Bongo5.com

Bongo5.com The leading entertainment website in Tanzania, since 2006! Follow us on twitter http://twitter.com/bongofive and on YoutTube http://youtube.com/bongofive
(2)

Bringing you the latest scoops, gossip and news from Tanzania. You can send us your stories and photos to the email [email protected]

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT Wazalendo Luhaga Mpina, Mgombea Mwenza wa Urais wa...
09/08/2025

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT Wazalendo Luhaga Mpina, Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Fatma Ferej na Mgombea wa Urais wa Zanzibar Ndugu Othman Masoud Othman wamepokelewa na maelfu ya wanachama wa ACT Wazalendo na wananchi wa Zanzibar.

Wanachama hao wapo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha upande wa Unguja leo tarehe 9 Agosti 2025.

Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt....
09/08/2025

Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Begi lenye Fomu zake za kugombea nafasi hiyo mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahak**a ya Rufani Jacobs Mwambegele katika Ofisi za Tume hiyo Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 09 Agosti, 2025.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kuanza kwa zoezi la ukaguzi wa mita za wateja nchini ili kudhibiti mapat...
09/08/2025

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kuanza kwa zoezi la ukaguzi wa mita za wateja nchini ili kudhibiti mapato na kubaini wateja wasio waaminifu wanaotumia umeme bila kulipia.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na huduma kwa wateja wa TANESCO Irene Gowelle wakati akizindua Ofisi ya Huduma kwa Wateja ya Kinondoni Kusini, iliyoko Kibamba, ikiwa ni jitihada za kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma na kusogea karibu zaidi na wananchi.

“Tumekuwa na changamoto ya upotevu wa mapato kutokana na mita zisizofanya kazi vizuri kutokana na umri lakini pia wako baadhi ya wateja ambao si waaminifu wamekua wakichezea mita kuiba umeme sasa zoezi hili litahakikisha tunazikagua mita hizo na kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale watabainika ni wezi wa umeme” alisisitiza Gowelle

Pamoja na hayo ametoa rai kwa wananchi na wateja kutumia mfumo wa utoaji taarifa za siri uliozinduliwa hivi karibuni kuwabaini na kuwafichua wale wote wanaolihujumu shirika kwa kuiba umeme na kuwahakikishia usalama wao na ulinzi kwa watoa taarifa.

Katika hatua nyingine Gowelle, amepongeza uongozi na wafanyakazi kwa wa Mkoa wa Kinondoni kusini kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kuboresha mazingira mazuri ya ofisi hiyo.

“Uwepo wa ofisi hii mpya ni hatua muhimu katika kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi. Matatizo ya wateja sasa yatatatuliwa kwa haraka zaidi kwa kuwa tumesogeza huduma karibu nao,” alisema Gowelle.

Aidha Gowelle amesisitiza matumizi sahihi ya umeme k**a nishati salama na rafiki kwa mazingira katika shughuli za kupikia, akihamasisha wananchi kuunga mkono kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kupikia kwa gharama nafuu.

Ametoa rai kwa wafanyakazi wa Ofisi hiyo kuipenda na kuitunza kwa uaminifu, sambamba na kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi. Pia alisisitiza kuimarishwa kwa ushirikiano baina ya idara ya ufundi na idara ya huduma kwa wateja, pamoja na kuendeleza utoaji wa elimu ili kuboresha zaidi huduma kwa wananchi.

Marioo anazidi kupasua anga, Spotify msanii namba Tatu kwa Streams wasanii wa Tanzania.Credit by
08/08/2025

Marioo anazidi kupasua anga, Spotify msanii namba Tatu kwa Streams wasanii wa Tanzania.

Credit by

LIGI NA MICHUANO HII ITAONEKANA DStv PEKEE, SEHEMU ZINGINE MARUFUKU.Taarifa kwa Umma:- “Ligi Kuu Uingereza, UEFA na mich...
08/08/2025

LIGI NA MICHUANO HII ITAONEKANA DStv PEKEE, SEHEMU ZINGINE MARUFUKU.

Taarifa kwa Umma:- “Ligi Kuu Uingereza, UEFA na michuano hii Itaonekana katika Kisimbuzi cha pekee na sio sehemu nyingine ile.

Swipe kuona Orodha yote

AGCOT Yashinda Kombe la Mshindi wa Kwanza Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki 2025 kwa Taasisi Isiyo ya KiserikaliA...
08/08/2025

AGCOT Yashinda Kombe la Mshindi wa Kwanza Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki 2025 kwa Taasisi Isiyo ya Kiserikali

AGCOT imetunukiwa kombe la mshindi wa kwanza kwa taasisi zisizo za kiserikali kwenye Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mwaka 2025, k**a ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika kutoa elimu kwa wakulima, wafugaji, na wavuvi.

Tangu siku ya kwanza ya maonesho haya yaliyofanyika katika viwanja vya Nanenane, Morogoro, AGCOT imekuwa ikiongoza kwa ubunifu na umahiri katika utoaji wa mafunzo mbalimbali ya kilimo, kiuchumi, uhifadhi wa mazao baada ya mavuno, teknolojia rafiki kwa mazingira, pamoja na fursa za masoko na mitaji kwa wakulima.

Banda la AGCOT limejizolea umaarufu kwa kuwa darasa wazi kwa wadau wa kilimo waliotembelea, ambapo wataalamu mbalimbali waliwepo kutoa elimu na kujibu maswali ya washiriki kwa kina na kwa wakati. Ushiriki wa AGCOT umeonyesha namna taasisi binafsi zinavyoweza kuwa kichocheo cha maendeleo endelevu katika sekta ya kilimo nchini.

Kupitia Instagram yake ameandika kuwa:  “Nimekuwa nikijaribu kukaa kimya kwa muda...Lakini kila unapojaribu kuzungumza v...
08/08/2025

Kupitia Instagram yake ameandika kuwa: “Nimekuwa nikijaribu kukaa kimya kwa muda...

Lakini kila unapojaribu kuzungumza vibaya kuhusu jina langu au brand yangu, naona k**a unanidharau au kuniona mjinga.
Kaka, jina hili nimeshalitafuta kwa jasho na damu.

Haikuwa rahisi kufika hapa. Sifanyi vitu kwa kiki.
Kila siku napambana kuwa bora zaidi ya jana.
Ndoto zangu ni kubwa, na nazihusisha moja kwa moja na kipaji nilichopewa na Mungu.

Najua umetumwa kuniharibia jina, kuharibu image yangu mbele ya watu.

Lakini niambie - utamshinda vipi mtu ambaye haishi kwa kiki, bali kwa ndoto zake?
Mimi ni imara.

Na kwa uwezo wa Mungu, hutaweza kuniangusha.

Credit by

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua Maabara Kuu ya Kilimo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima, Wafugaji...
08/08/2025

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua Maabara Kuu ya Kilimo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) ambayo kitaifa inafanyika mkoani Dodoma.

Spika Tulia, Lukuvi, Simbachawene, Stergomena waifariji familia ya Ndugai Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Dun...
08/08/2025

Spika Tulia, Lukuvi, Simbachawene, Stergomena waifariji familia ya Ndugai

Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk. Tulia Ackson, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax wamefika nyumbani kwa marehemu Spika Mstaafu Job Ndugai na kutoa pole kwa familia.

Mawaziri wengine waliofika nyumbani hapo na kutoa pole ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu William Lukuvu pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, George Simbachawene.

Marehemu Ndugai amefariki dunia Agosti 6, mwaka huko jijini Dodoma wakati akipatiwa matibabu.

Address

Dar Es Salaam
23207

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bongo5.com posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Bongo5.com:

Share