21/12/2023
MFAHAMU KOUASSI ATTOHOULA.
๐ Jina kamili: KOUASSI ATTOHOULA.
โWatu wa nyumbani kwao wanapenda kumuita kwa jina la KOUASSI ATTOHOULA YAO.
โRaia wa Ivory coast...Alizaliwa Anyama,Ivory coast
mnamo Dec 20,1996 (LEO BIRTHDAY YAKE) (Age 27)
๐กAna urefu wa 1.68m.
โWakala :VV Consulting.
โฌ Nafasi anayochezea ni beki wa kulia... Nafasi nyingine anayoweza kucheza ni beki wa kushoto/winga.
Alianza maisha ya soka kwenye akademi ya Mimosas na kuitumikia akademi hiyo kwenye vikosi vya U17 na U19.
โ
Julai 1,2017 akasajiliwa na klabu ya Williamsville ya nchini humo akitumikia kwa miaka miwili.
โ
Akauzwa kwenda klabu ya O.Khouribga ya nchini Morocco Jan 16,2019 aliitumikia kwa miezi 6 kisha akatolewa kwa mkopo kwenda kwenye klabu ya Kawkab Marrak mnamo Julai 17,2019.
โ
Mnamo Sep 15,2019 baada ya mkataba wa mkopo kuisha alirejea kwenye klabu yake ya O.Khouribga.
Na mkataba wake ndani ya klabu hiyo uliisha miezi miwili baade.
โ
๐กNdipo akajiunga tena na klabu ya Asec Mimosas ya Wakubwa Nov 9,2020.
Akiwa ligi ya Morocco alicheza mechi 9 na kufunga goli 1.
๐จAug 27 mwaka jana akiwa na umri wa miaka 25,miezi 8 na siku 7 alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast chini ya kocha Jean Louis Gasset.
Mpaka sasa ameichezea hiyo ya taifa (michuano ya CHAN,na timu ya taifa ya pamoja) michezo 6.
โAliwahi kuwa beki bora wa msimu wa ligi kuu Ivory Coast 2021/22.
๐ข Alikuwa miongoni kwa walioiunda kikosi bora cha msimu ligi kuu ya Ivory Coast kwenye msimu wa 2021/22 na msimu uliopita wa 2022/23
๐๐ Mshindi wa Makombe mawili ya Ligi kuu Ivory Coast
๐๐ Mshindi wa Makombe mawili ya FA.
HAPPY BIRTH DAY BEKI WA KUPANDA NA KUSHUKA.