02/10/2025
Bernardo Lopes, mchezaji chipukizi wa soka kutoka Rio De Janeiro Brazil, ambaye anacheza kwenye akademi ya Botafogo
Hali aliyonayoo usoni Bernardo imevuta hisia za watu wengi na kufanya picha zake siku za hivi karibuni kusambaa sana kwenye mitandao ya kijamii
Sasa swali ni je hali yake ya makovu aliyonayo usoni imesababishwa na nini?
Ukweli ni kwamba wakati Bernardo akiwa na umri wa mwaka mmoja tu alipata ajali mbaya ya kumwagikiwa na Maji ya moto akiwa nyumbani kwao.
Mama yake alikuwa akichemsha Maji ya kuoga kwenye birika, lakini alitoka kidogo kwenda nje na Bernardo akaingia jikoni na kwa bahati mbaya akavuta birika lenye maji yanayochemka ambayo yalimmwagikia usoni na mwilini mwake.
Madaktari wengi walidhani angekufa kutokana na kuungua vibaya sana, lakini baada ya miezi 7 ya upasuaji, kupandikizwa ngozi na muda wa kulazwa hospitalini aliweza kuendelea vizuri
Tangu wakati huo, alipenda kucheza mpira wa miguu. Alianza kucheza soka la mtaani na wajomba zake.Kisha alijiunga na akademi ya mtaani, na hivi majuzi alicheza katika mashindano mbele ya maskauti na baada ya kuvutiwa nae alichukuliwa na Botafogo. Baada ya kufanya majaribio yenye mafanikio, sasa ni sehemu ya wachezaji chipukizi wanaocheza kwenye akademi ya Botafogo na tayari amecheza mchezo wake wa kwanza akiwa kwenye akademi ya Botafogo
Bernardo ni mfano wa Hadithi ya kutokukata tamaa, ujasiri na kujiamini, kwani haogopi wala haoni haya juu ya makovu yake badala yake anaonyesha kipaji chake.
Image: Rising Ballers