Hazina TV

Hazina TV Official Global Hazna TV Plus Online Streaming Of Africa.

20/05/2024

WAZIRI BASHUNGWA ATUMIA HELIKOPTA KUKAGUA UREJESHAJI WA MAWASILIANO YA BARABARA YA DAR - LINDI.

Beki wa kulia wa Azam Fc Nathan Chilambo amesaini mkataba unaomfanya kuendelea kusalia katika viunga vya Chamazi kwa kus...
15/05/2024

Beki wa kulia wa Azam Fc Nathan Chilambo amesaini mkataba unaomfanya kuendelea kusalia katika viunga vya Chamazi kwa kusaini miaka miwili mpaka 2026.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema sekta ya utalii ina mchango mkub...
15/05/2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema sekta ya utalii ina mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi kupitia usafiri wa anga ambao ni kichochea kikuu cha ukuaji wa uchumi.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Kongamano la sita la usafiri wa anga Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Hoteli ya Verde Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 15 Mei 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza hatua iliyofikiwa na SMZ katika ukuaji wa sekta ya usafiri wa anga ya kutekeleza miradi kwa kukamilisha jengo la abiria uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Terminal 3, kuanza ujenzi jengo jipya la abiria Terminal 2 litakalohudumia abiria zaidi 1,300,000 kwa mwaka, ujenzi na ukarabati wa ujenzi wa jengo la zamani la Terminal 1, ujenzi wa jengo la biashara na ofisi katika jengo la tatu la abiria, jengo la kuhifadhi na kusafirisha hasa chakula vinavyoharibika kwa haraka, ujenzi wa vituo vitatu vya huduma za mafuta ya ndege, ujenzi wa uwanja wa ndege na upanuzi wa kiwanja cha ndege Pemba na jengo jipya la abiria na uwanja wa ujenzi wa kiwanja cha Nungwi.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewahimiza washiriki wote wa kongamano hilo kujadili na kutoa mapendekezo kwa kubainisha fursa zitazoweza kutumika katika sekta ya usafiri wa anga kwa manufaa ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki .

Kampuni ya huduma ya mawasiliano ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania, imesema imefanikiwa kurejesha kikamilifu huduma...
15/05/2024

Kampuni ya huduma ya mawasiliano ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania, imesema imefanikiwa kurejesha kikamilifu huduma ya internet hivyo wateja wake watanufaika Kwa kurejeshewa vifurushi vyao.

Hii ikiwa ni baada ya kutokea tatizo la kukatika Kwa nyaya chini ya bahari, taarifa hiyo imetolewa na kampuni pamoja na kuomba radhi kutokana na usumbufu huo.

✍🏼:

K**a ilivyo vita ya kuwania kiatu cha mfungani Bora Ligi kuu NBC Tanzania Bara ndivyo ilivyo Kwa upande wa mlinda mlango...
15/05/2024

K**a ilivyo vita ya kuwania kiatu cha mfungani Bora Ligi kuu NBC Tanzania Bara ndivyo ilivyo Kwa upande wa mlinda mlango bora kati ya Diara wa Yanga Sc na Matampi Coastal Union.

Unahisi nani kuchukua hii tuzo?

✍🏼 :

Yanga SC  wamebeba ubingwa wa Ligi kuu msimu wa 2023/24 ikiwa ni mara ya tatu mfululizo na kufanya kuwa Mabigwa wenye ma...
13/05/2024

Yanga SC wamebeba ubingwa wa Ligi kuu msimu wa 2023/24 ikiwa ni mara ya tatu mfululizo na kufanya kuwa Mabigwa wenye makombe 30 kabatini.

Full Time

Mtibwa 1-3 Yanga

Mwamuzi msaidizi namba mbili wa mchezo tajwa hapo juu, Shaban M***a kutoka Geita ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kw...
13/05/2024

Mwamuzi msaidizi namba mbili wa mchezo tajwa hapo juu, Shaban M***a kutoka Geita ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitano (5) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu.

Mwamuzi huyo alikataa bao halali lililofungwa na mchezaji Joseph Guede wa klabu ya Yanga kwa tafsiri yake kuwa mchezaji huyo alikuwa ameotea.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 42:1(1.8) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Miguel Gamondi ametozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kufanya vurugu ikiwemo kuwashambulia kwa maneno makali waamuzi wa mchezo tajwa hapo juu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha wawekezaji kutoka Korea k...
11/05/2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha wawekezaji kutoka Korea kuja Kuwekeza Zanzibar katika sekta mbalimbali ikiwemo uchumi wa buluu, ujenzi wa kumbi za mikutano ya kimataifa.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Mwenyekiti wa k**ati ya ulinzi ya kudumu ya Bunge la Korea , Mhe.Sul Hon na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe 11 Mei 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameishukuru Serikali ya Korea kwa kuendelea kuisaidia Zanzibar katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya sekta ya elimu, afya, uvuvi na mengineyo.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewashukuru ujumbe huo kwa kuitembelea Zanzibar.

