Sbn_tv

Sbn_tv sbn tv

Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 36, atashawishi ahamie kwa mabingwa wa ligi kuu England Manchester ...
27/08/2021

Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 36, atashawishi ahamie kwa mabingwa wa ligi kuu England Manchester City katika wiki hii ya mwisho ya usajili, huku nyota huyo wa zamani wa Manchester United akitamani kutokamilisha mkataba wake wa mwaka mmoja uliosalia na Wataliano hao . (L'Equipe - in French)

-

-

Follow us


Fb | twitter

-
-

                              

Rais mpya wa Zambia Hakainde Hichilema amesema ataanza kutangaza mawaziri wake siku ya Alhamisi.Rais huyo ameandika ujum...
27/08/2021

Rais mpya wa Zambia Hakainde Hichilema amesema ataanza kutangaza mawaziri wake siku ya Alhamisi.

Rais huyo ameandika ujumbe kwenye kurasa wake wa Twitter, kuwa mtu wa kwanza kuteuliwa atakuwa waziri wa fedha:

Bwana Hichilema alichaguliwa kuwa rais mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kumshinda mpinzani wake aliyekuwa rais wa taifa hilo Edgar Lungu, kwa mamilioni ya kura.

Rais huyo amehaidi raia wa Zambia kuboresha uchumi ambao ulikuwa umeshuka.

-

-

Follow us


Fb | twitter

-
-

                              

Mshambuliaji anayeshukiwa kuwa wa kujitoa muhanga amek**atwa nchini Uganda kwa kupanga kujilipua katika mazishi ya k**an...
27/08/2021

Mshambuliaji anayeshukiwa kuwa wa kujitoa muhanga amek**atwa nchini Uganda kwa kupanga kujilipua katika mazishi ya k**anda wa jeshi anayefahamika k**a ‘they lion of Mogadishu’’.

Meja Jenerali Paul Lockech alipewa jina hilo la bandia tangu wakati alipokuwa Mkuu wa kikosi cha Muugano wa Afrika kilichopo nchini Somalia (Amisom) kuanzia mwaka 2000.

Alisifika kwa kuwaondosha wanamgambo wa al-Shabab katika mji mkuu Mogadishu.

Amisom kilisema kuwa itamkumbuka k**a “ mnara wa ishara ya heshima katika mapigano dhidi ya wanamgambo wenye silaha” , na kwamba atakumbukwa k**a urithi ambao hauwezi kusahaulika.

Meja Jenerali Lokech mwenye umri wa miaka 55, ambaye alikuwa anafanya kazi akiwa Inspekta Jenerali wa polisi alifariki kutokana na ugonjwa wa kuganda kwa damu nyumbani kwake siku ya Jumamosi.

Rais Yoweri Museveni amekuwa akitarajiwa kuhudhiria mazishi yake katika wilaya ya kaskani Mwa nchi hiyo ya Pader.

Mshukiwa alik**atwa Alhamisi mchana katika operesheni ya pamoja baina ya maafisa mbalimbali wa usalama.

Msemaji wa jeshi Flavia Byekwaso amesema kuwa alipatikana na zana za kutengeneza mabomu, ikiwa ni pamoja na mabegi ya mabomu, fulana za mabomu ya kujitoa muhanga, na kifaa cha kukata waya wa kulipua mabomu.

Washukiwa wenzake pia wametambuliwa na operesheni bado inaendelea ili kuwapata, alisema.

Haki za wanawake nchini Afghanistan zitaheshimiwa "kulingana na mfumo wa sheria za Kiislamu", Taliban wamesema.Katika mk...
18/08/2021

Haki za wanawake nchini Afghanistan zitaheshimiwa "kulingana na mfumo wa sheria za Kiislamu", Taliban wamesema.

Katika mkutano wa kwanza na waandishi wa habari tangu Taliban walipochukua udhibiti wa nchi ya Afghanistan Jumapili, msemaji alisema wanawake watakuwa huru kufanya kazi lakini akatoa maelezo kidogo juu ya sheria na masharti mengine.

Msemaji wa kundi hilo Zabihullah Mujahid alirudia kwamba Waafghan wote lazima waishi "katika mfumo wa Uislamu".

