AbedikhalfanGroup

AbedikhalfanGroup Habarika hapa kila siku nakila saa ofisi yetu ipo wazi masaa 24 Abedikhalfangroup we are the best

SAID Ntibanzokiza, ‘Saido’mambo yake yalikuwa magumu mbele ya Biashara United kwa kushindwa kumtungua kipa namba moja wa...
17/02/2022

SAID Ntibanzokiza, ‘Saido’mambo yake yalikuwa magumu mbele ya Biashara United kwa kushindwa kumtungua kipa namba moja wa Biashara United, James Ssetuba jambo lililofanya kila muda awe anajisikitia anapokosa nafasi.

Inaelezwa kuwa Hospitali ya Chuo Kiku cha Aga Khan imefanikisha upandikizaji wa kwanza wa uume katika kanda ya Afrika ma...
17/02/2022

Inaelezwa kuwa Hospitali ya Chuo Kiku cha Aga Khan imefanikisha upandikizaji wa kwanza wa uume katika kanda ya Afrika mashariki na kati

Uongozi wa Hospitali hiyo umesema Upasuaji huo maalum umefanywa kwa mwanaume mwenye miaka kati ya 40 ambaye alikuwa na hali ya maumbile nyeti kushindwa kuwa tayari kushiriki tendo la ndoa

Tatizo hilo ambalo kitaalamu linaitwa Erectile dysfunction (ED) inaelezwa kuwa limemsumbua kwa miaka kadhaa.

MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spot Xtra Alhamisi.
17/02/2022

MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spot Xtra Alhamisi.

Tanzania kuanza kutengeneza chanjo ya coronaRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali yake inataka kuan...
17/02/2022

Tanzania kuanza kutengeneza chanjo ya corona

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali yake inataka kuanzisha kiwanda cha utengenezaji wa chanjo k**a njia moja ya kutimiza mipango ya serikali ya kukabiliana na ugonjwa wa corona na magonjwa mengineo.

Akizungumza na Rais wa baraza la Ulaya, Bwana Charles Michel huko Brussels hapo juzi, alisema kuwa Tanzania inataka kuwa muuzaji wa chanjo za kuokoa maisha kwa jamii ya Afrika Mashiriki (EAC) na nchi washirika wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Msimamo wa Tanzania kuhusu ushirikiano wa kibiashara wa EUTanzania imetupilia mbali madai ya uwezekano wa makubaliano ya...
17/02/2022

Msimamo wa Tanzania kuhusu ushirikiano wa kibiashara wa EU

Tanzania imetupilia mbali madai ya uwezekano wa makubaliano ya masharti ya Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Katika taarifa yake, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara nchini humo inashikilia kuwa itaridhia tu mkataba wa kibiashara baada ya masuala ambayo hayajakamilika kushughulikiwa kwa manufaa ya nchi na ukanda wa Afrika Mashariki.

Mwanamke wa Uganda atolewa figo bila kujua kwa mwajiri wake Saudi ArabiaMadaktari nchini Uganda wamethibitisha kuwa mwan...
17/02/2022

Mwanamke wa Uganda atolewa figo bila kujua kwa mwajiri wake Saudi Arabia

Madaktari nchini Uganda wamethibitisha kuwa mwanamke aliyekuwa akifanya ya nyumbani nchini Saudi Arabia, aliondolewa figo yake ya kulia na sio ajali ya gari k**a ilivyoarifiwa awali na mwajiri wake.

Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imethibitisha hilo, baada ya kupewa ripoti ya uchunguzi kutoka Hospitali kuu ya kitaifa ya Mulago.

Rais wa   Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ...
16/02/2022

Rais wa Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu leo Februari 16, 2022 katika Jiji la Brussels nchini Ubelgiji.

