Scope Media

Scope Media Tanzania Online Media deals with Sports & Entertainment news from Africa
(4)

Vilabu vikubwa vya soka Tanzania Simba na Yanga vimeendelea na pre season zao kwaajili ya kujiweka sawa na msimu mpya wa...
08/08/2025

Vilabu vikubwa vya soka Tanzania Simba na Yanga vimeendelea na pre season zao kwaajili ya kujiweka sawa na msimu mpya wa soka 20625/2026

Yanga wanafanya Pre season yao kwenye uwanja wa KMC Complex Dar es Salaam na Simba SC wanafanya Pre season yao Ismailia Misri.

"Hongera sana Aviola kwa Kushika nafasi ya 5 CAF Sasa kufanya hili jambo Linoge Tunaomba mechi moja ya kirafiki ili kina...
08/08/2025

"Hongera sana Aviola kwa Kushika nafasi ya 5 CAF Sasa kufanya hili jambo Linoge Tunaomba mechi moja ya kirafiki ili kina Doumbia na Pacome na wao wawapongeze"

Ameandika Meneja wa habari na mawasiliano wa Yanga SC Ally Kamwe kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa msimamo wa viwango vya ubora Afrika ambapo kwa Tanzania Klabu ya Simba ipo nafas...
08/08/2025

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa msimamo wa viwango vya ubora Afrika ambapo kwa Tanzania Klabu ya Simba ipo nafasi ya 5 (Alama 48), Yanga ipo nafasi ya 12 (Alama 34) na Namungo ipo nafasi ya 75 (Alama 1)

Katika orodha hiyo iliyoonyesha vilabu 75 Bora Afrika Azam FC haipo kabisa huku ikiwa imeshiriki michuano ya vilabu Afrika mara nyingi zaidi ya Namungo FC.

Ligi ya Kuu ya Uingereza (EPL) imetangaza kusitisha kampeni ya Stonewall's Rainbow Laces kwa msimu wa 2025–26 na badala ...
08/08/2025

Ligi ya Kuu ya Uingereza (EPL) imetangaza kusitisha kampeni ya Stonewall's Rainbow Laces kwa msimu wa 2025–26 na badala yake, ligi itazindua kampeni yake itakayolenga kutoa elimu kupitia programu za jamii na kushauriana na vilabu na vikundi vya mashabiki.

Uamuzi huu unakuja baada ya Mahak**a Kuu kutoa uamuzi kuhusu ufafanuzi wa mwanamke chini ya Sheria ya Usawa na huku kukiwa na wasiwasi kutoka kwa baadhi ya wachezaji na mashabiki kuhusu kampeni ya awali.

Leo ni kumbukizi ya kuzaliwa ya kiungo wa ulinzi wa kimataifa kutoka Uganda ambae alikuwa akicheza Yanga SC Khalid Aucho...
07/08/2025

Leo ni kumbukizi ya kuzaliwa ya kiungo wa ulinzi wa kimataifa kutoka Uganda ambae alikuwa akicheza Yanga SC Khalid Aucho

Aucho amezaliwa August 8, 1993 na Leo anatimiza miaka 31. Tuungane kwa pamoja kumtakia Happy Birthday Khalid Aucho

Mchezaji wa Yanga SC Kibwana Shomari kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ✍🏿 "Ukawe Msimu mwema na wa Mafanikio k...
07/08/2025

Mchezaji wa Yanga SC Kibwana Shomari kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ✍🏿

"Ukawe Msimu mwema na wa Mafanikio kwetu Wananchi".

Baada ya mwandishi wa habari Fabrizo Romano kuthibitisha kuwa Manchester United imekamlisha usajili wa Mshambuliaji Benj...
07/08/2025

Baada ya mwandishi wa habari Fabrizo Romano kuthibitisha kuwa Manchester United imekamlisha usajili wa Mshambuliaji Benjamin Sesko (22) kutoka klabu ya Rb Leipzig, Mchezaji mpya wa Yanga Mohamed Hussein ambae pia ni Shabiki wa Manchester United kupitia ukurasa wake wa insta story ameandika ujumbe kuuliza "Kwani sisi na Manchester United lini 😁".

Je kwa usajili huu unaiona Manchester United ikiwa tishio msimu ujao..?

