Mediawireexpress

Mediawireexpress Your News Hub for Uncovering Africa's untold narratives , one video at a time .

24/07/2025

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewatoa hofu wananchi kuhusu taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa mabaki ya viungo vya binadamu yamekutwa eneo la Magole Mpiji, likisema kuwa taarifa hiyo ni ya zamani na si tukio jipya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Julai 24, 2025 na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo SACP Jumanne Muliro, tukio linalozungumziwa lilitokea mwaka 2014 na lilishachunguzwa kwa kina na mamlaka mbalimbali, huku wahusika kufikishwa mahak**ani kwa mujibu wa sheria.

“Taarifa ya tukio hilo ni ya zamani miaka 11 iliyopita na ilitolewa ufafanuzi wake tarehe 22.7.2014 na aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam wakati huo”, imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Polisi wamesema kuwa katika tukio hilo, watu wanne wakiwemo madaktari na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU) walik**atwa kufuatia taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kuwepo kwa viungo vya miili ya binadamu vilivyotupwa katika bonde la Mto Mbezi eneo la Magole Mpiji, Kinondoni.

Uchunguzi uliohusisha Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wizara ya Afya na taasisi nyingine za uchunguzi ulibaini kuwa viungo hivyo vilitolewa kwenye maabara ya mafunzo ya IMTU na kutupwa kinyume cha taratibu.

Waliok**atwa walifikishwa mahak**ani mbele ya Hakimu Mfawidhi wa wakati huo, Kwey Rusema, ambapo Wakili wa Serikali Magoma Mtani aliwasomea mashtaka yanayohusiana na utupaji huo haramu wa mabaki ya miili ya binadamu.

Jeshi la Polisi limeonya kuwa halitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaosambaza taarifa za uongo au zenye lengo la kuzusha taharuki miongoni mwa wananchi.

24/07/2025

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila amefanya ukaguzo wa mwenendo wa usafiri na usafirishaji wa abiria kwa kutumia magari ya mwendokasi kwenye kituo cha Kimara Mwisho.

Akiwa kituoni hapo Chalamila ameonyeshal kutoridhishwa na ufanyaji kazi wa mabasi hayo kwani yapo machache huku wenye mahitaji maalum kutokuwa na mazingira wezeshi kutumia usafiri huo.

Meneja wa Operesheni kutoka wakala wa Mabasi yaendayo haraka amesema upungufu wa mabasi unatokana na uchakavu wa mabasi kwani mabasi yanayotumika kwa sasa yapo 60 pekee kati ya 200 yaliyoanza kufanya kazi 2015.

Wakala huyo ameeleza kuwa mabasi mengi ni chakavu na yanashindwa kufanyiwa ukarabati kutokana na vifaa kuhitajika kuagizwa nchini China.

24/07/2025

kifuatacho.....

24/07/2025

ais wa TLS wakili Boniface Mwabukusi amefanya maombi maalum kwaajili ya taifa la Tanzania akiliombea kurudi katika misingi ya kuasisiwa kwake na kudumishwa kwa undugu, amani, utu, haki, hekima na mshik**ano.

Mwabukusi amefanya maombi hayo Julai 23, 2025, aliposhiriki kongamano la msaada wa kisheria la mwaka 2025 lilofanyika Jijini Arusha.

24/07/2025

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema kuwa chama hicho hakiogopi vitisho, ukandamizaji wala hila dhidi ya wapinzani, na kitaendelea kusimama kidete kutetea haki, uhuru na maisha ya Watanzania wote.

Akizungumza Julai 23, 2025, wakati wa kutoa salamu za chama katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arumeru, Albert Elias Mollel, huko Ngaramtoni mkoani Arusha, Heche amesema kuwa taifa haliwezi kuendelea kwa viongozi wa umma kutumia mabavu kuwanyamazisha wanaowakosoa.

Aidha Heche ametoa matumaini kwa wanachama wa CHADEMA na Watanzania wote waliopoteza imani, akisema kuwa ushindi wa mabadiliko ni suala la muda tu.

