
03/07/2025
Mchezaji wa Klabu ya Liverpool, Diogo Jota amefariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea kwenye Jimbo la Zamora nchini Hispania.
Taarifa zinasema ajali hiyo imetokea baada ya gari walilokuwa wakisafiria Jota na kaka yake André (26) ambaye naye ni mchezaji wa soka wa kulipwa kuacha njia na kuwaka moto.