06/08/2025
JKT,JKU WAWAKILISHI WA TANZANIA CAF
Na
Cosmasy William Choga
Kenya inatazamiwa kuwa mwenyeji wa mechi za kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF CECAFA 2025. Michuano hiyo itafanyika Septemba 4-16 jijini Nairobi, Kenya.
Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) lilituma maombi ya kuandaa mashindano ya kanda ambayo yataleta pamoja timu nane.
"Tunafuraha kwamba michuano hiyo itarejea Kenya baada ya ile ya uzinduzi kuandaliwa hapo 2021," alisema Yusuf Mossi, Mkurugenzi wa Mashindano ya CECAFA.
CECAFA iliazimia kuandaa michuano hiyo kabla ya Septemba 18, 2025, ili kuruhusu wachezaji kupatikana kwa ajili ya timu zao za taifa katika awamu ya awali ya mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia la Wanawake U-20.
Vyama Wanachama vya Sudan, Somalia, Eritrea na Djibouti hawatatuma timu kushiriki michuano hiyo.
Mabingwa watetezi Commercial Bank of Ethiopia (CBE) FC na Yei Joint Stars ndizo timu pekee zilizojitokeza katika matoleo yote manne ya mwisho ya mchujo.
Washindi wa mchujo wa Kanda watawakilisha CECAFA kwenye Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF 2025.
Timu nane zitakazoshiriki michuano hiyo ni pamoja na; Top Girls Academy FC (Burundi), Kenya Police Bullets (Kenya), Yei Joint Stars FC (Sudan Kusini), JKT Queens (Tanzania), Commercial Bank of Ethiopia FC (Ethiopia), Kampala Queens (Uganda), Rayon Sports Womens FC (Rwanda), JKU Princesses FC (Zanzibar)
Sport STAR TV