
10/02/2025
UNAYE KATA TAMAA, SIKIA HILI.
Yakukufanya ukate tamaa ni mengi.
Uache kuendelea na hilo jambo ni mengi.
Umkasirikie Mungu kwa kuacha au kuchelewa kukufanyia ulichokuwa umemuomba.
Yakuamua kujiua nayo yapo mengi.
LAKINI PIA
Yapo Mengi mazuri ya kukufanya Uendelee mbele.
Ambayo Mungu amekufanyia toka utoto wako mpaka hapo ulipo ni mengi.
Ambayo watu wamekufanyia toka utoto wako, hapo ulipo ni mikono ya watu wengi imehusika kufika wewe hapo.
Wala siyo mkono wa mtu moja, usijindaganye.
Kumbuka: hili kila siku.
Wewe ni mti, ulio kwenye udongo.
Mazuri yote yanayo tokea kwenye mti kuna visababisho vingi sana.
Ambavyo ni jua, maji, mbolea nk.
Vyote hivyo vinapochaganyikana ndipo mambo mazuri yanatokea kwenye huo mti.
Na mtu anapatwa na mambo mengi ya kuumiza hayo yote ni maji, jua na mbolea (takataka). -Yote yanayo kutokea ni mbolea.
KUMBUKA LINGINE HILI
Kule uliko toka siyo kwako tena, kwako ni huko mbele , lakini na hapo ulipo (kwenye hali uliyo nayo) unatakiwa kutoka maana hicho ni kituo cha wewe kufika kwenye hatma yako.
Hata k**a umebaki na fimbo tu vipige vikwazo uendelee mbele.
Hata k**a umejaa ukoma, nyanyua miguu yako piga hatua mbele.
La mwisho la Kumbuka ni hili.
Kukata tamaa, kumkasirikia Mungu, kujiua, kuacha wokovu au utumishi, kurudi nyuma kwa sababu zozote unazo ziona hakuna kitakacho badilika.
Sana sana utaangukia kwenye chuma cha moto.
Wapo watu waliwahi kufanya huo ujinga lakini waliongeza matatizo zaidi.
Soma kitabu cha Yona sura ya nne yote.
Mungu haendeshwi, hatawaliwi, wala hafanyi kila tunalo litaka anafanya matakwa yake.
Ukiweza soma Wafalme wa kwanza sura ya kumi na tisa utakutana na mtu wa Mungu Eliya naye alikutana vipindi vya kukatisha tamaa lakini Mungu alimwambia ainuke ale na safari iendelee.
Hata wewe ujue safari bado inaendelea.
Kiti chako cha ukuu bado kinakusubiri, na walioandaliwa kukushangilia nao bado wanakusubiri.
Piga hatua mwanaume, mwanamke hata k**a kwa kujivuta, kutambaa, kukimbia au kupaa cha msingi tu ufike.
Usitumie siku za wanadamu, (siku za wanadamu jumatatu mpaka jumapili yaani kuhesabu siku) utazidi kukata tamaa.
Tumia siku za Mungu haziwahi wala hazichelewi. Mungu anasiku yake aliyoiandaa kwa ajili yako.
Neema na Amani ya Yesu Kristo iwe nawe, Amina.
Shalom!!