24/07/2025

Marcus Rashford amejiunga na FC Barcelona kwa mkopo kutoka Manchester United, kwa mkataba wa mwaka mmoja unaoisha Juni 30, 2026, na Barcelona ina chaguo la kumnunua mwishoni mwa mkopo huo.

24/07/2025
24/07/2025

Britain’s top air force officer has angrily avoided questions about Gaza, while his colleague pushed a journalist out of the way.

Air chief marshal Sir Rich Knighton hurried to a taxi outside Savoy Place in central London on Thursday, while being grilled by Declassified about his aerial surveillance of the conflict.

As Knighton’s car sped away, news broke that his Israeli opposite number, Major General Bar, had touched down at RAF Brize Norton in Oxfordshire to attend a nearby airshow the next day.

Bar is also responsible for Israel’s aerial bombardment of Gaza which has devastated the coastal strip and left tens of thousands of Palestinians dead.

Reporter: Phil Miller

24/07/2025
23/07/2025

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ameonesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Miji 28 unaotekelezwa katika Wilaya za Wanging'ombe na Makambako, mkoani Njombe.

Akizungumza katika ziara yake ya kikazi katika maeneo hayo tarehe 22 Julai 2025, Aweso amebaini mapungufu mbalimbali hasa upande wa Mkandarasi, ikiwemo kuchelewesha mradi na kuwepo kwa msimamizi asiyekuwa na sifa za kusimamia mradi.

Amesisitiza kuwa hatua za haraka lazima zichukuliwe dhidi ya wale wote wanaokwamisha utekelezaji wa mradi huo, ili kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma bora ya maji safi na salama k**a ilivyokusudiwa

Waziri Aweso amewaagiza watendaji wa Wizara ya Maji pamoja na Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kutoka Kampuni ya Larsen and Taubro Limited kuhakikisha kuwa kazi inafanyika kwa bidii, usiku na mchana.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Antony Mtaka, amewaasa wakandarasi wazawa, kwa kusema kwamba wanapopata fursa ya kutekeleza miradi mikubwa k**a hii, wanapaswa kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na weledi ili waweze kuendelea kuaminika katika utekelezaji wa miradi ya baadaye.

Aidha, mradi wa maji wa Wanging'ombe na Makambako, ukikamilika, utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 13 za maji kwa siku, hatua ambayo itaboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo hayo.

23/07/2025

Aliyekuwa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), marehemu Anastazia Mwamongi (72), aliyekutwa ameuawa kikatili ndani ya nyumba yake na watu wasiojulikana, amezikwa katika makaburi ya Igeleke, yaliyopo Kihesa Kilolo, Manispaa ya Iringa.

Maziko ya marehemu huyo yamehudhuriwa na mamia ya waombolezaji, wakiwemo wanachama wa CHADEMA ambao walitawala eneo hilo kwa sauti za “No Reforms No Election,” huku wakilaani tukio hilo na kudai haki itendeke juu ya tukio hilo.

Mwili wa marehemu Mama Mwamongi uligundulika tarehe 20 Julai 2025, baada ya watoto wake kupata wasiwasi kufuatia kushindwa kuwasiliana naye kwa zaidi ya siku nne mfululizo.

Hata hivyo, walipofika nyumbani kwake walikuta nyumba imefungwa, hivyo wakatoa taarifa kwa uongozi wa mtaa ambao ulihusisha vyombo vya dola, ndipo mwili wake ulipokutwa ukiwa umefungiwa ndani ya nyumba hiyo.

Akitoa salamu za pole katika maziko hayo, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Iringa Mjini, Frank Nyalusi, amesema kuwa marehemu Anastazia Mwamongi alikuwa ni kiongozi wa mfano kutokana na msimamo na ujasiri wake katika kutetea demokrasia na haki za wananchi.

Marehemu Anastazia Mwamongi alizaliwa Machi 3, 1952. Aliwahi kuwa kiongozi wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) mkoani Iringa akikumbukwa kwa ujasiri wake kisiasa na dhamira ya kuwatumikia wananchi.

Hadi sasa, chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mediawireexpress posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mediawireexpress:

Share