Hata hivyo, vikundi vya kutetea haki vinahofia uhuru wa wanawake unaweza kukadamizwa tena chini ya Taliban.

Kundi hilo la wapiganaji lilianzisha au kuunga mkono adhabu kulingana na tafsiri yao kali ya mfumo wa sheria ya Kiislam, yaani Sharia, wakati walipodhibiti Afghanistan kati ya 1996 na 2001.

Wanawake walilazimika kuvaa burka inayofunika kila mahali, na Taliban pia hawakukubali wasichana wenye umri wa miaka 10 na kuendelea kwenda shule.

Katika mkutano huo na wanahabari Jumanne, Bw. Mujahid alijibu maswali kadhaa kutoka kwa wanahabari wa kimataifa juu ya haki za wanawake chini ya serikali ya Taliban.

"Tutaruhusu wanawake kufanya kazi na kusoma ndani ya mifumo yetu", alisema.

"Wanawake watakuwa wachangamfu sana katika jamii yetu".

Lakini hakufafanua alipoulizwa juu ya kanuni za mavazi na ni majukumu gani wanawake wataweza kuwa nayo ndani ya nguvukazi ya nchi.

-

-

Follow us


Fb | twitter

-
-

                              

Kanisa la Mhubiri Nigeria Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua limetangaza siku na mahali atakapozikwa.Katika taar...
15/06/2021

Kanisa la Mhubiri Nigeria Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua limetangaza siku na mahali atakapozikwa.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN, lilisema Mhubiri TB Joshua atazikwa karibu na makao yake makuu mjini Lagos.

Mhubiri huyo aliyekuwa na umri wa miaka 57 alifariki Juni 5,2021 siku chache kabla ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

"Tunajiandaa kwa ibada ya kila wiki kukumbuka maisha ya Nabii TB Joshua

TB Joshua, alizaliwa tarehe 12 mwezi Juni 1963 katika mji wa Arigidi huko Aoko kaskazini mashariki mwa jimbo la Kusini magharibi mwa Nigeria.

TB Joshua anajulikana kuwa muhubiri Mkristo anayehubiri katika runinga.

Ndiye mwanzilishi wa kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN ambalo huhubiri moja kwa moja katika runinga ya Emmanuel TV mjini Lagos.

TB Joshua ana makanisa mengi katika mataifa tofauti barani Afrika na Amerika Kusini.

-

-

Follow us


Fb | twitter

-
-

                              

Mhe samia suluhu. ✍️✍️--Follow usFb | twitter--                               
15/06/2021

Mhe samia suluhu. ✍️✍️

-

-

Follow us


Fb | twitter

-
-

                              

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, bwana George Simbachawene amekanusha uwepo wa wakimbizi kusini mwa Tanzania .W...
15/06/2021

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, bwana George Simbachawene amekanusha uwepo wa wakimbizi kusini mwa Tanzania .

Waziri Simbachawane amesema Tanzania kazi yake k**a nchi ni kulinda mipaka yake na kulinda watu wake.

Vilevile ifahamike kuwa katika jumuiya ya kimataifa Tanzania inawahifadhi wakimbizi na waomba hifadhi zaidi ya laki mbili sabini na tano elfu kutoka nchi mbalimbali zilizopata machafuko ya kisiasa au mapigano ya wenyewe kwa wenyewe au sababu nyingine mbalimbali.

"Kazi ya taifa letu katika kulinda mipaka na nchi yake, mpaka wa kusini ambao tuapakana na Msumbiji kuna mikoa mitatu Lindi, Mtwara na Ruvuma, katika mikoa hiyo sisi hatuna wakimbizi kutoka nchi yeyote ila tunafahamu kuwa katika nchi ya Msumbiji jimbo la Cabo Delgado kuna machafuko ambayo yalifanywa na magaidi.

Magaidi wanafanya ghasia katika eneo hilo na hivyo watu wanakimbia katika maeneo mbalimbali, na katika upande wetu sisi si rahisi kuweza kuwachuja kujua huyu mkimbizi au gaidi, maana kwa macho hatuwezi kupima au kuona tofauti yao," Simbachawene amesema.

Aidha aliogeza kusema kuwa Tanzania haijaresha wakimbizi kwa sababu haina wakimbizi kusini mwa nchi yake.