Wachezaji watatu Waafrika wamejumuishwa kwenye orodha ya wachezaji 30 watakaowania Tuzo ya Balloon D'OR 2025 Wachezaji h...
07/08/2025

Wachezaji watatu Waafrika wamejumuishwa kwenye orodha ya wachezaji 30 watakaowania Tuzo ya Balloon D'OR 2025

Wachezaji hao ni Mohamed Salah (Misri/Liverpool), Serouh Guirassy (Guinea/B. Dortmund) na Achraf Hakimi (Morocco/PSG) Waafrika hawa wananungana na wachezaji wengine 27 kutoka Manara tofauti ambao ni Vinicius Jr, Lamine Yamal, Cole Palmer, Desire Doue, Gianluig Donnarumma, Denzel Dumfries, Erling Haaland, Jude Bellingham, Victor Gyokeres, Harry Kane, Robert Lewandowski, Kylian Mbape, Fabian Ruiz, Pedri, Declan Rice, Raphinha, Vitinha, Virgil Van Djik, Florian Wirtz, Michael Olise, Nuno Mendes, Joao Neves, Scott Mctomnay, Oussmane Dembele, Lautaro Martinez, Alexis Mac Allister na Khvicha Kvaratskhelia.

Je nani anastahili kutwaa tuzo hii mwaka 2025..?

Kocha mkuu mpya wa Singida Black Stars Miguel Gamondi leo ameongeza mazoezi ya kikosi hicho kilichokita kambi yake Jijin...
07/08/2025

Kocha mkuu mpya wa Singida Black Stars Miguel Gamondi leo ameongeza mazoezi ya kikosi hicho kilichokita kambi yake Jijini Arusha kwaajili ya kujiandaa na msimu wa soka 2025/2026

Gamondi ambae amewahi kutwaa Ubingwa wa ligi kuu ya NBC, Ngao ya Jamii na Kombe la Shirikisho la CRDB amerejea nchini hivi karibuni kwaajili ya kuiongoza Singida Black Stars ambayo itakuwa na kibarua kizto kwenye michuano ya Kimataifa ya CAFCC.

Klabu ya Yanga imesaini mkataba wa udhamini na Kampuni ya Haier wenye thamani ya Tshs Bilioni 3.3 kwa mkataba wa miaka m...
07/08/2025

Klabu ya Yanga imesaini mkataba wa udhamini na Kampuni ya Haier wenye thamani ya Tshs Bilioni 3.3 kwa mkataba wa miaka mitatu.

Logo ya Haier itakaa kwenye mkono wa jezi upande wa kushoto.

"Biashara k**a hizi zinapokuja mchezaji ambae na mkataba na klabu A alafu klabu B ikawa inamuhitaji, cha kwanza ambacho ...
07/08/2025

"Biashara k**a hizi zinapokuja mchezaji ambae na mkataba na klabu A alafu klabu B ikawa inamuhitaji, cha kwanza ambacho kinatangulia ni mazungumzo kati klabu na klabu haya mazungumzo yanafunguka pale ambapo mchezaji anataka klabu isikilize ofa zinapokuja mezani pale anapotaka kuondoka

Haya mazungumzo yanahusisha pesa ya usajili ya kumuhamisha mchezaji kutoka kwa klabu A kwenda kwa klabu B, alafu inakuja sign on fee ambayo inamuhisisha klabu inayomtaka mchezaji na mchezaji mwenyewe kwahiyo sisi k**a taasisi tumezungumza na mchezaji na tumepokea ofa tukishirikiana nae

Kwa sababu hata hizo ofa ambazo zinatajwa kuwa zimekuja Kuna ofa ambazo klabu inakubali kabisa kwamba hizi fedha tumekubali hili dili lifanyike, lakini upande wa Mchezaji unakuta maslahi sio rafiki au mchezaji hataki kwenda kwenye nchi husika hataki kucheza ligi

Sio suala la fedha peke yake muda mwingine Kuna masuala ya timu, Mazingira na maslahi na mara zote klabu ya Yanga imekuwa Karibu na Mzize kujadiliana nae vitu vyote hivyo, sio kwamba klabu ikishakubali hela yake tu haina inachofatilia kwa mchezaji

Kwa mfano zipo baadhi ya ofa ambazo klabu iliona hazina maslahi mazuri kwa mchezaji kwa mfano Kuna dili ilikuja ya timu kutoka Libya fedha zilikuwa nyingi kwa upande wa Mchezaji na klabu lakini tukaangalia Mazingira na profile ya timu yenyewe pamoja na umri wa Mchezaji wapi anatakiwa anende pande zote mbili tukasema hii dili hapana kwahiyo huyu sio mchezaji ambae tulimsajili tu kutoka sehemu ni mchezaji ambae anabeba Maendeleo ya soka la klabu ya Yanga kwahiyo ni lazima tuhakikishe anakwenda mahali sahihi".

Meneja wa habari na mawasiliano wa Yanga SC Ally Kamwe akizungumza kupitia Sports Hq ya EFM kuhusu usajili wa Clement Mzize.

Mudathir Yahya amechaguliwa kuwa Man of the Match kwenye mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Mauritania uliomalizika kwa Ta...
06/08/2025

Mudathir Yahya amechaguliwa kuwa Man of the Match kwenye mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Mauritania uliomalizika kwa Tanzania kushinda goli 1-0.

Address

Tandika

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Scope Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share