16/01/2026
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewak**ata watu watano kwa tuhuma za kumuua kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Hamza Malingumu Hussein (20) katika eneo la Lukobe, Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mk**a, amesema kijana huyo aliuawa baada ya kudhaniwa kimakosa kuwa ni mwizi.
Hata hivyo, familia ya marehemu imeeleza kuwa Hamza alikuwa mgonjwa wa akili na mgeni katika eneo hilo, taarifa ambayo pia imethibitishwa na Jeshi la Polisi.
Mjomba wa marehemu, Ngwenje Mohamed, amesema Hamza, mkazi wa Wilaya ya Kilosa, aliondoka nyumbani kwa mjomba wake mwingine, Nassib Ngwenje, mkazi wa Lukobe, majira ya saa tatu usiku bila kufahamika na watu wa nyumbani, kisha akaanza kuzurura mitaani.
“Baada ya kupata taarifa kuwa amepigwa na kupoteza fahamu akidhaniwa kuwa ni mwizi, tulijaribu kumkimbiza hospitali kwa kutumia bajaji, lakini alifariki dunia akiwa njiani,” amesema Ngwenje.
Jeshi la Polisi limesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea, na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika wote mara uchunguzi utakapokamilika.
Video full ipo YouTube ya Global TV
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.