Amesema katika ukanda wa Afrika Mashariki na ukanda wa maziwa makuu, Tanzania inaongoza kwa kuhifadhi wakimbizi na wana uzoefu huo na vilevile wana heshimu sana sheria za kimataifa kwa wakimbizi lakini mpaka sasa hawana wakimbizi wa Msumbiji alisisitiza kwa kusema ... "Hatuna wakimbizi kusini mwa Tanzania sasa tunawafukuza vipi!".

Awali, Mamlaka nchini Msumbiji zimesema kuwa zaidi ya raia 9,600 wa Msumbiji wanaokimbia vurugu kaskazini mwa Jimbo la Cabo Delgado "wamerudishwa kwa nguvu" kutoka Tanzania tangu Januari 2021, Diario de Noticias gazeti binafsi nchini humo limeripoti.

Kulingana na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa karibu watu 900 "walisukumwa kwa lazima" kuvuka mpaka kati ya tarehe 7 na 9 Juni.

Ripoti hiyo inakuja saa chache baada ya manusura walionukuliwa na tovuti inayomilikiwa na watu binafs

-

-

Follow us


Fb | twitter

-
-

                              

Mkuu wa Mkoa SIMIYU, Mhe. David Kafulila ametoa mwezi mmoja kwa wakurugenzi wote kuhakikisha zahati na vituo vyote vya a...
11/06/2021

Mkuu wa Mkoa SIMIYU, Mhe. David Kafulila ametoa mwezi mmoja kwa wakurugenzi wote kuhakikisha zahati na vituo vyote vya afya vinafunga na kutumia mfumo wa malipo( GOTHOMIS).

Ametoa maelekezo hayo wakati alipotembelea kituo cha Afya Mwandoya kilichopo Wilayani Meatu. Katika taarifa ya wilaya hiyo ilibainika kuwa kabla ya kuanza kutumia malipo kwa mfumo, makusanyo kwa mwezi yalikuwa wastani wa Tsh. 400,000/= kulinganisha na wastani wa Tsh. 3,000,000/= baada ya kufunga mfumo.

Aidha kati ya zahanati 47, zilizofungwa mfumo ni zahanati 8 tu. Taarifa hizo zinaonesha kuwa wastan wa mapato kwa zahanati zilizofungwa mfumo mapato yake yameongezeka kutoka Tsh.70,000/- mpaka Tsh. 400,000/-.

-

-

Follow us


Fb | twitter

-
-

                              

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa na kuteua wengine ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhan...
11/06/2021

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa na kuteua wengine ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhandisi Robert Luhumbi anahamia Mkoa wa Mwanza na Albert Chalamla uteuzi wake umetenguliwa.

-

-

Follow us


Fb | twitter

-
-

                              

Rais Samia Suluhu amemuhamisha Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhandisi Gabriel Robert Luhumbi kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza a...
11/06/2021

Rais Samia Suluhu amemuhamisha Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhandisi Gabriel Robert Luhumbi kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akichukua nafasi ya Albert Chalamila ambaye uteuzi wake umetenguliwa, swipe kuona teuzi nyingine.

-

-

Follow us


Fb | twitter

-
-

                              

Rais Samia Suluhu amemuhamisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Hapi kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara akichukua nafasi ya RC ...
11/06/2021

Rais Samia Suluhu amemuhamisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Hapi kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara akichukua nafasi ya RC Gabriel Luhumbi ambaye amehamishiwa Mwanza kuwa RC baada ya uteuzi wa RC Chalamila kutenguliwa.

Katika hatua nyingine Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa RC Tabora akichukua nafasi ya RC Hapi.

Zuwena Omari ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Simanjiro ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga akichukua nafasi ya Batilda, swipe kuona teuzi nyingine.

-

-

Follow us


Fb | twitter

-
-

                              

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20, anapania kujiunga na Chelsea na yuko tayari kusubi...
09/06/2021

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20, anapania kujiunga na Chelsea na yuko tayari kusubiri kwa mwaka mmoja kuhamia Stamford Bridge. (Telegraph, subscription required)

-

-

Follow us


Fb | twitter

-
-

                              

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sbn_tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Sbn_tv:

Share