
02/06/2025
Staa mpya wa Wydad Casablanca Stephane Aziz Ki ataweka historia katika maisha yake ya soka kwa kucheza Kombe la Dunia la Vilabu ambalo litaanza Juni 15 mwaka huu.
Wydad ni moja ya timu za Afrika ambazo zinashiriki michuano hiyo sambamba na Esperance,Al Ahly na Mamelodi Sundowns.
Timu hiyo kutoka Morocco itaanza kampeni ya kusaka taji hilo kwa mchezo wao wa kwanza wa Juni 18 dhidi ya Manchester City ambao utawakutanisha Stephane Aziz Ki na Erling Haaland.