sijo_august

sijo_august Goods available in Geita and Dar es salam, but deliverly are made wherever you are

Ukifika pale Italia, kuna sehemu ndogo ya nchi, inaitwa Vatican.Hapo ndipo yalipo makao makuu ya Kanisa la Roman Catholi...
28/06/2025

Ukifika pale Italia, kuna sehemu ndogo ya nchi, inaitwa Vatican.

Hapo ndipo yalipo makao makuu ya Kanisa la Roman Catholic.
Vatican wana jeshi lao special linaitwa Swiss Guards

Pale Italia wana pesa yao, ila haitumiki ukiingia Vatican. Kule Vatican wana pesa yao na unaweza kuitumia Italy.

Rais wa Italia, Bwana Sergio Mattarella hana mamlaka katika serikali ya Vatican, ila Papa ana mamlaka makubwa katika serikali ya Italia.

Mtu wa Vatican anahesabika ni Muitaliano pia, ila Muitaliano haesabiki k**a Mvatican.

Vatican wana jeshi lao linaitwa Swiss Guard ni kikosi maalum cha kijeshi kinacholinda Papa na makazi yake katika Vatican.

Kikosi hiki kilianzishwa rasmi tarehe 22 Januari 1506 na Papa Julius II, na ni mojawapo ya vikosi vya kijeshi vya zamani zaidi vinavyoendelea kufanya kazi duniani.

Polisi wa Italia wakienda Vatican, kuna sehemu hawatakiwi kukanyaga kabisa, yaani wamewekewa mipaka ya kuvuka nchini humo.

Vatican ina raia 800 tu!

Vatican hakuna hospital, so hakuna suala la kusema umepata uraia kwa kuzaliwa. Wao washajiwekea ni watu 800 tu.

Akifa mmoja, analetwa mwingine.

Hapo Vatican kuna museum 70,000 ambapo utaangalia historia za sehemu mbalimbali. Wana vitabu vya historia ya kila taifa duniani. So wanazijua nchi zote mpaka serikali zake. Na kwa siku hupokea watalii 25,000.

Vatican ina miaka 95 tu tangu alianzishwe.

Ndani ya Vatican, kuna maeneo mtu mwenye tattoo haruhusiwi kuingia.

Papa halipwi ila Vatican huingiza mapato ya dola milioni 300 kwa mwaka ambazo hutumika kwa ajili ya chakula, pesa kidogo kwa papa na kugharamia safari zake.

Wanajeshi kutoka nchini Uswisi ndio wanaoilinda Vatican.

Vatican haizitambui nchi mbili tu duniani, China na Korea Kaskazini.

Benki ya Vatican inamiliki assets ya dola bilioni 64.

ITAENDELEA

Timu ya watafiti wa bahari ikiongozwa na Dr Amina mtaalamu wa bahari mwenye asili ya Kenya na Ujeruman inaanza opereshen...
26/06/2025

Timu ya watafiti wa bahari ikiongozwa na Dr Amina mtaalamu wa bahari mwenye asili ya Kenya na Ujeruman inaanza operesheni.

Ili kuchunguza ndani ya sehemu ya chini kabisa ya kifusi cha meli ya Titanic ambako sonar zote zimewahi kufeli hadi sasa.

Ghafla wana sikia sauti ya ajabu mawimbi ya sauti yaliyorekodiwa kwa frequency isiyoeleweka.
Sauti hiyo inaonekana k**a nyimbo za Kilatini zilizopotoshwa, na maneno yanasikika k**a hivi "Kifo si mwish9 bali ni mlango"

Sauti hiyo inasikika kutoka chumba cha mizigo cha Titanic kilichozama kwa mwinuko usiotambulika eneo ambalo hakuna roboti aliyewahi kuingia na kurudi salama.

Wakiwa ndani ya ROV–Orpheus, roboti yenye akili bandia wanagundua lango la chuma la kale lenye nembo ya jicho lililochorwa juu ya mduara wa nyota nane ishara zisizokuwa sehemu ya Titanic.

Dr. Amina anafananisha alama hizo na maandiko ya kale ya Corpus Hermeticum, mafundisho ya siri ya kale kutoka Misri na Ugiriki, ambayo haikuwahi kufikiriwa kuwa yamefika kwenye karne ya 20.

Ndani ya chumba hicho, wanakuta sanduku la shaba limefungwa na misumari ya fedha na karatasi ya ngozi imefungwa ndani yake, ikiwa na maneno yafuatayo “Codex Abyssi – Usisome hadi utazame ndani ya nafsi yako.”

Wakiwasiliana na wakuu wa NASA, wanapewa jina la mtu aliyejaribu kulifikia eneo hilo mwaka 1997 kupitia expedition ya kisiri Profesa Lucien Bastet, mfaransa aliyeamini Titanic ilikuwa si meli tu bali chombo cha kificho kilichobeba vitu vya kale vilivyotolewa Misri.

Lucien alipotea – lakini daftari lake linapatikana katika soko la kale London. Linasema Chumba cha 13 kilibeba ‘Kitu’ kilichoibiwa kutoka Hekalu la Alexandrian. Wakuu wa meli walijua. Walificha. Na kilizama nao.

ITAENDELEA

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255744246410

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when sijo_august posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to sijo_august:

Share