18/07/2025
Tarehe 18 Julai 1918, ulimwengu ulikuwa katika giza la vita.
Vita ya Kwanza ya Dunia ilikuwa karibu kufika ukingoni…
Lakini siku hiyo hiyo — kijiji kidogo cha Mvezo, Afrika Kusini, kilishuhudia kuzaliwa kwa mtoto wa Kiafrika aliyeandikwa kwenye historia: Rolihlahla Mandela.
Mandela, ambaye baadaye alijulikana k**a Nelson Mandela, alikua katika mazingira ya ubaguzi na dhuluma.
Aliona rangi ya ngozi yake ikigeuzwa hukumu.
Alikua katika taifa ambalo Waafrika walinyimwa haki zao…
Lakini hakukubali kimya. Hakukubali uonevu.
Alichagua kupaza sauti — kwa kalamu, kwa hotuba, na baadaye kwa mapambano.
Kwa hilo, alihukumiwa kifungo cha miaka 27, kwenye gereza la Robben Island.
Lakini hata akiwa kifungoni — Mandela aliendelea kuamini katika ndoto ya Afrika yenye usawa, amani na maridhiano.
Mnamo mwaka 1990, Mandela aliachiwa huru.
Na mwaka 1994 — akawa Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini.
Aliongoza taifa kwa msamaha badala ya kisasi.
Alichagua umoja badala ya kugawanyika kwa chuki.
Leo hii, tarehe 18 Julai, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela.
Siku ya kutafakari thamani ya haki za binadamu, usawa, na msamaha.
Siku ya kujiuliza:
Je, sisi pia tuko tayari kusamehe kwa ajili ya kesho bora?
Mandela alituonesha kuwa shujaa si yule asiyeanguka… bali yule anayesimama tena kila mara akiwa na matumaini.
Tufatilie kupitia YouTube ya FURAHA TV, upate habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika kila siku. Usisahau ku-like, ku-comment, na kusubscribe ili uweze kuendelea kuhabarika na taarifa za uhakika.