
16/03/2025
Mwanamke mmoja raia wa Kenya aliyetambulika kwa jona la Margaret Nduta Macharia (37), aliyek**atwa mwaka 2023 nchini Vietnam na dawa za kulevya kilogramu mbili za Co***ne, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025.
VN Express inaripoti kwamba Nduta, 37, alikuwa ameajiriwa na mwanamume mmoja nchini Kenya kusafirisha koti hadi Laos, nchi iliyoko Kusini-mashariki mwa Asia. Aliagizwa kupeleka mizigo kwa mwanamke huko Laos na kurudi na 'bidhaa' ambazo hazijatajwa.
Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika viwanja vitatu vya ndege bila kuk**atwa, kabla ya kugundulika Vietnam. Viwanja hivyo ni; Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar).
Hata hivyo, Margaret akijitetea mahak**ani nchini Vietnam alidai hakufahamu k**a mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za usiku.
Sheria ya Vietnam inasema nini kuhusu hukumu ya kifo?
Siku ya Alhamisi, Machi 6, mahak**a ya Watu wa Jiji la Ho Chi Minh ilimhukumu kifo Nduta, ikiimarisha sera ya Vietnam ya kutovumilia kabisa makosa yanayohusiana na dawa za kulevya.
Chini ya mfumo wa kisheria wa nchi, watu wanaopatikana na hatia ya ulanguzi wa dawa za kulevya wanakabiliwa na baadhi ya adhabu kali zaidi duniani, ikiwa ni pamoja na kifungo cha muda mrefu au adhabu ya kifo, kulingana na ukubwa wa uhalifu.
Baada ya hukumu ya kifo kutolewa nchini Vietnam, mfumo wa kisheria hutoa mchakato wa mapitio ya kina kabla ya kutekelezwa. Kwa kawaida, kesi huchunguzwa kwa mara ya kwanza na Mahak**a ya Juu ya Watu na Utawala Mkuu wa Watu, ambayo ina hadi miezi miwili kutathmini rufaa yoyote ya kipekee.
Tena, mtu aliyepatikana na hatia ana siku saba za kumwomba Rais wa Taifa amuhurumie. Juhudi hizi zisipofaulu, utekelezaji umeratibiwa, ingawa ratiba ya matukio inatofautiana kulingana na mambo ya kisheria na maelezo mahususi ya kesi.
Credit by