21/04/2023
TANGAZO LA AJIRA KUTOKA WIZARA YA AFYA
Wizara ya Afya kupitia Kibali cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na. FA.97/128/01/”B”/72 cha tarehe 20 Aprili, 2023; Inatangaza nafasi za kazi 247 za Kada za Afya.
WIZARAya Afya imetangaza nafasi za ajira 247 zikihusisha madakitari bingwa 30, baada ya kupata Kibali cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Aprili 20, 2023.
1. Daktari daraja la II nafasi 15
2. Daktari wa meno daraja la II nafasi 10
3. Mfamasia daraja la II nafasi 10
4. Afisa Muuguzi daraja II nafasi 15
5. Afisa Muuguzi msaidizi daraja II nafasi 40
6. Afisa Mteknolojia daraja la II nafasi 15
7. Mteknolojia daraja la II nafasi 48
8. Mhandisi vifaa tiba daraja II nafasi 10
9. Fundi sanifu vifaa tiba daraja II nafasi 15
10. Fiziotherapia daraja la II nafasi 10
11. Afisa afya mazingira daraja II nafasi 10
12. Afisa afya mazingira msaidizi daraja II nafasi 15
13. Mtoa tiba kwa vitendo daraja II nafasi 4
Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa hospitali za rufaa za mikoa ya Kigoma, Katavi, Sumbawanga, Songea, Njombe, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Simiyu, Geita, Shinyanga, Ttabora, Singida, Manyara, na Mara.
Maeneo mengine ni Hospitali ya Kanda ya Chato, na Mtwara. Hospitali ya magonjwa ambukizi Kibbong’oto na vyuo vya afya.
Muda wa kutuma maombi haya ni ndani ya wiki mbili (2) tangu tarehe ya kutoka kwa Tangazo hili. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 04 Mei, 2023 saa 5:59 Usiku. Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ajira wa Wizara unaopatikana kupitia tovuti www.ajira.moh.go.tz.
Waombaji wote mnakumbushwa kuwa makini mnapowasilisha maombi kuhakikisha umejaza vizuri vipengele vyote vinavyotakiwa kwenye mfumo ikiwa ni pamoja na kuzingatia maelekezo ya kwenye tangazo kuambatisha nyaraka zote zinazohitajika.