
14/06/2025
Shilingi ya Tanzania imeimarika kwa kasi na kuwa miongoni mwa fedha zinazofanya vizuri zaidi duniani. Hii inatokana na kuongezeka kwa mapato ya dola kutoka sekta za dhahabu, kilimo, utalii na usafirishaji, pamoja na kanuni mpya zilizowekwa kuhusu matumizi ya fedha za kigeni nchini.
Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha wa BoT, Emmanuel Akaro, amesema sababu kubwa ya kuimarika kwa shilingi ni kupanda kwa bei ya dhahabu duniani, ambapo sasa inauzwa zaidi ya dola 3,300 kwa wakia moja. Tanzania huzalisha wakia milioni 1.9 za dhahabu kwa mwaka, hivyo mapato kutoka sekta hiyo yameongezeka kwa karibu dola bilioni 2.
Akaro ameongeza kuwa sekta ya utalii nayo imechangia kwa kiasi kikubwa, ambapo mwaka jana Tanzania ilipokea watalii milioni 2.6 walioliingizia Taifa Dola bilioni 3.9 ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na Dola milioni 715 zilizopatikana mwaka 2020 wakati wa janga la UVIKO-19.
Zaidi tembelea swahilitimes.co.tz