Ahmed Ally

Ahmed Ally Ahmed Ally Afisa Habari wa Simba Sports Club Tanzania 🇹🇿

Kituo kimoja cha Radio kimeripoti kuwa Mpanzu ameomba kuondoka Simba kwa kuwa amepata timu na anataka kununua Mkataba wa...
10/07/2025

Kituo kimoja cha Radio kimeripoti kuwa Mpanzu ameomba kuondoka Simba kwa kuwa amepata timu na anataka kununua Mkataba wake ambao thamani ya kuvunja Mkataba huo ni Milion 350

Taarifa hii ni mwendelezo wa taarifa za makusudi zenye lengo la kuzua taharuki ndani ya klabu yetu

Hakuna ofa yeyote ya Elia Mpanzu iliyowasilishwa kwenye klabu yetu wala mchezaji mwenyewe hajawasilisha ombi la aina hiyo

K**a haitoshi gharama ya kununua Mkataba wa Mpanzu ni zaidi ya thamani iliyotajwa na Radio hiyo

Kwa ufupi ni kwamba Volcano ataendelea kusalia Unyamani kwa misimu mingine ijayo

Kwenye mpango wa kuboresha kikosi chetu kwa ajili ya msimu ujao jukumu letu ni kuwabakisha Wachezaji wetu bora kisha kuongeza bora wengine

Mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuna taarifa za usajili kuhusu Simba wengine wanaihusisha Simba kwenye kila mchez...
10/07/2025

Mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuna taarifa za usajili kuhusu Simba wengine wanaihusisha Simba kwenye kila mchezaji ili kuwapa thamani Wachezaji wanaotaka kuwasajili

Taarifa tu ni kwamba usajili wetu safari hii unafanyika kwa umakini wa ICU, na Wachezaji waliopendekezwa na Mwalimu wameshasajiliwa na wengine wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili

Kwa sasa tunamalizia kutoa barua kwa wale tunaochana nao kisha tuanze kuvurumisha Thank You na baada ya hapo tuanze kudondosha chuma kimoja baada ya kingine

28/06/2025

Tuishi humu Wana Simba wenzangu!!!

Asante

Nianze na pole kwa Wana Simba kumaliza msimu bila ubingwa katika mashindano tuliyoshiriki hususan ligi kuu ya NBCWana Si...
27/06/2025

Nianze na pole kwa Wana Simba kumaliza msimu bila ubingwa katika mashindano tuliyoshiriki hususan ligi kuu ya NBC

Wana Simba tuepuke presha za wanaotuaminisha tumefeli kupita kiasi

Ni kweli hatujapata ubingwa lakini sote ni mashahidi kuwa timu yetu imepiga hatua kubwa sana kulinganisha na miaka ya nyuma na hilo ndio lilikua lengo letu kutengeneza timu ya ushindani.

Msimu huu tumefanikiwa kucheza Fainali ya CAF ambayo tumeshindwa kufanya hivyo kwa miaka 31

Msimu huu ubingwa wa ligi umeamuliwa na Dkk 45 za Kipindi cha pili cha mechi ya mwisho, wakati msimu uliopita tulipigania nafasi ya tatu

Points tulizofikisha msimu huu hatujawahi kufikisha kwa miaka minne iliyopita

Tulipotoka na tulipo ni tofauti sana, mwangaza wa mafanikio hauko mbali yetu

Si mara ya kwanza Simba kukaa miaka minne bila Ubingwa , tushakaa miaka mitano kutoka 2012 hadi 2017 lakini tulijipanga 2018 tukachukua kwa miaka Minne mfululizo.

Kupoteza mara 5 mfululizo dhidi ya Mtani kusitufanye tukajidharau

Madrid amepoteza El Classico nne dhidi Barcelona tena kwa vipigo vya vikali lakini katu huwezi kuwaona wanajitukana

Sio mfano wa kujivunia lakini lazima tukubali nyakati hizi hutokea kwenye mpira

Pamoja na ukubwa wote Manchester United wanaenda mwaka wa 13 bila Ubingwa, Sitaki kutoa mfano wa Arsenal

Mifano hii itupe taswira kuwa hatuko peke yetu kwenye mapito ya namna hii na hata hawa wanaocheka sasa yapo magumu waliyopitia

Ombi langu wangu Wana Simba, tuwape nafasi viongozi wetu wafanye tathmini na baada ya hapo watupe muongozo tunaendaje mbele kuipambania Simba yetu

Heshima yetu itarudi kwa kushik**ana na kusimama pamoja

Nguvu Moja!!!!!!!

Nimepata Pawa….Saa 1:30 Usiku leo nitatoa tamko kuhusu klabu yetu ya Simba
27/06/2025

Nimepata Pawa….

Saa 1:30 Usiku leo nitatoa tamko kuhusu klabu yetu ya Simba

Rasmi leo ndio umekua mtu mzima wa kimpira, ingekua kimaumbile tungesema umebaleghe hii leoMatusi, kejeli, na dhihaka zo...
07/02/2025

Rasmi leo ndio umekua mtu mzima wa kimpira, ingekua kimaumbile tungesema umebaleghe hii leo

Matusi, kejeli, na dhihaka zote utakazopokea leo ni ukaribisho kwenye ukubwa wako, yasikutishe tamaa na wala yasikuvunje moyo, KARIBU UKUBWANI

Umeumiza mioyoo ya Wana Simba, lakini wewe sio wa kwanza kwenye mpira, wapo wenzio makosa yao yaliwanyima Kombe la Dunia

Kosa hili linakuongezea ukomavu

Ndugu zangu Wana Simba najua tunahisira na kijana wetu lakini kila mtu kazini kwake anakosea

Na tukumbuke kabla ya kujifunga alishaisaidia timu kupata goli hivyo sukari na chumvi vimechanganyikana hii leo na bahati mbaya chumvi imezidi

Tukasirike lakini tusimchukie, na k**a haitoshi tumsamehe na tuanze kumtia moyo

Kipindi hiki anatuhitaji zaidi sisi familia yake kumtetea na kumpigania ili arejee kwenye utulivu wake wa kiakali na aendelee kuipigania Simba yetu

Tunapatia pamoja, tunakosea pamoja, tunajisahihisha pamoja tunasonga mbele l

Tumekabidhi Toyota Crown kwa Mteja wetu  Ni rahisi sana kuagiza na  fika ofisini kwetu Osterbay Jijini Dsm au tupigie kw...
21/08/2024

Tumekabidhi Toyota Crown kwa Mteja wetu

Ni rahisi sana kuagiza na fika ofisini kwetu Osterbay Jijini Dsm au tupigie kwa namba #0748898888

Ubaya Ubwela unaendelea Kwa Ushindi huu tumefuzu Kwenda Nusu Fainali
21/08/2024

Ubaya Ubwela unaendelea Kwa Ushindi huu tumefuzu Kwenda Nusu Fainali

Tumeanza Ligi Kwa furaha
21/08/2024

Tumeanza Ligi Kwa furaha

Na hapo hajaruka amejinyoooosha tuu
21/08/2024

Na hapo hajaruka amejinyoooosha tuu

Siku ya kazi 🏟️
21/08/2024

Siku ya kazi 🏟️

Kiongozi Bora Uwanjani
20/08/2024

Kiongozi Bora Uwanjani

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255777777770

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ahmed Ally posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share