Rabbi Media Group

Rabbi Media Group Rabbi Media Group
>Rabbi Television tunapatikana kwenye kisimbuzi cha Startimes antena na Azam Dish

Full Time mchezo umeisha kwa nchi ya Ujerumani kufunga mabao matatu dhidi ya Scotland.
14/06/2024

Full Time mchezo umeisha kwa nchi ya Ujerumani kufunga mabao matatu dhidi ya Scotland.

Mchezo umeisha kwa timu ya Tanzania kuifunga Zambia bao moja hakika kombe la dunia tutaenda.
11/06/2024

Mchezo umeisha kwa timu ya Tanzania kuifunga Zambia bao moja hakika kombe la dunia tutaenda.

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya utenguzi na uteuzi wa nafasi mbalimbali ambapo amemteua Kenan Laban K...
11/06/2024

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya utenguzi na uteuzi wa nafasi mbalimbali ambapo amemteua Kenan Laban Kihongosi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, kabla ya uteuzi huo Kihongosi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba na anachukua nafasi ya Dkt. Yahaya Ismail Nawanda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Pia amemteua Christopher Magala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara akichukua nafasi ya Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Rais Samia amemteua pia Elias Daniel Mwandobo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, kabla ya uteuzi, Mwandobo alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu na pia Rais Samia amemteua George Hillary Herbert kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, kabla ya uteuzi, Herbert alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani.

Uapisho wa Mkuu wa Mkoa na Msajili wa Mahakama ya Rufani utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA kuhusu nauli za abiria wa...
11/06/2024

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA kuhusu nauli za abiria wa daraja la kawaida kwa Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora baada ya kufanyia kazi maombi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na maoni ya Wadau wengine ambapo Dar es salaam hadi Morogoro (KM 192) nauli ni Tsh. 13000 na Dar es salaam hadi Dodoma (KM 444) nauli ni Tsh. 31000.

“Nauli hizi ni kwa daraja la kawaida kwa Watu wazima na Watoto kuanzia umri wa miaka 4 hadi 12 ambapo nauli zitalipwa na abiria kwa kilomita, nauli itakayolipwa na Mtu mzima na Mtoto mwenye umri zaidi ya miaka 12 ni Tsh. 69.51 kwa kilomita, na Mtoto kuanzia kuanzia miaka 4 hadi 12 atalipia Tsh. 34.76 kwa kilomita”

“Mtoto mwenye umri wa chini ya miaka minne (4) hatolipa nauli, hata hivyo taarifa zao na Wasafiri
wote zitatunzwa kwenye mfumo wa tarifa za abiria wanaosafiri kila siku”

Magazetini leo Juni 11.
10/06/2024

Magazetini leo Juni 11.

Magazetini leo Juni 10 hapa Rabbi Tv.
09/06/2024

Magazetini leo Juni 10 hapa Rabbi Tv.

Wakati sakata la uongozi likiendelea katika klabu ya Simba SC na aliyekuwa CEO wa klabu hiyo Babra Gonzalenz kuwa  anahu...
08/06/2024

Wakati sakata la uongozi likiendelea katika klabu ya Simba SC na aliyekuwa CEO wa klabu hiyo Babra Gonzalenz kuwa anahusishwa kurejea kwenye nafasi yake ya awali ikiwa ni timu mpya ya uongozi anaoupanga Mwekezaji wa klabu hiyo Mo Dewji licha ya taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba SC kuthibitisha kuwa Babra hatorejea kwenye nafasi hiyo.

Babra amekuwa akiandika jumbe mbalimbali kupitia mtandao wake wa X (Twitter) na kuonekana kuwa hajapendezwa na jambo hilo la yeye kuzushiwa kutaka kurudi katika klabu hiyo.

Je, unadhani ni wakati sahihi Babara kurejea Simba SC?

Magazetini leo juni 8.
07/06/2024

Magazetini leo juni 8.

Lile pambano kubwa kabisa kati ya Mike Tyson na Jake Paul limepelekwa mbele na sasa litakuwa November 15 mwaka huu na li...
07/06/2024

Lile pambano kubwa kabisa kati ya Mike Tyson na Jake Paul limepelekwa mbele na sasa litakuwa November 15 mwaka huu na litaonyeshwa live kupitia Netflix.

Pambano hili lilikuwa lifanyike mwezi ujao lakini kutokana na Mike Tyson kuugua ghafla wakati akiwa kwenye ndege pambano hili likahairishwa mpaka pale tarehe mpya itakapotangazwa ambayo ni November 15.

Klabu ya Singida Black Stars imeingia makubaliano na aliyekuwa kocha wa zamani wa Simba Sport Club, Patrick Aussems raia...
07/06/2024

Klabu ya Singida Black Stars imeingia makubaliano na aliyekuwa kocha wa zamani wa Simba Sport Club, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji kuwa kocha mkuu kwa mkataba wa msimu mmoja.

Aussems amefundisha baadhi ya timu mbalimbali Afrika zikiwemo Simba SC, Al Hilal ya Sudan na AFC Leopards ya Kenya.

Messi anasema kuwa Real Madrid ni timu bora, je unakubaliana naye?
07/06/2024

Messi anasema kuwa Real Madrid ni timu bora, je unakubaliana naye?

Ni siku saba tu ndio zimebaki kuelekea
07/06/2024

Ni siku saba tu ndio zimebaki kuelekea

Address

Dominay Poin
Dar Es Salaam
16109

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Rabbi Media Group posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Rabbi Media Group:

Share