Ujumbe huo pia uliambatana na Balozi wa Korea nchini Tanzania, Mhe.Kim Sun Pyo

Wizara ya Afya kupitia mashindano ya Afya na usafi wa mazingira kwenye ngazi za Majiji ambapo ilihusisha Majiji sita huk...
11/05/2024

Wizara ya Afya kupitia mashindano ya Afya na usafi wa mazingira kwenye ngazi za Majiji ambapo ilihusisha Majiji sita huku Jiji la Tanga likiibuka kuwa mshindi wa kwanza kwa 84%.

Likifuatiwa na Halmashauri ya Jiji la mbeya ambalo limepata 78%, Jiji la Arusha likiwa limepata 77%, Jiji la Dar es salaam likiwa limepata 66%, Jiji la Dodoma likiwa limepata 60% na Jiji la Mwanza likiwa limepata 57.

Pia kwa upande wa Majiji ya Arusha na Dar es Salaam yalikubwa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwa miezi sita (6) iliyopita hali iliyopelekea kukosa ushindi na kuchukuliwa na Tanga pamoja na Mbeya.

(✍🏼: )

11/05/2024

Half time Yanga 0-0 Kagera sugar
08/05/2024

Half time

Yanga 0-0 Kagera sugar

Miss USA 2023 Noelia Voigt mwenye umri wa miaka (24), ametangaza kujiuzulu nafasi yake Ili kuzingatia Afya yake ya akili...
08/05/2024

Miss USA 2023 Noelia Voigt mwenye umri wa miaka (24), ametangaza kujiuzulu nafasi yake Ili kuzingatia Afya yake ya akili.

Noelia alivalishwa taji hilo k**a miss USA katika shindano linalofanyika kila mwaka ambalo lilifanyika Septemba 2023.

"Kamwe usihatarishe ustawi wako wa mwili na kiakili, Afya yetu ni utajiri wetu," Noelia Voigt.

(✍🏼: )

Kikosi cha Yanga kinachoanza dhidi ya Kagera sugar katika kikosi hicho Pacome anaoneka akiwa yupo sawa na kuanza kwenye ...
08/05/2024

Kikosi cha Yanga kinachoanza dhidi ya Kagera sugar katika kikosi hicho Pacome anaoneka akiwa yupo sawa na kuanza kwenye mchezo huo.

Mchezo ni saa 1:00 usiku.

Wanakinondoni wachezea kichapo kutoka kwa Tanganyika Mashujaa FC Full time Mashujaa Fc 3-0 KMC Fc
08/05/2024

Wanakinondoni wachezea kichapo kutoka kwa Tanganyika Mashujaa FC

Full time
Mashujaa Fc 3-0 KMC Fc

Mtandao wa burudani za video TikTok ambayo ni kampuni mama ya Uchina ya ByteDance, imewasilisha pingamizi mahak**ani la ...
08/05/2024

Mtandao wa burudani za video TikTok ambayo ni kampuni mama ya Uchina ya ByteDance, imewasilisha pingamizi mahak**ani la kisheria dhidi ya serikali ya Marekani kuhusu sheria inayolazimisha kuwauzia programu ili iendelee kuwepo Marekani.

Rais wa Kenya William Ruto, ametoa agizo la kufunguliwa kwa shule zote Mei 13, 2024 ambazo zilifungwa kutokana na mafuri...
08/05/2024

Rais wa Kenya William Ruto, ametoa agizo la kufunguliwa kwa shule zote Mei 13, 2024 ambazo zilifungwa kutokana na mafuriko yaliyokuwa yamesababishwa na mvua kubwa.

Uamuzi huu unakuja kutokana na utabiri wa hali ya hewa ulionesha kupungua kwa mvua, awali shule zilipangwa kufunguliwa tena Aprili 29, 2024.

(✍🏼: )

Wizara ya Ujenzi, Timu ya Wataalam kutoka Wakala ya Barabara (TANROADS) ikishirikiana na Makandarasi, wanaendelea na zoe...
08/05/2024

Wizara ya Ujenzi, Timu ya Wataalam kutoka Wakala ya Barabara (TANROADS) ikishirikiana na Makandarasi, wanaendelea na zoezi la urejeshaji wa Miundombinu ya Barabara katika eneo la Songas ambalo nalo lilikatika katika Barabara Kuu ya Lindi – Dar es Salaam kutokana na mvua kubwa zilizonyesha na kuambatana na Kimbunga Hidaya.

Hadi kufikia leo Mei 08, 2024 kazi ya urejeshaji wa Miundombinu ya Barabara hiyo katika eneo la Somanga ipo katika hatua za ukamilishaji ambapo magari ya mawe yamesharuhusiwa kupita kuelekea maeneo mingine yaliyoathiriwa.

Watangazaji wa clouds Media B dozen pamoja na Adam Mchovu wamepewa usukani wa kujiendesha Jahazi kutoka kwa marehemu Gar...
08/05/2024

Watangazaji wa clouds Media B dozen pamoja na Adam Mchovu wamepewa usukani wa kujiendesha Jahazi kutoka kwa marehemu Gardner G Habash 'Captain' wakiungana na watangazaji walikuwepo akiwemo Bantu pamoja na dj ommy.

Address

Magomeni Mapipa
Dar Es Salaam
20283

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hazina TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Hazina TV:

Share