Wana Simba mpooo au vipi
16/02/2022

Wana Simba mpooo au vipi

Auawa kwa kukatwa mapanga na binamu yakeMwanafunzi wa darasa la 7 shule ya msingi Mwenge manispaa ya Morogoro, Faidhati ...
16/02/2022

Auawa kwa kukatwa mapanga na binamu yake

Mwanafunzi wa darasa la 7 shule ya msingi Mwenge manispaa ya Morogoro, Faidhati Ibrahim (13), ameuawa kwa kukatwa na mapanga na binamu yake Shomari Malima, akiwa nyumbani kwao mtaa wa Tambukareli, huku sababu ikitajwa ni ugomvi wa kifamilia kati ya mama wa marehemu na mama wa mtuhumiwa.

Pundamilia ' Ndasiata' ualbino ameonekana Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mapema Februari mwaka huu.Hivi karibuni kumekuwa...
16/02/2022

Pundamilia ' Ndasiata' ualbino ameonekana Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mapema Februari mwaka huu.

Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wanyama wenye rangi za kuangaza ambapo ualbino ndio sababu ya kawaida ya muonekano huo.

Wakati, pumbamilia maarufu Tira ambaye pia alionekana Kenya na Tanzania alikuwa na rangi nyeusi iliyozidi na sasa anaendelea vizuri katika maeneo ya Serengeti, Tanzania ambako inaaminika kuwa ndio nchi yake ya asili.

Hatma ya Mbowe na wenzake kujulikana IjumaaYa wiki hii
15/02/2022

Hatma ya Mbowe na wenzake kujulikana Ijumaa

Ya wiki hii

Fahamu faida za Kitunguu Maji mwiliniKitunguu maji ni aina ya mboga yenye harufu kali inayochangamsha mwili. Pia kitungu...
08/06/2021

Fahamu faida za Kitunguu Maji mwilini

Kitunguu maji ni aina ya mboga yenye harufu kali inayochangamsha mwili. Pia kitunguu ni kiungo ambacho kina virutubisho katika vyakula na kuvifanya viwe na ladha nzuri.

Nchi mashuhuri na maarufu inayolima kiungo hicho ni Misri na kusambaa zaidi duniani na nchini Tanzania kinalimwa zaidi katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Arusha na mikoa mingine ambayo ina rutba nzuri ya kustawisha kiungo hicho.

Kiungo hicho kimekuwa kikitibu na kuponya maradhi mbalimbali kutokana na kuwa na salfa ambayo ni nzuri, hasa kwenye ini na husaidia kuponya kansa kwenye utumbo na kinywa kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya vitamini C.

Kitunguu maji kina kazi nyingi katika mwili wa binaadamu, kwani hutibu magonjwa mbalimbali, ikiwemo kikohozi, vidonda vya tumbo na mifupa, ngozi koo, figo, tumbo na mkojo, kufunga hamu ya kula, hutia kiu na hulainisha tumboni.

Pia, kitunguu maji ni chanzo cha madini mengi ambayo yanapatikana katika kiungo hicho ambayo yana umuhimu mkubwa katika mwili wa binaadamu.

Licha ya kuwa na umuhimu huo, pia huimarisha afya ya moyo, kuzuia kansa, huukinga mwili dhidi ya vidonda vya tumbo, huongeza joto mwilini na huzuia vimelea vya magonjwa mbalimbali katika mwili wa binaadamu.

Faida za kitunguu maji katika mwili wa binaadamu ni pamoja na kuupa mwili nishati, kuongeza nguvu, huimarisha misuli ya mwili, huongeza hamu ya kula, hulainisha tumbo na kuondoa tatizo la kukosa choo.

Pia faida nyingine ya kitunguu ni kuwa kinatibu pumu, uvimbe wa pafu, saratani, majipu, mvilio wa damu, kufungua choo, kupunguza uzito na chunusi.

Kitunguu maji kinaweza kutengenezewa juisi kwa kukikatakata ma kisha kukisaga kwa blenda kwa kuchanganya na maji ya kunywa mara unapojisikia vibaya hasa kwa watu ambao wanasumbuliwa na kifua mara kwa mara.

Pia unaweza kuchanganya na asali na kunywa nayo inasaidia kwa kiasi kikubwa kutibu maumivu ya tumbo na uvimbe mwilini. Maji ya kitunguu kwa mujibu wa wataalamu wa tiba wanasema yanatibu matatizo ya macho

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AbedikhalfanGroup posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share