26/09/2025
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) wameondoka ukumbini wakati Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akihutubia jijini New York. Hatua hiyo ilikuwa ishara ya kupinga mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza.
Tukio hili si la kwanza, kwani mara kadhaa katika miaka iliyopita wajumbe wamewahi kususia hotuba za Netanyahu wakionesha kutoridhishwa na sera za Israel dhidi ya Wapalestina.
Mwaka huu Gaza na Palestina zimekuwa ajenda kuu ya mjadala wa UNGA, ambapo mataifa mengi yameunga mkono kusitishwa kwa vita na kutambuliwa rasmi kwa taifa la Palestina.
Je, unadhani misimamo k**a huu wa kususia hotuba za Israel unaweza kweli kuleta mabadiliko na nafuu kwa Wapalestina? Tuambie maoni yako.