
29/11/2023
Ikiwa ni siku 3 tu tarehe 26 novemba kamphuni ya mabasi ya baraka classic bus, linalofanya safari zake Kati ya wilaya ya Tandahimba Mtwara na Dar es salaam kufeli breki na kuua watu 14.
Leo 29 novemba, watu 13 wameripotiwa kufariki dunia, huku wengine 25 wakijeruhiwa katika ajali ya basi iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Allys Star lenye namba za usajili T 178 DVD, baada ya basi hilo kugonga kichwa cha treni, katika eneo Manyoni, mkoani Singida.