wa nchi.