15/01/2026
✍️ Anaandika Cheyo Lutengeno tz
Yanga SC wamemtambulisha Laurindo Maria 'Depu' kuwa mchezaji wao mpya wa klabu hiyo.
Huu usajili wa tatu kwa Yanga SC msimu huu wakiendelea kuziba magap, Depu ni raia wa Angola aliyekuwa Radomiak Radom bado umri wa kuhesabu miaka 25 pekee.
Amewahi kukanyaga viunga vya Petro de Luanda na Sagrada Esperança za Angola, Gil Vicente ya Ureno, Vojvodina ya Serbia kabla ya kuwatumiakia Radomiak Radom ya Poland.
Una Prince Dube mtaftaji anaweza kucheza pembeni na hata nyuma ya mshambuliaji wa mwisho kwa sababu ya uwezo wa kuchezea mpira.
Una Mzize winga unaweza mtumia k**a mshambuliaji wa mwisho anakupa nguvu, kupiga mbali, kukaba, pasi na magoli.
Then una Dilson Mario uzoefu pale juu, ujuzi wa kufunga magoli magumu na mepesi, kasi, anakupa pressing kutoka kwenye buld up za wapinzani nguvu na magoli.
Follow Kijiweni24 Tv