04/07/2025
Mjumbe wa Mkutano mkuu CCM Taifa Kutokea Wilaya ya Mbogwe Ndugu. *PATRICK GEORGE MSAFI* ambae ni Mkazi wa Masumbwe Kijiji cha Nyakasaluma amerejesha rasmi Fomu yake ya kuwania Kiti Cha Ubunge katika Jimbo la Mbogwe. Hii ni baada ya Kufanya vizuri katika nafasi aliyoaminiwa na Wana CCM tangu 2022 alipochaguliwa katika nafasi yake ya ujumbe. Amekuwa Kiongozi Msikivu,Mwenye hekima na msaada mkubwa ndani ya chama na jamii inayomzunguka.
Richa yakuwa mwaka 2020 *MSAFI* aliingia katika kinyang'anyiro cha ubunge bila Mafanikio yoyote hakukata tamaa na hakusita kukisaidia chama chake na watu wanaomzunguka tangu *2021*. Historia inaonyesha ,amekuwa ni kiongozi mwenye Hofu ya Mungu na upendo mkubwa kwa kila mmoja. Kiongozi mwenye utashi aneyeoongozwa kwa *Hekima* na *BUSARA* katika kufanya maamuzi Sahihi.
Uongozi ni kuonyesha njia *PATRICK* amefanya kazi hiyo kwa kuonyesha dira na muelekeo kwa vijana, Wanawake na makundi Maalum Kwa Vitendo.Kulingana na uzoefu wake katika Masuala ya uongozi na utumishi Bora kwa umma. Vikundi,Taasis Binafsi na za kiserikali zimenufaika na matunda ya *MSAFI* tangu alipochaguliwa kuwa Mjumbe wa mkutano Mkuu Taifa zikiwemo asasi za Kidini,Elimu,Michezo n.k
Aidha *PATRICK GEORGE MSAFI* Baada ya Kusaidiwa Michango Mbalimbali na kodi za Wananchi Kupitia Halmashauri ya Mbogwe Kipindii hicho ikiwa Bukombe Walimsaidia kuendelea na masomo ya Elimu ya Juu katika Masuala ya Uchumi na Fedha,aliamini Ajira ya kwanza ingemrudisha nyumbani kuwatumikia Waliomsomesha k**a ishara ya shukurani. Richa ya Kufanya kazi nje ya wilaya yake baada ya masomo, Jicho na moyo wake aliwaza nyumbani. Amerudisha Fadhila Mbogwe kwa Vitendo na kushiriki shughuli nyingi za maendeleo Kupitia chama cha mapinduzi na serikali yake.
Hata hivyo Kipimo cha imani yake ya utu na vitendo viliyotukuka, vimeendana na kauli mbiu ya Dokta *SAMIA SULUHU HASSAN* "KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE". Wananchi wa Mbogwe na Watanzania kwa ujumla wanamtakia kila la kheri *PATRICK GEORGE MSAFI* , katika